Tuesday, July 12, 2016

SIKU URENO WALIPOIDUWAZA UFARANSA

Paris. Ni mchezo ambao uliiwezesha Ureno kuibuka mabingwa kwa kuifunga Ufaransa 1-0  katika fainali iliyofanyika kwenye Uwanja wa Stade de France jijini Paris.


Ushindi huo umeshangaza wengi walioipa Ufaransa nafasi kubwa ya kutwaa taji na kuungana na Hispania na Ujerumani kama mataifa pekee ambayo yamewahi kushinda fainali hizo mara tatu.


Ufaransa chini ya kocha Didier Deschamps iliduwazwa na kipigo hicho cha kwanza tangu kuanza kwa mashindano hayo yaliyodumu kwa mwezi mzima.

Ukuta wa Ureno kwa sehemu kubwa ndio ilikuwa chachu ya ushindi baada ya kuwazuia washambuliaji wa Ufaransa kufunga bao katika dakika zote 120 za mchezo.

Beki wa Real Madrid, Pepe aliwaongoza wenzake vyema kuwazima nyota wa Ufaransa huku kipa, Rui Patricio naye akiokoa hatari nyingi kwenye lango la Ureno.

No comments:

Post a Comment