Nice, Ufaransa
Shambulizi linaloaminika kuwa la kigaidi limeua zaidi ya watu 84 wakiwemo watoto huko katika mji wa Nice nchini Ufaransa. Shambulio hilo limetokea kwa mtu kuendesha gari kubwa la mizigo katikati ya watu waliokuwa wamekusanyika kuangalia fataki na kusheherekea sikukuu ya Bastille Day ambayo hulinganishwa na sikukuu ya uhuru nchini Ufaransa.
Vyombo mbalimbali vya habari vinaripoti kwamba gari hilo la mizigo lilikuwa limesheheni silaha na mabomu na kwamba dereva alianza kwanza kuwashambulia watu kwa kutumia silaha kabla ya kuanza kuwakanyaga. Aliendelea kufanya hivyo mpaka alipouawa na polisi kwa kupigwa risasi.
Gari za Mizigi lililotumiwa na mshambuliaji |
Rais wa Ufaransa Francois Hollande, kwenye hotuba ya moja kwa moja runingani, amesema tukio hilo ni la kigaidi. Amesema hali ya tahadhari, iliyotarajiwa kufikia kikomo mwisho wa mwezi huu itaongezwa kwa miezi mingine mitatu. Wanajeshi pia wataendelea kutumiwa kuwasaidia polisi kudumisha usalama. Raia wameshauriwa kusalia manyumbani.
Waziri wa mambo ya ndani Bernard Cazeneuve amesema watu 84 wamefariki, na wengine 18 wamo katika hali mahututi. Watoto karibu 50 wanauguza majeraha hospitalini.
No comments:
Post a Comment