Thursday, May 25, 2017

UJUE UGONJWA WA KIDOLE TUMBO (APPENDIX), DALILI ZAKE NA MATIBABU.

Kidole tumbo au Appendix hupatikana katika utumbo mkubwa, urefu wake ni kama kidole cha mwisho cha mkono. Sehemu hii hupitisha myeyuko wa chakula na endapo katika chakula hicho kuna michanga au vitu vidogovidogo vigumu, hujikita humo na kushindwa kutoka.


Kidole tumbo pia kinapatikana upande wa kulia wa tumbo kutoka usawa wa kitovu na nyonga ya kulia.
Taka ngumu hizo zikishajikita kwenye kidole  tumbo na kushindwa kutoka ndipo kinapoanza kuvimba, hali hii kitaalam huitwa ‘Inflammation’. Hapa kidole tumbo kinavimba na kuwa na maumivu na pia hupata maambukizi ya bakteria.



Dalili za ugonjwa
Mgonjwa huanza kuhisi maumivu ya tumbo  kuanzia usawa wa kitovu ambayo huwa makali na kuacha kisha kusambaa taratibu kuelekea upande wa kulia.

Baada ya muda mgonjwa huanza kutapika  kisha kupata homa. Dalili hizi huwa haziji pamoja, huanza moja na kufuata nyingine lakini mgonjwa akiwahi kupata tiba dalili nyingine haziendelei. Baada ya hapo mgonjwa hupata homa.

Dalili za ugonjwa zinatofautiana kufuatana na aina ya ugonjwa huu ambapo kawaida umegawanyika katika hali ya ukali ‘Acute’ na hali ya usugu ‘chronic’. Maumivu makali yanayoambatana na homa na kutapika tunaita ni ‘Acute’
Maumivu ya ugonjwa huu ukifikia hatua mbaya husambaa hadi katika uti wa mgongo usawa wa kitovu au ‘Belly button’.

Pamoja na kwamba maumivu huanzia usawa wa kitovu, lakini dalili za awali kabisa huanzia juu ya kitovu ambayo huja na kupotea na mgonjwa anaweza kujihisi ana ugonjwa wa vidonda vya tumbo, baadaye ndipo hushuka chini taratibu na kusambaa.

Dalili hizi ni tofauti na watoto ambao hulalamika tumbo linauma sehemu zote kukiwa hakuna eneo maalam na baadaye maumivu huwa makali sana kwa tumbo lote hata akiguswa linauma sana.
Hali ya tumbo kuuma huambatana na kujaa gesi kwa wote yaani wanaume, wanawake na watoto.

Chanzo cha tatizo
Kama tulivyoona hapo awali chanzo cha tatizo, maumivu makali ‘Acute’ hapa hutokana na vile vitu vigumu vilivyoingia katika kidole tumbo kushindwa kutoka hivyo huziba kwa juu na zile taka ngumu huganda humo na kidole tumbo kuzidi kuvimba.

Hali ya usugu wa maumivu hutokana na taka ngumu hizo kukaa humo kwa muda fulani na baadaye hutoka huku ukiacha hali ya kidole tumbo kuwa na uvimbe.

Hali ya uvimbe ikikaa muda mrefu husababisha mzunguko wa damu kuzuiliwa sehemu hiyo hivyo kidole tumbo huvimba zaidi na husababisha kuta za Appendix kuharibika ‘Necrtotic’ na kukusanya majimaji kama usaha.
Hali hii husababisha tatizo liitwalo ‘Peritonitis’ yaani tumbo lote huathirika na kuuma. Mgonjwa akichelewa kupata tiba, usaha huu husambaa katika mfumo wa damu na kusababisha kifo.

Uchunguzi
Huzingatia historia ya mgonjwa, dalili na ishara zitajitokeza, vipimo vya damu vitafanyika, vipimo vingine ni vya Ultrasound na CT Scan ya tumbo vitasaidia kujua tatizo kwa undani zaidi.
Zipo pia njia mbalimbali za uchunguzi ambazo daktari anaweza kuzitumia mfano ‘Rovsing’s sign’ na  sitokovkty’s sign na nyinginezo.

Matibabu
Tatizo hili katika hatua za awali mgonjwa anaweza kutibiwa kwa dawa lakini tatizo linapoendelea inabidi afanyiwe upasuaji kuondoa Appendix.


Tatizo likiwa kubwa, upasuaji wa dharura hufanyika. Ni vema uwahi hospitali kwa uchunguzi na tiba.

53 comments:

  1. Naitwa DENIS Michael Chambi.
    Mimi ni miongoni mwa wahanga wa ugonjwa huu, ulinianza muda mrefu kwa haraka naweza kusema ni miaka takribani miaka 10, wakati ugonjwa huu unanianza nilihisi kuwa ni vidonda vya tumbo kutokana na kwamba kila nilipokula maharage, au pililpili nilikuwa nikipata maumivu makaliambayo kama ikinitokea nakosa nguvu ,kama nmesimamaau natembea nitaanguka, maumicu haya yanakuwa yanatembea kutoka choni ya kitomvu upande wa kulia mkaka kwenye mkono wa kulia ambapo kama nimeshika mitu na mkono huu bai nitakiachia, zaidi a kupoata ushauri wa madaktari pale nilipowaeleza tatizo hili sikuwahi kupata dawa yeyeote wengi walikuwa wakinieleza kuwa ni vidinda vya tumbo na wengine wakiniambia ni APPENDEX. Naomba unisaidie niweze kupata msaada wako kwa hali na mali . Nipo TANGA napatikana kwa namba hii 0678712746/0622917607

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nenda hiyo hospital ya ngaromela. Pale palikuwa Tanga hoteli. Yupo mtaalamu. Mm nimetoka hapo j3

      Delete
    2. Kama upo ma mawasiliano yake naomba tafathari

      Delete
  2. Matibababu yake yapoje na ghalama zake

    ReplyDelete
  3. Nami nashangaa ni dalili hizi hizi, ila maumivu ni upande wa kushoto ambao hicho kitu kinawaka na kuachia. Kisha gesi. Nilifkiri naumwa Figo lakini ikawa sivyo. Nimeambiwa vidonda vya tumbo mara nyingi native wapi. Yawezekan ni appendix.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakika mkuu mi mwenyewe nahangaika na haya maumivu tena ni upande wa kushoto tu nimepiga ultrasound hawaoni tatizo nikaenda dar group hospital nikaambiwa nina vidonda vya tumbo nikapewa madawa kibao nimekunywa yote yakaisha lkn hakuna ahuweni

      Delete
    2. Hata mimi inanisumbua me nilijua ni apendex chaajabu ni kushoto.....ila hilo litakua kitu inaitwa chango me ndo nimeambiwa hivyo

      Delete
    3. Mm pia nasikia maumivu makali Sana usawa wa kitovu kwenda kulia mpaka sehemu ya mguu ya kukanyagia panawaka moto hatari inaweza ikawa ni apendex?

      Delete
  4. Sasa unaweza kutibika kilahisi maana mama yangu kaugua uo ugonjwa

    ReplyDelete
  5. Mim nakula sana udongo na mchele mbichi tangia nikiwa na miaka 8 paka sasa na miaka 24 bado nakula tu najaribu kuacha lakini nashindwa tangia mwezi april umeanza napata maumizu kama hayo laki tatizo nimesema wazazi wangu wanasema nikiacha kula udongo na mchele mbichi ya hayamaumivu yataisha. Sasa sijui ni kweli maan sijawahi kwenda kupima

    ReplyDelete
  6. Naomba msaada mim naumwa juu ya kitovu mda meingine kitovu chote kinavuta kwa ndani na pia Nina hara lakin sio sana ila tumbo linauma sana juu ya kitovu he na hii ni dalili ya kidole tumbo?

    ReplyDelete
  7. Mimi naumwa sana upande wa kulia na kisigino mguu wa kulia kilianza kuuma na maumivu yakpanda kwenye nyonga,nilienda kwa Dr Alinipatia dawa na amesema ni dalili za kidole tumbo Dr amesema nkimaliza hizodawa kama maumivu yataendelea nkapime exray ili nifanyiwe operation,naona maumivu naanza kurudi kwa mbali tena

    ReplyDelete
  8. Je maumivu yakitokea upande wa kusho kuja kifuani inaweza kua yenyewe au itakua ni tatizo lingine?.ni Ally kutoka dar es Salaam

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nawashauri muende hospital kubwa kubwa kama za wilaya kwa ajili ya uchunguzi

      Delete
  9. Mgonjwa alie fanyiwa operation ya Apendex anatakiwa kukaa kwa muda gani bila kufanya tendo la ndoa.?! Naendapo atafanya mapema mfano ndani ya mwezi tangu afanyiwe operation nn kitatokea?!

    ReplyDelete
  10. Gharama za matibabu ni shilingi ngapi??

    ReplyDelete
  11. Asant kwa elimu je matunda gani yanasaidia kupunguza vitu vigumu kidolen humo

    ReplyDelete
    Replies
    1. matunda yanayosaidia kupunguza ugonjwa wa appendix ni aina hote ya matunda unayoyajua wewe pia unashauriwa kunywa maji ya kutosha kila siku husaidia kupungza vijidudu

      Delete
  12. Naitwa mnubi nami ni miongoni mwa wahanga wa tatz Hilo Nina mda nalo mrefu takilibani miaka 13 nilikuwa naitaji msaada wako nipate dawa ya kutuliza maumivu tu mahana nipo safarini nikiludi ndo niende kwenye kituo cha afya nikapate tiba

    ReplyDelete
  13. Mimi nakula Sana chalk najitahidi kuacha nashindwa, Nina miaka 4 dada tangu nimeaza kula now naona tumbo langu haliko sawa maumivu makali Kama ya vidonda vya tumbo hutokea Mara kwa Mara , je chalk zinaweza kuwa chanzo?? Ahsanteee

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na kwanini ndugu Ule chaki? Je kwa haraka haraka wewe Unaona ni sawa? Acha mara Moja na ni heri umuombe Mungu na ukatae Hiyo Hali maana vingine huambatana na mapepo unakuta yakuendesha kula kitu Fulani unakuwa addicted kumbe Sio wewe

      Delete
  14. Mm na hisi nipo na hii kitu ila cna uhakika kwa sababu pia nipo na vidonda vya tumbo sasa sielewi kuwa huwa vidonda vya tumbo au hii kitu

    ReplyDelete
  15. Mama yangu anaumwa Sana jamani ugonjwa huu ... Kwani operation sh,ngapi???

    ReplyDelete
  16. Nina maumivu Makal ya kiuno upande wa kulia hadi nashindwa kubeba kitu ata chenye ujazo wa kg1 natumbo langu chini ya kitovu limeongezeka je inawezekana ni kidole tumbo?

    ReplyDelete
  17. Naomba ushauri.
    Nina maumivu chini ya kitovu upande wa kulia(Usawa wa eneo la kuvalia Mkanda) .Nimejaribu kupima(Ultrasound),nikaambiwa Sina tatizo.Wiki mbili zilizopita nilitumia dawa nikapata nafuu,Ila kwa wiki moja tatizo limerudi Tena.Nimeshauri na Dk mmoja kujaribu kutumia Azuma na Bulufelini Ila bado naona mabadiliko ni madogo Sana.

    Je,ni kipimo gani zaidi nachoweza kupima kikanipatia jawabu la uhakika?

    Naombeni msaada

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mm ni muanga mmoja wapo waili swala ndug huu ugonjwa usikie mm nimefanyiwa operation na ss Nina wiki mbili nauguza kidonda so ninaendelea vzr

      Delete
    2. Ulikua unajiskiaje maana nam sijielewi apa ndugu zangu

      Delete
  18. Mimi naharisha kutapika pia mguu unamaumivu makali sana sana siwez hata kukaa hata kusimama nimeambiwa ni apendex bi kweli inasababisha kuuma kwa mguu kuanzia kiunoni kushuka kwenye mapaja

    ReplyDelete
  19. Ukiwa na kidole tumbo, kuna muda utapata maumivu wakat wa tendo kwenye baadhi ya styles?

    ReplyDelete
  20. Mwanangu ametoka leo rabinsia kutolewa kidole tumbo. The 28/10/2021. Hawali nilimpeleka hospital fulani wakashindwa kujua ugonjwa mpaka alivyozidiwa sana tukampeleka rabinsia na kugundua tatizo hili kuwa lishakuwa kubwa. Tulibishana na daktari kwa kuwa nilishasoma humu yeye akidai mtoto miaka 11 awezi kupata ugonjwa huu. Tulikaa hospital hiyo mpya bunju siku tatu mpaka nne mwili unazidi kujaa sumu homa usiku kucha, kila masaa manne sindano za maumivu. Namshkru daktari kutoka rabinisia aliitwa pale kudadisi ndipo aliposhauri akimbizwe afanyiwe upasuaji haraka. Ndipo nilipogundua kwamba hata watu wa vifaa tiba vya uchunguzi inabidi wasome sana kwani mtu wa ultrasound alifel kabisa kuona tatizo lakini wa rabinsia akaona na akakuta usaa ushaanza kuzagaa. Nilitamani

    ReplyDelete
    Replies
    1. ulitumia kiasi gani cha pesa?

      Delete
    2. Kweli kabisa sjui wanakwama wap hawa watu yan wanakupa majibu marais tu yani huumwi kitu kale bata

      Delete
  21. Mi pia nmeamza kuumwa juzi nmebmuhadithia mtu nnavyoumwa akaniambia Ni appendix ndo nmekuja kugoogle nakutana na dalili ambayo kweli Ni nayo.

    ReplyDelete
  22. Me naumwa tumbo juu ya kitovu na ni maumivu makal Sana mpka naishiwa nguvu naomba kujua tibayake

    ReplyDelete
  23. Ndug Amna tiba ya kidole tumbo zaid ya operation tu yaani kukiondoa hapo kabsaa kabla akijaleta madhara na kupeleka kifo

    ReplyDelete
  24. Asante sana ndugu zangu nimesoma makala hii nimeielewa vizuri kabisa mama angu anaumwa tumbo Kwa wiki Sasa ila Kwa dalili alizonazi ni dhahiri anasumbuliwa na Appendix naomba tumwombee mpaka Sasa anaenda hospitali Tena kubwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani inawezekana ukapata kidole tumbo bila kuwa unakula udongo,mchele nk. Unaweza pata kidole tumbo?

      Delete
    2. Ndiyo unapata ni ugonjwa kama magonjwa mengine

      Delete
  25. Naumwa pembeni ya kitovu kulia na vichomi na kwenye mtoku kuna wakati panavimba hadi nachechemea inawezekana ni kidole tumbo? Nisaidie namba yangu ya kupiga 0764848666

    ReplyDelete
  26. waruka salakasi hawapatwi na tatizo hili,Docta tusaidie kutuambie mazoezi ya kuzingatia kuepukana na tatizo hili

    ReplyDelete
  27. Ahsantee leo nimejua kitu

    ReplyDelete
  28. Replies
    1. Garama nimetumia 100000 hospital za serikali

      Delete
  29. Huuuu ugonjwa appendex sikia kwa mtu

    ReplyDelete
  30. Huu ugonjwa wa apendex hatari sana

    ReplyDelete