DR. MAGUFULI MGENI RASMI BARAZA LA EID.
Rais John Magufuli na Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa wakisalimiana mara baada ya rais kuwasili katika viwanja vya Karimjee kuhudhuria baraza la Eid.
Waziri mkuu Mheshimiwa Kasim Majaliwa akipeana mkono na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli kwenye hafla ya baraza la Eid.Pembeni ni Rais mstaafu Alhaji Ally Hassan Mwinyi.
Rais John Magufuli, Waziri mkuu Kasim Majaliwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zubeir wakifurahia jambo kwenye hafla ya baraza la Eid.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli akihutubia katika baraza la Eid la kitaifa lililofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment