Saturday, July 16, 2016

JARIBIO LA MAPINDUZI LIMESHINDWA-ERDOGAN

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amelihakikishia taifa kwamba yupo madarakani na kwamba jaribio la mapinduzi sasa limeshindwa.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan

Milio ya bunduki na milipuko hata hivyo iliendelea kusikika katika mji mkuu Ankara pamoja na Istanbul usiku kucha mpaka asubuhi na haikujulikana nani anashika madaraka ya nchi.

Waziri mkuu Binali Yildrim alihutubia taiufa Jumamosi mchana akiita usiku huo kuwa ulikuwa ni doa jeusi kwa taifa la Uturuki.
“Hatua ya kwanza ya tukio hili imefikia mwisho wanajeshi waasi 2839 watafunguliwa mashitaka ya uhaini".
Kwa sasa katiba ya Uturuki hairuhusu adhabu ya kifo lakini waziri mkuu huyo amesema serikali huenda ikaomba kufanya mabadiliko ya kifungu hicho cha katiba.
Wananchi wa Uturuki wakiwa juu ya Vifaru
vya jeshi wakisherehekea kushindwa kwa jaribio
la kumpindua Rais Recep Tayyip Erdogan usiku wa
kuamkia leo.

Tangu tangazo hilo kutolewa neno #Idamistiyorum au “nataka adhabu ya kifo” limesambaa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter huko Uturuki .
Usiku kucha miji ya Ankara na Istanbul ilikumbwa na milio ya risasi na milipuko baada ya wanajeshi waasi kufanya mashambulizi wakitumia vifaru na helikopta.

No comments:

Post a Comment