WAISLAM WA DHEDEBU LA BAYE FALL NCHINI SENEGAL HAWAFUNGI SWAUMU YA RAMADHAN
Saumu ambayo hudumu kwa takriban siku thelathini ni moja ya nguzo kuu za dini hiyo.
Katika kipindi hicho chote mtu mwenye akili zake hutakikana kujizuia kula na kunywa ili angalau aelewe jinsi wale ambao hawana uwezo wa kununua chakula huhisi.
Kama ni mgonjwa, ama ni mwanamke anayenyonyesha ama ambaye yuko kwa hedhi.
Lakini kuna jamii fulani huko Senegal ambao wao ni waislamu ila hawajakuwa wakifunga nao ni watu wazima na akili zao.
Wafuasi hao wa dhehebu la Baye Fall lililoasisiwa sheikh Amadou Bamba wanafuata itikadi ya Sufi.
Imani yao inawataka wajinyime na kuwalisha jamii wasiojiweza.
Wakati wa ramadhan wafuasi wa dhehebu hilo hupika chakula na kuwapa futari wale waislamu wanaofunga kula na kunywa.
Kulingana nao thawabu wanazopata kwa kuwalisha wale wanaofunga kula na kunywa ni kubwa mno kuliko kujenga misikiti 1000.
Mara nyingi utaona umati wa watu wakiwa wamebeba sinia kubwa kubwa za vyakula mbalimbali wakiwaandalia wale wanaofunga.
Wakati huu wa ramadhan bila shaka wanasikitika wakati wao wa kuvuna amana umekamilika haraka.
No comments:
Post a Comment