Kijana wa Kitanzania Samson Charles Bidan (20) anahofiwa kupoteza maisha baada ya kuzama kwenye mchanga uliwekwa pembezoni mwa mto katika mji wa Lincoln jimbo la Nebraska nchini Marekani.
Samson Charles Bidan |
Samson Bidan mwenye urefu wa futi saba aliondoka nchini kwenda Marekani kwa ajili ya masomo katika chuo cha North Platte Community College (NPCC), pia alijunga na klabu ya mpira wa kikapu ya wanaume inayomilikiwa na chuo hicho na alikuwa amepangiwa kucheza mpira wa kikapu chini ya kocha Kevin O'Connor.
Ajali hiyo imetokea Jumatatu usiku, tarehe 11 July wakati Samson pamoja na watu wengine wawili walipokuwa wakicheza mchezo wa kukimbia majini kwa kutumia boti ndogo.Mchezo huo huko Marekani unajulikana kama "Kayak" ambapo Samson na mwenzake ambaye ni mwanamke walizama kwenye lindi la mchanga unaokadiriwa kuwa na urefu wa kina cha kati ya futi 50 hadi 80.
Mashuhuda wanasema Samson alipiga kelele za kuomba msaada lakini jitihada za kumuokoa zilishindikana. Mwenzake aliyekuwa naye aliweza kuokolewa haraka.
Samson Charles Bidan |
Jitihada za kuutafuta mwili wa Samson zinaendela kufanywa na timu za uokoaji za Nebraska Game and Parks Commision pamoja na Lincoln County Dive Team na hadi sasa hivi bado hawajafanikiwa kuuona mwili wake.
"Hii ni siku ya kutisha na huzuni kwa NPCC na program ya riadha ya usiku. Katika muda mfupi aliojiunga na chuo, Samson alikuwa na mvuto mkubwa sana kwa wanafunzi wenzake, kitivo pamoja na wafanyakazi. Alikuwa ni mtu mwenye tabasamu usoni mwake na ataendelea kukumbukwa" alisema Dr. Jody Tomanek ambaye ni makamu wa rais wa North Platte Community College alipokuwa akizungumza na jarida la NP Post.
Blog hii ilifanya mawasiliano na kaka wa Samson Bidan ndugu John Joseph Charles ambaye pia amethibitisha kuwa mwili wa ndugu yake bado haujapatikana na jitihada za kumtafuta bado zinaendelea.
No comments:
Post a Comment