Watu waliojitokeza kushuhudia tukio la kukanyagana ndani ya ukumbi wakati wa sherehe za Iddi huko mjini Kumasi nchini Ghana. |
Watu tisa wamefariki dunia katika jiji la Kumasi ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini Ghana baada ya kukanyagana kwenye sherehe ya Sikukuu ya Eid el Fitr inayohitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan hapo jana.
Majeruhi walipelekwa katika Hospitali iliyokaribu ambapo mmoja wao alikuwa katika hali mbaya. Kituo cha redio cha Joy FM kiliripoti.
Kuna taarifa za kunganganya kuhusiana na sababu la tukio hilo la kukanyagana lililotoke usiku. Mmoja kati ya mashuhuda alinukuliwa akisema kuwa kukatika kwa umeme kulisababisha taharuki na vurugu wakati watu wakigombania kuondoka ukumbini.
Shuhuda mwingine alisema kuwa taa zilizimika ukumbini wakati sherehe zikielekea kumalizika lakini watu hawakuweza kutoka nje kwa sababu milango ya ukumbi ilikuwa imefungwa..
Waislamu walisherehekea sikuku ya Eid el fitr siku ya Jumatano kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment