Rais Trump akizungumza na Waziri wa Mambo ya nje wa
Urusi Sergey Lavrov(kushoto) Ikulu mjini Washington.
|
Rais Trump amekutana na Lavrov pamoja na balozi wa Russia mjini Washington, Sergueï Kisliak katika ikulu ya nchi hiyo. Hata hivyo, picha zilizomuonyesha Trump akionyesha tabasamu kwa kukutana na viongozi hao wa Russia, zimeibua malalamiko kwa Wamarekani ambao wanaiona Moscow kuwa hasimu wa taifa hilo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani, mkutano huo wa Trump na viongozi hao wa Russia, haukuwafurahisha wanadiplomasia wa Marekani na kwamba mapokezi ya Trump kwa Lavrov hufanyiwa viongozi wenye hadhi ya urais. Habari zaidi zinasema kuwa, kitendo cha kutandikwa zulia jekundu kwa wanadiplomasia hao wa Russia, ni harakati ya kuzisifia siasa za Moscow, katika hali ambayo hadi sasa nchi hiyo inatuhumiwa kuingilia uchaguzi wa rais wa mwaka jana nchini Marekani.
Wamarekani anaoandamana kumpinga Rais Trump
Katika mkutano huo baina ya Rais Donald Trump na Sergey Lavrov viongozi hao wamezungumzia juu ya namna ya kutekelezwa makubaliano kwa ajili ya kutengwa maeneo yenye kiwango cha chini cha mivutano chini Syria hususan karibu na mipaka ya Syria na Jordan. Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, katika mazungumzo hayo hakukujadiliwa vikwazo vya Marekani na nchi za Ulaya dhidi ya nchi yake.
No comments:
Post a Comment