Vita ya siku sita (Six day war or 1967 Arab–Israeli War, or Third Arab–Israeli War) ilipiganwa kati ya June 5 hadi 10, 1967. Vita ilihusisha Israel, Marekani na Uingereza dhidi ya Mataifa ya kiarabu ya Misri, Jordan, Syria na Lebanon yakiungwa mkono na Urusi kwa kuuziwa silaha. Vita hii ilikuwa ni muendelezo wa uhasama ulioanza tangu mwaka 1948 kati ya Israel na Wapalestina uliotokana na kuzaliwa kwa Taifa la Israel. Marekani na Uingereza zilishiriki katika vita hii kwa lengo la kuilinda Israel na kukabiliana na ushawishi wa Urusi katika mataifa ya Kiarabu ambao ulikuwa ni kitisho kwa maslahi ya kiuchumi ya Marekani.
Vifaru vya Israel aina ya Centurion vikiwa katika maandalizi ya vita Mwezi June, 1967. |
Ingawa kulikuwa na hali tete baina ya mataifa ya kiarabu na Israel kwa muda mrefu tangu kuanzishwa kwa Taifa la Israel, lakini chanzo kikuu cha vita hii ya siku sita kilisababishwa na Misri kukiuka sheria za kimataifa baada ya kuizuia Israel kutumia mlango bahari wa Tiran kwa ajili ya kupitisha meli zilizokuwa zinasafirisha shehena ya mafuta kutoka Iran kwenda Israel. Iran ndio kilikuwa chanzo kikuu cha Mafuta kwa taifa la Israel. Hatua hiyo ya Misri ilipelekea Israel kuanzisha vita kwa shambulizi kubwa la kushtukiza dhidi ya jeshi la anga la Misri mnamo June 05, 1967.
Mlango bahari wa Tiran |
Katika makala hii fupi kuhusiana na vita vya siku sita nimeamua kuandika ukweli ambao vyombo vya habari vya Israel, vyombo vya habari vya mataifa ya magharibi na mashabiki wa Israel ambao baadhi yao ushabiki wao unatokana na shinikizo la kiimani zaidi hawataki kuusikia wala kuuandika katika makala zao. Ukweli huu ni kwamba ISRAEL HAIKUPIGANA PEKE YAKE KATIKA VITA YA SIKU SITA.
Wakati Misri ilipofunga mlango bahari wa Tirane (Tiran straits) Mei 22-23, 1967 mwezi mmoja kabla ya vita ili kuzuia meli zisipeleke mafuta Israel, Rais wa Marekani wakati huo Lyndon Johnson aliionya Misri kuwa kitendo hicho ni sawa na Tangazo la vita kwa kuwa kinakiuka sheria za kimataifa. Rais Johnson alikwenda mbali zaidi kwa kuiambia Misri kuwa ikiwa vita itatokea basi Israel haitakuwa peke yake, labda yenyewe itake kwenda vitani peke yake (Israel will not be alone unless it decides to go alone.)
May 26, 1967 Shirika la upelelezi la Marekani la CIA lilitoa taarifa za kiintelijensia zikikadiria kuwa Israel kama itaingia vitani kwa wakati huo basi itawachukua wastani wa siku 7 hadi 10 kushinda vita. Israel yenyewe iliamini kuwa ingekuwa na uwezo wa kushinda vita ndani ya siku tatu au nne. Huu ni ushahidi wa namna Israel ilivyokuwa ikisaidiwa kiintelijensia na CIA katika vita ya siku sita.
Katika kitabu chake cha Six Days, aliyekuwa mwandishi wa BBC (BBC Correspondent based in Jerusalem) Jeremy F. J. Bowen anasema kwamba June 4, 1967, meli ya Israel iliyopewa jina la Miryam iliondoka katika bandari ya Felixstowe ikiwa imebeba Makontena ya machine guns, 105 mm tank shells, na magari ya kivita kuelekea Israel. Huo ulikuwa ni muendelezo wa shehena kubwa a silaha zilizokuwa zinatumwa kwa siri kutoka nchini Uingereza na Marekani kwa ajili ya maandalizi ya vita ya siku sita. Bowen anaandika kwamba Waziri Mkuu wa Uingereza Mr. Harold Wilson alimwandikia barua ya siri Waziri mkuu wa Israel Mr. Levi Eshkol akimhakikishia kuwa Uingereza itakuwa bega kwa bega na Israel katika uwanja wa mapambano.
Kwa mujibu wa Mwandishi mashuhuri wa Marekani na mchambuzi nguli wa siasa za mashariki ya kati George Lenczowski, akiizungumzia vita ya siku sita, aliandika kuwa mnamo tarehe 23 May 1967 siku moja baada ya Marekani kuionya Misri kuwa kuizuia Israel isipitishe meli kwenye mlango bahari wa Tiran ni sawa na Tangazo la vita, Rais Lyndon Johnson aliidhinisha kwa siri kupelekwa kwa shehena ya zana za kivita nchini Israel kwa njia ya ndege hivyo kukiuka marufuku ya kupeleka silaha katika eneo la Mashariki ya kati yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa.
Mwaka 1993 wakati akifanya mahojiano katika maktaba ya The Johnson Presidential Library oral history archives, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani wakati wa vita ya siku sita, Robert Strange McNamara alikiri kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani iliamuru Meli ya Kivita (Air Craft carrier) iliyokuwa imebeba ndege za kivita kuelekea mashariki ya bahari ya Meditereania kwa lengo la kuisadia na kuilinda Israel katika vita iliyotarajiwa kuanza wakati wowote.
Pia Meli ya upelelezi (Spy Ship) ya USS Liberty nayo ilipelekwa katika peninsular ya sinai ili kuchunguza na kuipa taarifa Israel kuhusiana na harakati za jeshi la Misri. Wakati vita ilipokuwa imepamba moto usiku, ndege za kivita za Israel ziliishambulia kimakosa meli hii katika peninsula ya Sinai upande wa bahari ya mediterania zikidhani ilikuwa ni meli ya kivita ya Misri. Shambulizi hili lilisabisha vifo vya askari 34 wa Marekani na wengine 171 walijeruhiwa, pia meli iliharibika vibaya. Israel iliomba msamaha kwa shambulio hilo, pia ililipa fidia kwa familia za askari waliouawa na kujeruhiwa.
Meli ya upelelezi ya Marekani USS Liberty |
June 9, 1967, katika hotuba yake ya kujiuzulu Rais Gamal Abdel Nasser alisema kuwa Manowari za kivita (Air craft Carriers) za Marekani na Uingereza zilikuwa katika pwani ya Israel zikisaidia jeshi la anga la Israel kushambulia safu za mbele za askari wa Misri na Syria. Abdel Nasser alisema kuwa "bila kutia chumvi jeshi la anga la adui linafanya mashambukizi ya anga yenye nguvu mara tatu ya uwezo wake wa kawaida ("... Indeed, it can be said without exaggeration that the enemy was operating with an air force three times stronger than his normal force")Hata hivyo ombi lake la kijiuzulu lilikataliwa.
Siku ya pili tokea kuanza kwa vita vyombo vya habari vya kiarabu viliripoti uwepo wa majeshi ya Marekani na Uingereza yakipigana bega kwa bega upande wa Israel. Radio Cairo na Gazeti la Serikali ya Misri la Al-Ahram ziliripoti kwamba Marekani pia ilikuwa ikifanya Mashambulizi Mazito ya anga dhidi ya Misri kutoea kwenye Manowari yake (Aircraft carrier) iliyokuwa kwenye kituo chake cha kijeshi cha Wheelus Air base cha huko Libya, pia American Spy Satelite ilikuwa ikituma picha za mienendo ya majeshi ya Waarabu kwa jeshi la Israel.
Ikumbukwe kuwa miongoni mwa sababu zilizopelekea Muamar Gaddafi kupindua Serikali ya Libya tarehe 1 September 1969 ni hiki kitendo cha kuruhusu Marekani Kushambulia Majeshi ya Misri ikitokea katika pwani ya Libya wakati wa vita ya siku sita. Pia iliripotiwa kupitia radio Damascus kuwa Mfalme Hussein wa Jordan binafsi alithibitisha kuwa radar za Jordan zilionyesha ndege za kivita za Uingereza zikiruka kutoka kwenye Air craft Carrier iliyokuwa karibu na pwani ya Israel nakufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya Waarabu.
Katika vita hii Israel, Marekani na Uingereza waliibuka na Ushindi mkubwa ulioiwezesha Israel kuongeza eneo lake la ardhi baada ya kufanikiwa kuiteka milima ya Golan kutoka Syria, Ukanda wa Gaza kutoka Misri na eneo la West bank kutoka Jordan.
Ramani inayoonyesha ushindi wa Israel baada ya vita ya siku sita. |
Ukinakili Makala zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
© Copy rights of this article reserved
®Written by Masudi Rugombana
Napatikana kupitia simu namba
+255743 184 044.
Email: masudirugombana@gmail.com
No comments:
Post a Comment