Kidole tumbo au Appendix hupatikana katika utumbo mkubwa, urefu wake ni kama kidole cha mwisho cha mkono. Sehemu hii hupitisha myeyuko wa chakula na endapo katika chakula hicho kuna michanga au vitu vidogovidogo vigumu, hujikita humo na kushindwa kutoka.
Kidole tumbo pia kinapatikana upande wa kulia wa tumbo kutoka usawa wa kitovu na nyonga ya kulia.
Taka ngumu hizo zikishajikita kwenye kidole tumbo na kushindwa kutoka ndipo kinapoanza kuvimba, hali hii kitaalam huitwa ‘Inflammation’. Hapa kidole tumbo kinavimba na kuwa na maumivu na pia hupata maambukizi ya bakteria.
Dalili za ugonjwa
Mgonjwa huanza kuhisi maumivu ya tumbo kuanzia usawa wa kitovu ambayo huwa makali na kuacha kisha kusambaa taratibu kuelekea upande wa kulia.
Baada ya muda mgonjwa huanza kutapika kisha kupata homa. Dalili hizi huwa haziji pamoja, huanza moja na kufuata nyingine lakini mgonjwa akiwahi kupata tiba dalili nyingine haziendelei. Baada ya hapo mgonjwa hupata homa.
Dalili za ugonjwa zinatofautiana kufuatana na aina ya ugonjwa huu ambapo kawaida umegawanyika katika hali ya ukali ‘Acute’ na hali ya usugu ‘chronic’. Maumivu makali yanayoambatana na homa na kutapika tunaita ni ‘Acute’
Maumivu ya ugonjwa huu ukifikia hatua mbaya husambaa hadi katika uti wa mgongo usawa wa kitovu au ‘Belly button’.
Pamoja na kwamba maumivu huanzia usawa wa kitovu, lakini dalili za awali kabisa huanzia juu ya kitovu ambayo huja na kupotea na mgonjwa anaweza kujihisi ana ugonjwa wa vidonda vya tumbo, baadaye ndipo hushuka chini taratibu na kusambaa.
Dalili hizi ni tofauti na watoto ambao hulalamika tumbo linauma sehemu zote kukiwa hakuna eneo maalam na baadaye maumivu huwa makali sana kwa tumbo lote hata akiguswa linauma sana.
Hali ya tumbo kuuma huambatana na kujaa gesi kwa wote yaani wanaume, wanawake na watoto.
Chanzo cha tatizo
Kama tulivyoona hapo awali chanzo cha tatizo, maumivu makali ‘Acute’ hapa hutokana na vile vitu vigumu vilivyoingia katika kidole tumbo kushindwa kutoka hivyo huziba kwa juu na zile taka ngumu huganda humo na kidole tumbo kuzidi kuvimba.
Hali ya usugu wa maumivu hutokana na taka ngumu hizo kukaa humo kwa muda fulani na baadaye hutoka huku ukiacha hali ya kidole tumbo kuwa na uvimbe.
Hali ya uvimbe ikikaa muda mrefu husababisha mzunguko wa damu kuzuiliwa sehemu hiyo hivyo kidole tumbo huvimba zaidi na husababisha kuta za Appendix kuharibika ‘Necrtotic’ na kukusanya majimaji kama usaha.
Hali hii husababisha tatizo liitwalo ‘Peritonitis’ yaani tumbo lote huathirika na kuuma. Mgonjwa akichelewa kupata tiba, usaha huu husambaa katika mfumo wa damu na kusababisha kifo.
Uchunguzi
Huzingatia historia ya mgonjwa, dalili na ishara zitajitokeza, vipimo vya damu vitafanyika, vipimo vingine ni vya Ultrasound na CT Scan ya tumbo vitasaidia kujua tatizo kwa undani zaidi.
Zipo pia njia mbalimbali za uchunguzi ambazo daktari anaweza kuzitumia mfano ‘Rovsing’s sign’ na sitokovkty’s sign na nyinginezo.
Matibabu
Tatizo hili katika hatua za awali mgonjwa anaweza kutibiwa kwa dawa lakini tatizo linapoendelea inabidi afanyiwe upasuaji kuondoa Appendix.
Tatizo likiwa kubwa, upasuaji wa dharura hufanyika. Ni vema uwahi hospitali kwa uchunguzi na tiba.
Showing posts with label Lishe na Tiba za Kisunna. Show all posts
Showing posts with label Lishe na Tiba za Kisunna. Show all posts
Thursday, May 25, 2017
Sunday, September 18, 2016
Fahamu maua ya rosela na faida zake.
Rosela ni ni maua yanaoteshwa au kupandwa mazingira ya kawaida haswa nyumbani, maua haya yanapatikana kirahisi katika nyumba za ndugu, jamaa na marafiki na sehemu zinginezo japo kuwa baadhi ya watu huyaita maua damu
MATUMIZI YA ROSELA NA FAIDA ZAKE KWA BINADAMU
Maua ya rosella utengenezwa juisi inayo ongeza damu mwilini kwa haraka
Hutumiwa kama mboga na mbegu zake hutoa mafuta yanayo tumika kama dawa ya vidonda
Dawa ya magonjwa mbalimbali kama kushusha presha, sukari, uric acid mwilini, inatibu kikohozi na mafua, ina punguza mwili pia hutengeneza ngozi na kuifanya iwe laini
Maua ya rosela hutumika kutengenezea juisi , chai ,jam, pia hutumiwa kama rangi ya chakula
MAMBO MENGINEYO KUHUSU MAUA HAYA
Maua ya rosella yana vitamin C,A,D B1,B2,calcium,magnesium,iron, nk
PENDEKEZO
Kulingana na matumizi na faida za maua ya rosella ni vyema kupanda kwa wingi maua haya katika mazingira ya nyumbani kama ya navyo pandwa maua mengine ili iwe rahisi kuyapata pindi yanapo hitajika.

Thursday, August 11, 2016
MAAMBUKIZI SUGU YA NJIA YA MKOJO
Maambukizi Sugu ya Njia ya Mkojo (Chronic UTI) ni Nini?
Njia ya mkojo ni sehemu ya mfumo wa mkojo wenye ogani mbalimbali kama figo, urethra (mirija inayobeba mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu cha mkojo.
Yapo maambukizi ambayo hayatibiki kwa urahisi au yanajirudia mara kwa mara licha ya kutibiwa. Maambukizi sugu ya njia ya mkojo (Chronic Urinary Tract Infections (UTIs) ni miongoni.
Njia ya mkojo ni sehemu ya mfumo wa mkojo wenye ogani mbalimbali kama figo, urethra (mirija inayobeba mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu cha mkojo).
Maambukizi kwenye njia ya mkojo yanaweza kutokea sehemu yoyote katika mfumo huu. Ikiwa maambukizi yataathiri kibofu cha mkojo peke yake ni rahisi kutibika lakini yakisambaa mpaka kwenye figo, mwathirika huumwa zaidi na pengine kulazwa hospitali.
Ingawa maambukizi ya njia ya mkojo yanaweza kumpata mtu yeyote kwa wakati wowote, sanasana wanawake. Utafiti wa National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases (NIDDK) inakadiria kuwa katika kila wanawake watano, mmoja ana maambukizi sugu ya njia ya mkojo yanayojirudia mara kwa mara.
Kinachoongeza hatari ya maambukizi sugu ya njia ya mkojo
Maumbile: Maambukizi sugu ya njia ya mkojo huwapata sana wanawake kutokana na maumbile yao.
Kwanza, urethra yao ipo karibu sana na puru (rectum) hivyo kurahisisha bakteria kutoka kwenye puru kuingia kwenye urethra hasa wakati wa kutawaza. Mara nyingi hutokea endapo mhusika atajisafisha kwa kurudisha mkono kutoka nyuma kwenda mbele. Watoto wadogo wa kike hupata maambukizi ya UTI kwa kuwa hawaijui kanuni hii.
Pili, urethra ya mwanamke ni fupi zaidi ikilinganishwa na ya mwanaume. Bakteria wana umbali mfupi wa kusafiri kufika kwenye kibofu cha mkojo ambako wanaweza kuzaliana na kuongezeka kiurahisi na kusababisha maambukizi.
Aina ya Maisha: Kuna aina ya maisha ambayo yanaweza kukufanya uwe kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi kwa urahisi. Kwa mfano kutumia diaphragm (mpira laini maalumu unaowekwa ukeni wenye kizibo cha kuzuia mbegu za mwanamme kupenya ili kukutana na yai la mwanamke) inaweza kusukuma juu urethra na kufanya iwe vigumu kutoa mkojo wote baada ya kukojoa. Mkojo unaobaki kwenye kibofu huongeza uwezekano wa bakteria kuzaliana na kusababisha maambukizi.
Vilevile, matumizi ya vitu vyenye kemikali kuosha uke vinavyoua bakteria walinzi wa kwenye uke, kama sabuni, marashi au viua mbegu za kiume (spermicides). Pia, kunywa dawa za kuua bakteria mwilini huweza kuua walinzi kwenye uke. Hii inaweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi sugu ya njia ya mkojo.
Kukoma hedhi: Kukoma hedhi husababisha mabadiliko ya homoni ambayo mwisho husababisha kubadilika kwa hali ya bakteria walinzi ndani ya uke hivyo kufanya wafe kwa wingi na uke kukosa ulinzi na kufanya iwe rahisi kupata maambukizi ya njia ya mkojo mara kwa mara.
Aina za maambukizi ya UTI
Maambukizi ya njia ya mkojo husababishwa na bakteria ambao mara nyingi huingia kwenye mfumo wa mkojo kupitia urethra na kisha kuzaliana na kuongezeka zaidi kwenye kibofu cha mkojo. Ili kuelewa zaidi maambukizi haya namna yanavyotokea ni vizuri kugawanya maambukizi katika kibofu cha mkojo na maambukizi katika urethra.
Maambukizi katika kibofu cha mkojo (Cystitis) mara nyingi husababishwa na bakteria waitwao Escherichia coli. E.coli ni bakteria wanaoishi kwenye utumbo wa watu na wanyama wenye afya nzuri. Bakteria hawa wakiwa mahala pao hawana madhara, isipokuwa wakipata upenyo wa kutoka huenda njia ya mkojo na kusababisha maambukizi.
Mara nyingi hutokea pale mabaki ya kinyesi yasiyoonekana yanapoingia kwenye njia ya mkojo.
Kushiriki ngono ya kinyume na maumbile kunaongeza hatari ya kupata maambukizi ya UTI.
Maambukizi katika urethra (Urethritis) yanaweza kusababishwa na E.coli au magonjwa na maambikizi ya zinaa au yanayofahamika Sexually Transimitted Infections (STI) kama pangusa, kisonono au klamidia. Hata hivyo, magonjwa na maambukizi haya ya zinaa mara chache husababisha maambukizi ya njia ya mkojo.
Dalili za Maambukizi sugu ya UTI
Kwa mtu anayehisi maumivu chini ya kitovu au kwenye kibofu cha mkojo au mara kwa mara, kukojoa mkojo uliochanganyika na damu ni dalili za wazi za maambukizi haya.
Dalili zingine ni kutoa mkojo mzito, kuhisi kuchomwa au maumivu wakati wa haja ndogo na maumivu kwenye figo yaani chini ya mgongo au mbavu.
Ikiwa maambukizi yatasambaa hadi kwenye figo, yanaweza kusababisha kichefuchefu, kutapika, baridi, homa kali (zaidi ya nyuzi joto 38.3), uchovu na kuchanganyikiwa.
Mara nyingi, dalili hizi hutofautiana kati ya watoto na watu wazima. Umakini unahitajika kumbaini mtoto mwenye maambukizi haya.
Wakati gani wa kumuona daktari?
Mwanzoni, dalili za maambukizi ya njia ya mkojo zinaweza zisiwe zenye maumivu makali lakini baadaye yakawa makali kiasi cha kutovumilika na kuathiri shughuli za kila siku.
Ikiwa dalili zitakuwapo kwa zaidi ya siku tano, inashauriwa ni vyema ukamuona daktari. Pia, muone daktari haraka ikiwa mwili utachemka sana, ikiwa una mimba au kisukari.
Ikiwa una maambukizi sugu ya njia ya mkojo hii ina maana ulikuwa na maambukizi ambayo hayakutibiwa ipasavyo. Madaktari huwatuma wateja wao maabara kwa ajili ya vipimo zaidi kubaini ni maambukizi ya aina gani. Wataalamu wa maabara huangalia mkojo kupitia hadubini ili kuona bakteria wanaosababisha maambukizi.
Kuotesha mkojo (urine culture test) ni kipimo kingine kinachoweza kufanywa na wataalamu wa maabara ili kubaini aina mahususi ya bakteria aliyemshambulia mgonjwa husika na mara nyingi hurahisisha uchaguzi wa dawa kwa daktari anayetoa tiba. Kipimo hiki huchukua siku moja mpaka tatu kabla majibu kutoka.
Ikiwa daktari atahisi kuna uharibifu wa figo uliosababishwa na maambukizi hayo atapendekeza vipimo zaidi vya figo kama X-ray na Ultrasound. Kama una maambukizi yanayojirudia mara kwa mara daktari anaweza kufanya kipimo cha cystoscopy kinachohusisha mpira mrefu wenye lenzi mwishoni unaotumika kuangalia urethra na kibofu cha mkojo. Daktari anaweza kuangalia pia tofauti za kimaumbile alizonazo mwanamke zinazosababisha kujirudia kwa maambukizi.
Madhara ya muda mrefu ya UTI
Maambukizi sugu ya njia ya mkojo yanaweza kusababisha madhara kwenye figo. Ugonjwa wa figo husababisha kuharibika kwa figo yenyewe na kwa watoto wadogo, kusambaa kwa bakteria kwenye damu (septicaemia). Kwa wajawazito huongeza hatari ya kuzaa watoto njiti endapo hautakabiliwa kwa wakati.
Kujikinga na UTI
Kojoa mara nyingi uwezavyo muda wowote unapojihisi kufanya hivyo.
Wakati wa kutawaza, safisha kwa kupeleka mkono nyuma.
Kunywa maji mengi kusafisha bakteria kwenye njia ya mkojo kila mara unapokojoa bila kusahau kuvaa chupi iliyotengenezwa kwa pamba.
Epuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana na kutumia diaphragm kama njia ya uzazi wa mpango.
Tumia mafuta ya kulainisha wakati wa tendo la ndoa ikiwa inawezekana ili kuondoa michubuko isiyo ya lazima yenye kufanya upenyo wa bakteria.
Kwa wanawake, epuka kuoga ndani ya mapovu mengi kwa kuwa kemikali zilizopo kwenye sabuni huingia kwenye uke na kuua bakteria walinzi hivyo kufanya iwe rahisi kupata maambukizi.
Kwa wanaume, ikiwa haujatahiriwa osha vizuri uume wako mara kwa mara baada ya haja ndogo au tendo la ndoa
Thursday, August 4, 2016
UFAHAMU UGONJWA WA MKANDA WA JESHI
MPENZI msomaji wa ukurasa huu wa lishe na tiba za kisuna, leo tuangalie ugonjwa unaojulikana kama mkanda wa jeshi. Tumekuwa tukishuhudia baadhi ya watu wenye ugonjwa huu wakionekana kuwa wana maambukizi ya VVU bila kuwa na uhakika wa afya zao au bila kutambua chanzo sahihi cha ugonjwa wenyewe.
Hali hii imewafanya baadhi ya watu kuamini kuwa mtu mwenye ugonjwa wa mkanda wa jeshi anakuwa na ugonjwa wa UKIMWI jambo ambalo halina ukweli kwa asilimia mia moja kwani sio wote wenye ugonjwa huu wanakuwa na VVU.
Ugonjwa huu kitaalamu unajulikana shingles au herpes zoster ambapo ugonjwa huu husababishwa na virusi aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga. Ugonjwa huu wa mkanda wa jeshi huathiri ngozi ambapo huambatana na vipele na michubuko kama ya kuungua yenye kuambatana na maumivu makali.
Visababishi
Dk Grace Chirwa kutoka Hospitali ya Temeke Dar es Salaam anasema kuwa ugonjwa huu husababishwa na virusi aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga. Baada ya mtu kupatwa na ugonjwa wa tetekuwanga, virusi vya ugonjwa huo hubaki katika hali ya kupooza/ kutokuwa na madhara katika baadhi ya neva mwilini.
Baada ya kukaa mwilini kwa miaka kadhaa, iwapo kinga za mwili zitashuka kwa sababu yoyote virusi hawa hupata nguvu na kuwa imara jambo linalopelekea kutokea kwa ugonjwa wa mkanda wa jeshi. Ugonjwa huu unapotokea ni mara chache sana ugonjwa huo kujirudia mara ya pili kwa maisha ya mtu huyo.
Vihatarishi
Ugonjwa huu unaweza kumpata mtu wa umri wowote ingawa watu wa makundi fulani wanakuwa katika hali ya hatari zaidi kupatwa na ugonjwa huo.
Makundi ambayo yapo kwenye hatari zaidi ni watu walio na umri wa zaidi ya miaka 60, mtu aliyewahi kuugua ugonjwa wa tetekuwanga kabla ya kufikisha umri wa mwaka mmoja.
Pia watu ambao kinga zao za mwili zimepungua kwa sababu zozote zile ikiwemo mwenye maambukizi ya HIV, saratani pamoja na utapiamlo:
Licha ya hiyo ugonjwa huu hauambukizwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kama yalivyo magonjwa mengine. Inapotokea mtoto au mtu mzima ambaye hajawahi kupata ugonjwa wa tete kuwanga au kupata chanjo yake akakutana na mgonjwa wa mkanda wa jeshi, mtoto huyo au mtu huyo anaweza kuugua ugonjwa wa tetekuwanga na siyo mkanda wa jeshi.
Dalili
Dk Chirwa anasema kuwa dalili ya awali kabisa ya mkanda wa jeshi ni maumivu makali sehemu fulani/ upande mmoja wa mwili yanayoambatana na hali ya ganzi na hisia za kuungua kwenye ngozi.
Maumivu hayo pamoja na hisia hizo za kuungua hutokea kabla ya vipele/ michubuko kutokea kwenye ngozi.
Kawaida ya dalili hizi za vipele au michubuko huusisha eneo fulani la mwili hasa kuanzia kwenye uti wa mgongo kuzunguka kuelekea eneo la tumbo au kifua. Michubuko pia inaweza kutokea kwenye maeneo yanayozunguka uso, macho, midomo au masikio.
Dalili nyingine za ugonjwa huu ni maumivu ya tumbo, homa, maumivu ya mwili mzima, kuwa na vidonda sehemu za siri, kuwa na maumivu katika sehemu za kichwa, kuwa na maumivu ya viungo, kuvimba kwa tezi pamoja na tatizo la kutoona iwapo neva za maeneo ya uso zimeathirika.
Vipimo
Ni mara chache sana kufanya vipimo kwa ajili ya kutambua ugonjwa huu, isipokuwa kwa nchi zilizoendelea. Kwa ujumla utambuzi wa ugonjwa huu hufanyika kwa kuangalia historia ya mgonjwa na kuchunguza sehemu ya ngozi iliyoathiriwa. Pia vipimo vya damu FBP huonesha ongezeko la chembe nyeupe za damu.

Saturday, July 23, 2016
UTAFITI WAONYESHA POMBE INASABABISHA SARATANI
Utafiti mpya imedokeza kwamba kuna uhusiano mkubwa baina ya unywaji pombe na aina saba za saratani.
Matokeo ya utafiti huo yaliyochapishwa katika jarida la "Addiction" yanaonyesha kuna uhusiano mkubwa wa moja kwa moja kati ya unywaji pombe na madhara ya kiafya ingawa bado haijabainika hilo linatokea vipi kibiolojia.
Saratani ambazo imegunduliwa zina uhusiano mkubwa na unywaji pombe ni pamoja na saratani ya mdomo na koo, saratani ya kikoromeo, saratani ya ini, saratani ya utumbo mpana, saratani ya matumbo na saratani ya matiti
Mwezi Januari mwaka huu, afisa mkuu wa matibabu nchini Uingereza alitahadharisha kwamba hakuna kiwango chochote cha unywaji pombe ambacho hakina madhara kwa mwili.
Unywaji pombe unakadiriwa kusababisha vifo vya watu 500,000 kutokana na saratani mwaka 2012 pekee.
Chanzo:BBC

Friday, July 15, 2016
MCHANGANYIKO WA ASALI NA MDALASINI KATIKA KUTIBU MARADHI
FAIDA ZA MCHANGANYIKO WA ASALI NA MDALASINI
Matatizo mengi yanayosumbua jamii hutibika sio tu kwa hospitali bali meng hutibiwa kwa njia za asilia haswa za kissuna. Tuangalie faida za Mdalasini na Asali kwa baadhi ya maradhi
1) MATATIZO YA KIBOFU
Vijiko viwili vya unga wa mdalasini na vijiko viwili vya asali changanya vyote na glass moja ya maji ya moto tumia asubuh na usiku
2) KANSA
Utapata matukeo mazur kwa kansa ya mifupa na tumbo,chukua kijiko cha asali na kijiko cha mdalasini changanya kisha tumia mara tatu kwa siku muda wa mwenzi mzima
3) MATATIZO YA UZAZI
Kwa mwanaume tumia vijiko viwili vya asali kila unapo kwenda kulala itakupa manii zenye uimara
kwa mwanamkechanganya mdalasini na asali zote nusu kijiko kisha finya mchanganyiko huo kwa vidole na uweke kwenye fizi za meno ili ujichanganye na mate uingie mwilini na kuimarisha mfuko wa uzazi
4) TUMBO
Asali na mdalasini huondoa maumivu ya tumbo,huondoa gesi na hutibu vidonda vya tumbo kwa kuondoa wadudu walioko tumboni na pia kukupa afya nzuri.
5) MAFUA Wanasayansi wa spain wamethibitisha kua asali hua na mchanganyiko ambao huasidia kutibu mafua
6) MAGONJWA YA NGOZI
Pakaa asali na mdalasini kwa makadirio sawa hutibu magonjwa yote ya ngozi
7) HARUFU MBAYA YA KINYWA.
Kitu cha kwanza asubuhi piga mswaki kwa mchanganyiko wa asali na mdalasini kijiko kimoja kwa kila dawa kisha sukutua kwa maji moto
8) PUNGUZA UNENE
NJIA YA KWANZA
tumia kwa mfumo huu yaani asali iwe nyingi kuliko mdalasini mfano kijiko kimoja cha mdalasini kwa vijiko viwili vya asali
NJIA YA PILI
chemsha kikombe kikubwa cha maji kisha epua maji weka mdalasini acha yapoe kwa nusu saa na hakikisha maji yamepoa ndo uweke asali kwan maji yamoto huua virutubisho vya asali kisha utakunywa NUSU ya mchanganyiko huo usiku wakati wa kulala kisha asubuhi malizia mchanganyiko huo BILA kuuchemsha tena
9) CHUNUSI
Chukua vijiko vitatu vya asali na kijiko kimoja cha mdalasini kisha weka mchanganyiko huo kwenye chunusi kabla hujalala kisha asubuhi utautoa kwa maji ya moto tumia kila siku ndani ya wiki mbili chunusi zitakwisha
FAIDA ZINGINE
Huongeza nguvu na kukupa uchangamfu pia huongeza nguvu za kiume na kukusaidia kujiskia vyema katika tendo, hurudisha nywele, kwa vipara huongeza nguvu za mwili na kukusaidia kuto kuzeeka mapema, na ndio tiba pekee inayotibu magonjwa ya mifupa

Tuesday, July 5, 2016
FAIDA ZA MBEGU ZA MABOGA.
Unaweza kuzidharau mbegu za maboga, lakini ni miongoni mwa mbegu zenye faida kubwa mwilini, zinazoweza kuzuia na kutibu hata magonjwa hatari yaliyoshindikana hospitalini.
Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi uliokwishafanyika, zifuatazo ni faida za kifya mtu anazoweza kuzipata kwa kula mbegu za maboga, zikiwa mbichi ama zilizokaangwa:
HUIMARISHA MOYO, MIFUPA
Mbegu za Maboga (Pumkin Seeds), zina kiwango kingi cha madini aina ya Magnesium ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo, uimarishaji mifupa, mishipa ya damu na ufanisi wa utumbo mpana. Magnesium imeonesha uwezo mkubwa wa kuzuia mshituko wa moyo na kiharusi.
KINGA YA MWILI
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini aina ya Zinc, ambayo yana faida nyingi mwilini, zikiwemo uimarishaji wa kinga mwilini, ukuaji wa seli, macho na ngozi ya mwili. Vile vile Zinc huimarisha nguvu za kiume.
SARATANI YA KIBOFU
Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha Zinc, utafiti umeonesha kuwa mafuta na mbegu zenyewe za mabogo huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya kibofu.
KINGA YA KISUKARI
Utafiti umeonesha pia kuwa mbegu za maboga huweza kuimarisha utokaji wa ‘insulin’ mwilini, hivyo kuwa kinga au kuleta ahueni kubwa kwa wagonjwa wa kisukari.
TIBA KWA WALIOFIKIA UKOMO
Mafuta ya mbegu za maboga hayana madhara, zaidi yana kirutubisho muhimu cha kurekebisha Cholesterol mwilini, kushusha shinikizo la damu, kuzuia uvimbe, maumivu ya kichwa, maumivu ya viungo vya mwili na vile vile huondoa maumivu mbalimbali yanayowapata wanawake wenye umri mkubwa waliofikia ukomo wa hedhi (Menopause).
UGONJWA WA INI
Mbegu za maboga pia zina kamba lishe na kinga kubwa ya kupambana na magonjwa nyemelezi. Mbali na hayo, mbegu zina virutubisho vinavyotoa kinga dhidi ya magonjwa ya ini na moyo.
USINGIZI
Kwa watu wenye matatizo ya usingizi, wanashauriwa kula punje kadhaa pamoja na tunda lolote muda mfupi kabla ya kupanda kitandani, utafiti umeonesha kuwa mbegu za maboga zina kirutubisho kinachochea uzalishaji wa homoni za usingizi kwa wingi.
UVIMBE
Mbegu za maboga zimeonesha kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa yote ya uvimbe mwilini, yakiwemo ya kuvimba miguu, vidole na hata majipu.
JINSI YA KULA MBEGU
Hakikisha unakula mbegu ambazo hazijaoza na zilizosafi ambazo hazijakaa muda mrefu. Kwa usalama zaidi, zioshe kwa maji safi kisha zianike, inapendeza zaidi ukila bila kukaanga, lakini pia ukiamua kula za kukaanga bado utapata faida zake, muhimu usiziunguze wakati wa kukaanga. Kwa kawaida hukaangwa kwa muda usiozidi dakika 10 tu.

Subscribe to:
Posts (Atom)