London, Uingereza
Bi Theresa May ndiye Waziri Mkuu mpya wa Uingereza. May aliteuliwa na Malkia Elizabeth wa pili siku ya Jumatano na kuwa mwanamke wa pili kushikilia wadhifa huo ktika historia ya Uingereza.
Waziri mkuu mpya wa Uingereza Bi Theresa May |
Bi Theresa May ndiye Waziri Mkuu mpya wa Uingereza. May aliteuliwa na Malkia Elizabeth wa pili siku ya Jumatano na kuwa mwanamke wa pili kushikilia wadhifa huo katika historia ya Uingereza.
Mwanasiasa huyo wa chama cha Wahafidhina alitangazwa kama muwaniaji wa pekee baada ya mpinzani wake Andrea Leadsome kutangaza siku ya Jumatatu kuwa hatoendelea kuwania nafasi hiyo.
Akizungumza nje ya makao yake mapya ya 10 Downing Street, Bi Theresa amesema kuwa litakuwa jukumu lake “kujenga Uingereza iliyo bora.”
May, ambaye alikuwa ameandamana na mumewe aidha alisema ushirikiano kati ya Uingereza, Scotland na Wales na Ireland ya Kaskazini utaendelea kuimarika.
Bi Theresa May akiwa na Mumewe Bwana Philip May |
May amechukua usukani baada ya aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, David Cameron, kujiuzulu baada ya wapiga kura kuamua kuwa Uingereza ijiondoe kutoka kwenye umoja wa ulaya. Cameron alikuwa anapinga hatua hiyo ya kujiondoa.
Akitoa hotuba yake ya mwisho kama Waziri mkuu, Cameron alisema ana Imani kuwa Bi may atatoa muongozo mzuri kwa taifa hususan katika majadiliano ya mikakati itakayopelekea Uingereza kujiondoa rasmi kutoka kwenye
Umoja huo.
May mwenye umri wa miaka 59 anatarajiwa kutangaza baraza lake la mawaziri wakati wowote.
No comments:
Post a Comment