KIGALI, RWANDA
Rais Paul Kagame akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu |
ULINZI mkali ulishuhudiwa juzi katika mji mzima wa Kigali wakati Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwasili kwa ziara ya siku moja.
Wakati askari wakiwa wametanda kila kona ya jiji, barabara kuu zinazounganisha mji huo mkuu na uwanja wa ndege zilifungwa na kusababisha foleni na usumbufu mkubwa.
Netanyahu aliye ambaye yupo kwenye ziara ya siku nne barani Afrika aliwasili hapa kwa saa chache ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea kumbukumbu ya mauaji ya kimbari huko Gisozi, pia alifanya mazungumzo na Rais Paul Kagame katika Kijiji cha Urugwiro.
Wakati akiwasili alikaribishwa na Kagame na kukagua gwaride la heshima uwanja wa ndege kabla ya kuelekea Gisozi anbako kuna mabaki ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Wawili hao walitarajia kufanya mkutano wa pamoja na wahabari kabla ya Netanyahu kuhitimisha ziara yake.
No comments:
Post a Comment