Saturday, July 16, 2016

Salva Kiir amtaka Riek Machar kwenye Meza ya mazungumzo

Juba, Sudan Kusini

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemtaka mpinzani wake na Makamu wake wa kwanza wa rais Riek Machar kuja katika meza ya mazungumzo ili kupata mwafaka, baada ya watu zaidi ya 300 kupoteza maisha katika mapigano yaliyozuka mwishoni mwa juma lililopita jijini Juba.

Rais Salva Kiir wa Sudani Kusini

Akizungumza kwa mara ya kwanza, rais Kiir amesema hataki tena kushuhudia umwagaji damu nchini humo na kumtaka Machar kuwa karibu naye ili kwa pamoja wakubaliane namna ya kuzuia mapigano kama haya katika siku zijazo.

Kiongozi wa upinzani na Makamu wa rais wa Sudani Kusini Bwana Riek Machar

Rais Kiir ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na kiongozi wa waangalizi wa utekelezwaji wa mkataba wa amani rais wa zamani wa Bostwana Festus Mogae na Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika nchini humo Alpha Oumar Konare, katika Ikulu ya Juba.

Riek Machar tayari ameondoka jijini Juba, na hakuna anayefahamu alipo lakini rais Kiir amesema alizingumza naye asubuhi ya leo lakini Machar hakuonesha dalili zozote za kurejea.

No comments:

Post a Comment