Thursday, July 14, 2016

JUNO YATUMA PICHA YA KWANZA KUTOKA SAYARI YA JUPITA

Washington.
Chombo cha utafiti cha idara ya mambo ya anga ya Marekani NASA kinachojulikana kama Juno kimetuma picha yake ya kwanza ya sayari ya Jupiter toka kilipowasili katika sayari hiyo.
Picha hii ya rangi kutoka NASA  imetengeneza kutoka kwenye picha za mwanzo zilizopigwa na Kamera ya chombo chao cha anga za juu cha JUNO mara tu baada ya kuingia kwenye orbit ya sayari ya Jupita siku ya July 05.
Idara hiyo ya Marekani imetoa picha inayoionyesha sayari ya Jupiter ikiwa imezungukwa na miezi yake minne mikubwa.
Juno ilifika katika mzunguko wa Jupiter wiki iliyopita baada ya safari yake ya miaka mitano, ya kusafiri kilometa bilioni 2.8.
Waendeshaji wa chombo hicho waliopo duniani walizima kamera na vyombo vingine vya chombo hicho kilipokuwa kunapita mazingira ya Jupiter yenye mionzi mikali.
Kamera ya Juno inatarajiwa kutuma picha zenye ubora wa juu za Jupiter mwezi ujao wakati kitakapoanza safari ya kuisogelea zaidi sayari hiyo.

No comments:

Post a Comment