SWALA YA EID EL FITR KITAIFA.
Waumini wa dini ya kiislam wakiwa katika swala ya Eid el fitri leo iliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja leo asubuhi.Ibada hiyo ilihudhuriwa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa na Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi
Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye msikiti wa Ijumaa,mjini Tanga leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
SWALA YA EID EL FITR KIMATAIFA
Waumini wakiingia Kwenye msikiti mkuu wa Niujie huko Beijing China leo kwa ajili ya ibada ya Swala ya Eid kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Waislamu wakiswali Swala ya Eid el Fitri mjini Adis Ababa nchini Ethiopia Leo hii kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mwananchi wa Palestina akiwa ameshika maputo mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Swala ya Eid el Fitri kwenye msikiti wa Al Aqsa jijini Jerusalem leo asubuhi.
Wanawake wa Kashmir wakishiriki Swala ya Eid el Fitr leo asubuhi mjini Srinagar.
Waumini wa dini ya kiislam wakiswali Swala ya Eid el Fitri iliyofanyika katika msikiti mkuu wa Taifa jijini Kuala Lampur nchini Malaysia.
Mamia ya Waislamu wakiwa katika Swala ya Eid el Fitr iliyofanyika leo asubuhi jijini Tehran nchini Iran.
Maelfu ya Waislamu wakiwa katika ibada ya Swala ya Eid el Fitr mjini Tirana nchini Albania huko kusini mwa bara la Ulaya.
No comments:
Post a Comment