Showing posts with label Michezo na Burudani. Show all posts
Showing posts with label Michezo na Burudani. Show all posts

Wednesday, October 5, 2016

RIGOBERT SONG AIRLIFTED TO FRANCE AFTER EMERGING FROM COMA

Former Cameroon international Rigobert Song has been flown from Cameroon to France for further treatment after coming out of a two-day coma. He was admitted to Yaounde Central Hospital on Sunday after falling unconscious.
On Tuesday he waved to fans outside the Yaounde Emergency Centre as he was taken away to the airport.
Rigobert Song

Yaounde Emergency Centre director Dr. Louis Joss Bitang A Mafok said Song had suffered a "cerebral hemorrhage".
Cameroon Health Minister Andre Mama Fouda offered his support: "Song has departed to Pitie Salpetriere hospital in Paris, where he will continue treatment. I am grateful to the Head of State Honorable Paul Biya for instructing the government to take the necessary measures to ensure that Song recovers.’’

"We hail the professionalism of medical doctors in Cameroon and we continue to pray for a safe trip for Rigobert Song and that he should recover very fast," he added.
On Tuesday, Dr. Mafok confirmed Song had "come out of his coma and the oxygen has been disconnected", adding "his high blood pressure has returned to normal and the cerebral haemorrhage has been controlled.


In a career spanning from 1993 to 2010, Song represented Cameroon 137 times. He enjoyed spells in England with Liverpool and West Ham, and ended his career with Turkish club Trabzonspor.
Former Cameroon team-mate Samuel Eto'o tweeted in French: "I wish you courage and a speedy recovery big brother."

Ex-Liverpool players Jamie Carragher, Stan Collymore and Robbie Fowler have also sent messages of support, while Liverpool club tweeted: "Our thoughts are with Rigobert Song and his family at this time."

Thursday, July 14, 2016

JERRY MURO ASALIMU AMRI

Msemaji wa Yanga Jerry Muro
HATIMAYE msemaji wa Yanga, Jerry Muro amekubali yaishe kwa uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Muro alikuwa akitunishiana kifua na TFF pale alipofungiwa kwa mwaka mmoja na faini ya Sh milioni 3, akidai kuwa hakubaliani na adhabu hiyo na kwamba akili kubwa haiwezi kuongozwa na akili ndogo.
Muro alienda mbali zaidi na kudai kuwa yeye sio muajiriwa wa TFF hivyo TFF haina mamlaka ya kumfungia kwa vile yeye sio mwanachama wa shirikisho hilo na kama kufungiwa basi ifungiwe klabu.
Hata hivyo habari ambazo HabariLeo ilizipata hivi karibuni zilisema kuwa uongozi wa Yanga ni kama umemtosa Muro kwa kile ulichodai kuwa haujamtuma Muro kutoa lugha za kashfa na kuzungumza maneno mengi kwenye vyombo vya habari.
Muro jana aliandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram: “Nikifikiria figisu za soka la bongo, aisee nachoka kabisa, acha nijiweke pembeni kwa muda, nitawamiss mashabiki wangu wa kimataifa, acha nikae mbali kwa mbali”.
Akizungumzia suala hilo, Katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdetit alisema: “Barua ya Jerry kashaipata, uongozi wa Yanga kupitia kwa mwenyekiti wetu umemwambia atulie, akae pembeni kidogo, mwenyekiti kwa sasa yupo nje ya nchi,”alisema Baraka.
Makosa yaliyomtia lupango Muro ni kukashifu, kuipinga na kuishambulia TFF kwenye vyombo vya habari hukumu ambayo imeridhiwa na Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa ambaye ndiye aliyewasilisha malalamiko ya TFF kwenye kamati ya maadili akiwa kama mtendaji mkuu wa shirikisho hilo.
Hii inakuwa ni adhabu ya pili kwa Muro baada ya Mei 5 mwaka jana, Kamati ya Nidhamu ya TFF kumpiga faini ya Sh milioni 5 kwa kutoa kauli za chuki, kisirani na uchochezi dhidi ya uongozi wa Bodi ya Ligi (TPLB) nchini na TFF.

Wednesday, July 13, 2016

KIJANA MTANZANIA AHOFIWA KUPOTEZA MAISHA NCHINI MAREKANI

Nebraska, Marekani

Kijana wa Kitanzania Samson Charles Bidan (20) anahofiwa kupoteza maisha baada ya kuzama  kwenye mchanga uliwekwa pembezoni mwa mto katika mji wa Lincoln jimbo la Nebraska nchini Marekani.

Samson Charles Bidan

Samson Bidan mwenye urefu wa futi saba aliondoka nchini kwenda Marekani kwa ajili ya masomo katika chuo cha North Platte Community College (NPCC), pia alijunga na klabu ya mpira wa kikapu ya wanaume inayomilikiwa na chuo hicho na alikuwa amepangiwa kucheza mpira wa kikapu chini ya kocha Kevin O'Connor.

Ajali hiyo imetokea Jumatatu usiku, tarehe 11 July wakati Samson pamoja na watu wengine wawili walipokuwa wakicheza mchezo wa kukimbia majini kwa kutumia boti ndogo.Mchezo huo huko Marekani unajulikana kama "Kayak" ambapo Samson na  mwenzake ambaye ni mwanamke walizama kwenye lindi la mchanga unaokadiriwa kuwa na urefu wa kina cha kati ya futi 50 hadi 80.

Mashuhuda wanasema Samson alipiga kelele za kuomba msaada lakini jitihada za kumuokoa zilishindikana. Mwenzake  aliyekuwa naye aliweza kuokolewa haraka.
Samson Charles Bidan

Jitihada za kuutafuta mwili wa Samson zinaendela kufanywa na timu za uokoaji za Nebraska Game and Parks Commision pamoja na Lincoln County Dive Team na hadi sasa hivi bado hawajafanikiwa kuuona mwili wake.

"Hii ni siku ya kutisha na huzuni kwa NPCC na program ya riadha ya usiku. Katika muda mfupi aliojiunga na chuo, Samson alikuwa na mvuto mkubwa sana kwa wanafunzi wenzake, kitivo pamoja na wafanyakazi. Alikuwa ni mtu mwenye tabasamu usoni mwake na ataendelea kukumbukwa" alisema Dr. Jody Tomanek ambaye ni makamu wa rais wa North Platte Community College alipokuwa akizungumza na jarida la NP Post.

Blog hii ilifanya mawasiliano na kaka wa Samson Bidan ndugu John Joseph Charles ambaye pia amethibitisha kuwa mwili wa ndugu yake bado haujapatikana na jitihada za kumtafuta bado zinaendelea.

WENGER AMTAKA HENRY KUACHANA NA UCHAMBUZI WA SOKA

London, England
Kocha wa Klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amemtaka mchezaji wake wa zamani, Thierry Henry, kuchagua moja kati ya kuendelea kuwa kocha au mchambuzi wa soka.
Henry kwa sasa ni kocha wa vijana wa Arsenal, pia ni mchambuzi wa soka katika kituo cha utangazaji cha Sky Sports nchini England.

Wenger anamshangaa Henry kufanya kazi ya kufundisha na baadaye kwenda kukosoa.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 66, amedai kwamba haina maana kutumia siku zote kufundisha timu, kisha ikifika mwishoni mwa wiki anakaa kwenye runinga na kuanza kuwakosoa wachezaji.
“Hakuna sababu ya kuendelea kuwa kocha, huku baada ya kuwafundisha wachezaji unakwenda kuwakosoa kwenye uchambuzi, Henry anatakiwa kuchagua moja, kati ya uchambuzi na ukocha, ni bora aendelee na ukocha kwa kuwa wachezaji wengi wanatamani kufika alikofika.
“Lakini sidhani kama kuna watakaotamani kufanya kile ambacho anakifanya sasa katika uchambuzi wake,” alisema Wenger.

Henry analipwa na kituo hicho cha utangazaji pauni milioni 4 kwa mwaka, hivyo anaamini hata kama akiendelea kuwa katika klabu hiyo ya Arsenal hawezi kulipwa fedha hizo zote zaidi ya kugawana na viongozi wengine atakaokuwa nao.

Henry akifanya uchambuzi wa soka kwenye kituo cha runinga cha Sky.

Hata hivyo, kauli ya Wenger inaonekana kumgusa Henry ambaye amedai anaweza kutafuta klabu nyingine ya kufundisha kama maneno ya kocha huyo yakiendelea.
Inadaiwa kwamba Wenger alianza kupishana kauli na Henry baada ya kueleza katika uchambuzi wake, kuwa Olivier Giroud hatoshi kuongoza safu ya ushambuliaji ya Arsenal.
Hivyo, Henry alimtaka Wenger kufanya mipango ya kusajili mshambuliaji mwingine ili kuongeza nguvu, kauli ambayo ilionekana kama kumkosoa kocha huyo.
Katika hatua nyingine, Arsenal inatarajia kumwongezea mkataba Wenger kufuatia taarifa kuwa anawaniwa na timu ya taifa ya England kuchukua nafasi ya Roy Hodgson aliyejiuzulu baada ya kutolewa kwenye michuano ya Euro 2016.
Hata hivyo, Wenger alikanusha uvumi huo akisema hana mpango wa kuifundisha timu hiyo na kwamba ataendelea kuinoa Arsenal.

Tuesday, July 12, 2016

SIKU URENO WALIPOIDUWAZA UFARANSA

Paris. Ni mchezo ambao uliiwezesha Ureno kuibuka mabingwa kwa kuifunga Ufaransa 1-0  katika fainali iliyofanyika kwenye Uwanja wa Stade de France jijini Paris.


Ushindi huo umeshangaza wengi walioipa Ufaransa nafasi kubwa ya kutwaa taji na kuungana na Hispania na Ujerumani kama mataifa pekee ambayo yamewahi kushinda fainali hizo mara tatu.


Ufaransa chini ya kocha Didier Deschamps iliduwazwa na kipigo hicho cha kwanza tangu kuanza kwa mashindano hayo yaliyodumu kwa mwezi mzima.

Ukuta wa Ureno kwa sehemu kubwa ndio ilikuwa chachu ya ushindi baada ya kuwazuia washambuliaji wa Ufaransa kufunga bao katika dakika zote 120 za mchezo.

Beki wa Real Madrid, Pepe aliwaongoza wenzake vyema kuwazima nyota wa Ufaransa huku kipa, Rui Patricio naye akiokoa hatari nyingi kwenye lango la Ureno.

Tuesday, July 5, 2016

SERIKALI YAWAGEUKIA WAVAMIZI WA VIWANJA.

Dar es Salaam. Serikali imeapa kukomesha tabia ya uvamizi wa viwanja vya michezo na maeneo ya wazi kama moja ya harakati zake katika kuhamasisha na kuinua sekta ya michezo nchini.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuwa sekta ya michezo haiwezi kupiga hatua kama maeneo ambayo yalitakiwa kuzalisha vipaji yanatumika kwa shughuli zisizo za kimichezo.




Nape alisema Serikali ya awamu ya tano imechoka kuwavumilia wavamizi wa maeneo ya wazi kwa sababu ni miongoni mwa maadui wakuu wanaorudisha nyuma michezo nchini.
“Tulishasema baada ya bunge tutafanya operesheni kubwa ya kurudisha viwanja vilivyovamiwa. Haijalishi ni nani kajenga, turudishe. Nadhani kwa kuwa Bunge limeisha, tutaanza operesheni.
“Dar es Salaam inaongoza kwa maeneo mengi yaliyovamiwa. Nitoe wito kwa madiwani waache uhuni wa kuvamia maeneo ya wazi na kuyagawa kwa ajili ya matumizi mengineyo.
“Hatutaacha badala ya kwenda mbele, tukiruhusu maeneo kuendelea kuvamiwa na kuchukuliwa maana yake tutakuwa tunarudi nyuma,” alisema Waziri Nape.
Waziri huyo alitoa agizo kuwa kuanzia sasa mamlaka zinazo husika na mipango miji, zianze kutenga maeneo ya wazi kwenye eneo lenye makazi ya watu kwa ajili ya kuibua vipaji mbalimbali za michezo.
“Tuache sasa kupanga mipango ya matumizi ya ardhi bila kuweka maeneo kwa ajili ya michezo. Kuna maeneo mengi yanapangwa matumizi kwa ajili ya makazi halafu wanasahau kuwa katika makazi ni vizuri kukawa na maeneo kwa ajili ya michezo,” alisema Nape.