Kwa Kijerumani meli hii ilijulikana kama Graf von Götzen, ilipewa jina hili kwa heshima ya Gustav Adolf van Götzen, mpelelezi wa Kijerumani na gavana wa Afrika Mashariki ya Ujeruman ( German East Africa ). Inapatikana Mkoani Kigoma, Magharibi wa Tanzania na inajulikana kwa jina Maarufu la MV Liemba.
Ilitengenezwa na kampuni ya Meyer Werft mojawapo ya makampuni makubwa ya utengenezaji meli nchini Ujerumani yenye makao yake katika mji wa Papenburg, jimbo la Lower Saxony, kaskazini magharibi ya Ujerumani.Ilizinduliwa rasmi tarehe 5 February 1915. Ina urefu wa mita 71.4 sawa na futi 234.25.
Meli hii ambayo hufanya safari zake Ziwa Tanganyika licha ya kubeba abiria na mizigo yao, pia imebeba historia na kivutio kikubwa cha utalii. Inamilikiwa na Shirika la Reli la Tanzania, hufanya safari zake kuelekea Mpulungu, Zambia na Kassanga, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ni miongoni mwa meli chache duniani kuishi na kuendelea kufanya kazi kwa karibu karne nzima sasa. Mwaka jana, meli hii ya Liemba ilitimiza miaka 100, sawa na karne tangu ianze kufanya safari zake kwenye Ziwa Tanganyika.
Thamani na umaarufu wake viliongezeka baada ya historia yake kuchapishwa kwenye jarida Maarufu la GEO la nchimi ujerumani mwaka 2007. Kwa sasa inasimamiwa na kuendelezwa na kampuni ya Marine Service Company Ltd.
No comments:
Post a Comment