BUJUMBURA.
Polisi wa Burundi wanachunguza mauaji ya mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Hafsa Mossi aliyepigwa risasi mjini Bujumbura Jumatano.
Willy Nyamitwe, mshauri wa habari wa rais pierre nkurunziza amesema Mossi aliuawa na “majambazi.”
Mossi aliwahi kuwa waziri katika serikali ya rais Nkurunziza na mtangazaji maarufu wa idhaa ya Kiswahili ya shirika la utangazaji la BBC.
Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Klouise Mushikiwabo aliandika katika ujumbe wa twitter kuwa amesikitishwa na kifo cha Mossi ambaye anasema “aliuawa” kisiasa.
Zaidi ya watu 450 wameuawa Burundi tangu rais Nkurunziza ashike uongozi kwa awamu ya tatu, hatua ambayo wapinzani wanasema ilikiuka katiba na mkataba wa amani uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe 2005.
No comments:
Post a Comment