Saturday, July 16, 2016

Watu watano washikiliwa na polisi kwa kupanga shambulizi la kigaidi nchini Ufaransa

Polisi nchini Ufaransa wanasema watu watano wanaoshukiwa kupanga tukio la mtu aliyewagonga watu mjini Nice na kusababisha vifo vya watu 84 siku ya Alhamisi usiku, wanazuiliwa.
Gazeti la Le Monde limeripoti kuwa, polisi walifanikiwa kuwakamata washukiwa hao siku ya Jumamosi huku wawili wakitiwa mbaroni siku ya Ijumaa.


Aidha, imebainika wazi sasa kuwa Mohamed Lahouaiej-Bouhlel mwenye asili ya Tunisia, ndiye aliyeliendesha Lori hilo na kutekeleza mauaji hayo kabla ya kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Kundi la Islamic State limedai kuwa dereva wa lori hilo alikuwa ni mfuasi wao.
Jaber: Kaka wa mshambuliaji aliyeuwa watu 84 kwenye
shambulizi la Nice, nchini Ufaransa.

Serikali nchini humo imetangaza kuongeza muda wa hali ya hatari nchini humo kwa  miezi mitatu zaidi kwa sababu za kiusalama.
Rais Francois Hollande aliyetaja tukio hilo kama la kigaidi, leo Jumamosi anaongoza kikao cha dharura kuhusu kilichotokea siku ya Alhamisi usiku mjini Nice.

No comments:

Post a Comment