Tuesday, November 28, 2017

DMITRY MEDVEDEV: Mwanasiasa mwenye nguvu kubwa katika utawala wa Rais Vladmir Putin.

Na Masudi Rugombana.

Dmitry Anatolyevich Medvedev ni Waziri mkuu wa Urusi na Mwenyekiti wa chama cha  United Russia, chama tawala cha kihafidhina cha mrengo wa kulia kikubwa kuliko vyama vyote vya siasa nchini Urusi. Mwanasiasa huyu shupavu mwenye umri wa miaka 52 anatajwa kuwa mtu wa karibu zaidi na mwenye ushawishi mkubwa kwa Rais Vladmir Putin akifuatiwa na bwana Vladislav Surkov mwenye asili ya Chechnya, msaidizi wa Rais Vladmir Putin ambaye nyuma ya pazia ana nguvu kubwa katika maamuzi yanayotolewa kwenye Ikulu ya Urusi (Kremlin). Vladislav Surkov pia alishawahi kuwa naibu Waziri Mkuu wa Urusi kati ya December 2011 hadi May 2012.

Waziri Mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev

Wengine wanaounda timu ya watu wa karibu zaidi na Rais Putin (Putin's inner cycle) ni mfanyabiashara Igor Sechin, huyu ni Afisa mtendaji mkuu (CEO) wa kampuni ya Rosneft, kampuni kubwa ya Mafuta ambayo nusu ya hisa zake zinamilikiwa na serikali ya Urusi, Sechin pia alishawahi kuwa naibu Waziri mkuu wa Urusi kuanzia mwaka 2008 hadi 2012. Pia kuna Mfanyabiasha bilionea Gennady Timchenko, mshirika wa karibu zaidi na Putin ambaye ni mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya Volga Group inayojishughulisha na  uwekezaji katika nishati, usafirishaji na miundombinu. Bilionea huyu mwenye Uraia wa nchi tatu za Urusi, Armenia na Finland anashikilia nafasi ya 85 Duniani kwa utajiri kwa mujibu wa Jarida la Forbes la Marekani.

Wengine ni Spika wa Bunge la Urusi (DUMA) Vyacheslav Volodin. Sergey Chemezov jasusi wa zamani wa KGB aliyefanya kazi pamoja na Vladmir Putin huko Ujerumani Mashariki. Arkady Rotenberg na Boris Rotenberg, ndugu wawili ambao ni wafanyabiashara mabilionea. Wamiliki hawa wa kampuni ya ujenzi ya SGM Group wanatajwa kuwa na urafiki mkubwa na Putin ulioanzia tangu enzi za utotoni. Pia kuna Yury Kovalchuk mfanyabiashara bilionea, mwenyekiti na mmiliki mkubwa zaidi wa hisa wa beki ya Rossiya, mojawapo ya benki kubwa kabisa nchini Urusi, pia anatajwa kama mtu anayeshughulikia masuala ya kifedha katika account binafsi za Rais Vladmir Putin zilizopo kwenye benki mbali mbali (Putin's personal banker).

Medvedev, Rais wa Urusi kuanzia mwaka 2008-2012 ndiye kijana zaidi kuliko Marais wote waliowahi kuiongoza Urusi tangu mwaka 1918, anatajwa kuwa ni kiongozi aliyepata mafanikio makubwa katika uongozi wake wa miaka minne nchini Urusi. Chini ya uongozi wake Urusi imepata mafanikio makubwa Kisiasa, kiuchumi, kijamii na kidiplomasia.

UCHUMI
Anasifika kwa kuanzisha,  kuhamasisha na kusimamia kikamilifu mkakati wa kuugeuza uchumi wa Urusi kuwa wa kisasa (modernization of the Russia economy) kwa kuifanya nchi ipunguze utegemezi katika sekta za mafuta na gesi na kuanzisha mfumo wa uchumi mseto (diversified economy) unaotegemea zaidi teknolojia ya hali ya juu pamoja na ubunifu. Hatua hizi za Medvedev ambazo kwa sasa anaendelea kuzisimamia kwenye wadhifa wake wa Waziri mkuu wa Urusi zimeifanya Urusi kupiga hatua kubwa kwenye teknolojia za mawasiliano, matibabu, madawa, uhandisi wa nguvu za kinyuklia (nuclear power engineering) mawasiliano ya simu na anga.

MAENDELEO YA JAMII
Ilikuwa ni serikali yake iliyoanzisha na kuelekeza moja kwa moja fedha katika mfuko maalumu wa  kampeni ya kukuza kiwango cha kuzaliana baada ya Urusi kukumbwa na tatizo la upungufu wa watu hivyo alifanikiwa katika kupunguza tatizo la upungufu wa idadi ya watu nchini Urusi.Pia ni katika kipindi cha utawala wake alileta mageuzi katika jeshi la polisi na kuzifanya mahakama kuwa huru zaidi. Miongoni mwa alama za uongozi wake ni pamoja  na kufanya  mabadiliko ya katiba kwa kuongeza muda wa kikomo cha Urais kutoka miaka minne hadi sita. Pia aliongeza muda wa ukomo wa bunge kutoka miaka minne hadi mitano.

DIPLOMASIA
Katika ngazi ya kidiplomasia, anasifika kwa kuimarisha uhusiano kati ya Urusi na mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU). Ni katika utawala wake ndipo uhusiano wa Marekani na Urusi uliimarika zaidi hasa baada ya msuguano mkali uliosababishwa na hatua yake ya kuingia vitani dhidi ya Georgia mnamo August 8, 2008 (miezi mitatu baada ya kuingia madarakani) katika mgogoro wa Abkhazia na South Ossetia katika oparesheni iliyojulikana kama "Operation Clear Field" ambapo Urusi ilishinda vita ndani ya siku nne na kuyaondoa majeshi ya Georgia kwenye majimbo hayo ambayo baadae Urusi ilitangaza kuyatambua kama ni nchi huru mnamo August 26, 2008.

Dmitry Medvedev na Barack Obama

Medvedev alifanikiwa kupunguza kasi ya NATO kujitanua kuelekea Mashariki ya Ulaya na kuzuia nchi za CIS (Nchi kumi na moja ambazo ni Jamhuri za zamani za Sovieti union) kujiunga na NATO. Diplomasia yake ilisadia kwa kiasi kikubwa kujenga picha nzuri ya Urusi katika jumuiya ya kimataifa.

VITA DHIDI YA RUSHWA
Vita yake dhidi ya rushwa  aliyoitangaza rasmi mwaka 2008 mara baada ya kuingia madarakani haikuleta mafanikio makubwa. Mwaka 2011 alitangaza rasmi kuwa mkakati wake wa kupambana na rushwa ulikuwa umeshindwa kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo aliendeleza vita dhidi ya rushwa kuanzisha mkakati wa taifa wa kupambana na rushwa, sera ya serikali ya muda mfupi inayofanyiwa marekebisho kila baada ya miaka miwili.

Medvedev alikumbana na changamoto kubwa Mwezi March 2017 baada ya kiongozi wa Upinzani Alexei Navalny kumtuhumu kwa kujihusisha na rushwa, tuhuma ambazo zilishindwa kuthibitishwa. Akizungumzia tuhuma hizo, Msemaji wa Rais Medvedev Natalya Timakova aliziita ni "propaganda zilizopenyezwa kwa hila", naye Msemaji wa Rais Vladmir Putin bwana Dmitry Peskov akizungumzia tuhuma hizo alimwita bwana Alexei Navalny kuwa ni "raia hatari aliyetiwa hatiani kwa sifa mbaya" Ikumbukwe kuwa Alexei ambaye alitangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2018, February 2017 alitiwa hatiani kwa makosa ya ubadhirifu (embezzlement) na kuhukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitano.Hukumu ambayo imemfanya akose sifa za kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2018.

Uchunguzi unaonyesha kwamba Alexei alilishwa taarifa hizo na wanasiasa wa ngazi ya juu wenye lengo la kuwachafua wenzao katika harakati zao za kutaka kuwa na nguvu ya ushawishi katika Ikulu ya Kremlin. Urusi inashika nafasi ya 131 Duniani kwa viwango vya rushwa kwa mujibu wa ripoti ya Transparency international ya kwaka 2016.

UHUSIANO WAKE NA RAIS VLADMIR PUTIN
Medvedev na Putin hawakujuana barabarani, historia yao katika uongozi inaanzia mwaka 1990 wakati mwalimu wao Anatoly Sobchak alipochaguliwa kuwa Meya wa jiji la St. Petersberg. Dmitry Medvedev ndiye alikuwa meneja wa kampeni wa Sobchak . Baada ya kuapishwa Meya Sobchak aliwachukua Medvedev na Putin kuwa washauri, Putin akiwa mshauri (adviser) wa Meya na Medved akiwa mshauri (Consultant) kwenye kamati ya mambo ya nje katika halmashauri ya jiji la St. Petersberg. Baadaye Putin alipanda cheo hadi kuwa naibu Mwenyekiti wa hamshauri ya jiji la St. Petersberg.
Mwezi June 1996 baada ya Meya Sobchak kushindwa uchaguzi, Vladmir Putin alihamishiwa kwenye ofisi ya Rais jijini Moscow wakati wa utawala wa Rais Boris Yeltsin na Medvedev alirudi kufundisha Sheria katika chuo kikuu cha St. Petersberg.

Rais wa Urusi Vladmir Putin (kulia) na Waziri wake mkuu
Dmitry Medvedev

November 1999 kwa ushawishi wa Putin, Medvedev alihamishiwa jijini Moscow na kuteuliwa kuwa naibu mnadhimu mkuu (Deputy Chief of Staff) katika ofisi ya Rais (the Russian Presidential Administration) miezi miwili baada ya Vladmir Putin kuteuliwa na Rais Boris Yeltsin kuwa Waziri Mkuu wa Urusi.

Tarehe 31 December 1999, Rais Boris Yeltsin ambaye alikuwa anasumbuliwa na maradhi alijiuzulu ghafla na kwa mujibu wa katiba ya Urusi, Waziri Mkuu Vladmir Putin alikaimu nafasi ya Urais ( Acting President) hadi Mwezi May mwaka 2000. Wakati wa kampeni za uchaguzi wa Urais, Vladmir Putin alimteua Dmitry Medvedev kuwa Meneja wake wa kampeni. Putin alishinda uchaguzi kwa kupata 53% ya kura.

Mwaka 2003 Vladmir Putin alimpandisha cheo Medvedev kutoka Naibu Mnadhimu mkuu hadi kuwa Mnadhimu mkuu wa Ikulu ya Urusi (Kremlin). November 2005, Putin alimteua Medvedev kuwa naibu wa kwanza wa Waziri mkuu wa Urusi ambaye majukumu yake yalikuwa ni kushughulikia miradi ambayo ni kipaumbele cha taifa (National Priority Projects).

Mwaka 2008 wakati Putin alipomaliza mihula miwili ya uongozi, ambapo kwa Mujibu wa katiba hakuruhusiwa kuendelea na Muhula wa tatu mfululizo, Chama cha United Russia kikiungwa mkono na vyama vingine vitatu kilimteua Dmitry Medvedev kuwa mgombea Urais na Putin alitangaza kuunga mkono uteuzi wa Medvedev. Mara tu baada ya kuapishwa kuwa Rais, Dmitry Medvedev alimteua Vladimir Putin kuwa Waziri wake mkuu nafasi aliyoitumikia kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2012. Kuanzia hapo ndipo vigogo hawa walipoanza kupokezana madaraka ya chama na Serikali kwa zamu mpaka sasa hivi.

UTAWALA PACHA (TANDEM RULE)
Putin mwenye umri wa miaka 65 ana madaraka yote kama rais, lakini Medvedev mwenye umri wa miaka 52 ni waziri mkuu na kiongozi wa chama tawala cha United Russia, chama kikubwa chenye wabunge wengi bungeni kwa hivyo anaongoza chombo cha msingi cha madaraka kinachompa uwezo wa kuwa mtoaji maamuzi mkubwa.

Rais Vladmir Putin na Waziri Mkuu Dmitry Medvedev
wakifanya mazoezi ya viungo

Kutokana na umaarufu mkubwa na ushawishi alionao miongoni mwa wananchi wa Urusi kwa kuweza kumudu vyema nafasi mbili za juu kabisa za uongozi katika serikali (Nafasi ya Rais na Waziri mkuu kwa vipindi tofauti) umaarufu wa Medvedev unakwenda sambamba na ule wa bosi wake Vladmir Putin. Hatua ya Viongozi hawa wawili mashuhuri huko Urusi kuendelea kubadilishana nafasi za juu za uongozi kwa zamu na kwa njia ya kidemocrasia kunaifanya Urusi ionekane kama inatawaliwa na tawala mbili  (Tandem rule) zenye nguvu sawa.

Ukinakili Makala zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
© Copy rights of this article reserved
®Written by Masudi Rugombana

Napatikana kupitia simu namba

+255743 184 044.
Email: masudirugombana@gmail.com


Monday, November 27, 2017

DOLA YA MRIMA (KILWA) ILIOKUWA TAIFA KUU AFRIKA KARNE YA KUMI (1070 A.D)

NA: Comred Mbwana Allyamtu
Sunday -7/9/2016

Mji wa Kilwa ni mji maarufu sana barani Afrika kwa sifa zake sio kwamba kwa sababu ya jina lake au ukarimu wa watu wake bali ni kwa historia yake toka zama za kale za historia ya ulimwengu na habari za wanahistoria toka duniani kote.

Bila shaka binafsi sina shaka kabisa na hili kwa sababu nilipata bahati ya kutembelea iliokuwa miji kadhaa ya Dola la Mrima yani miji ya Kilwa, Tanga ( mta'nga'ta), Sadani, Kaole, Zanzibar,Mombasa na Bagamoyo lakin pamoja na kujionea utajiri wa kihistoria niliojionea sikusita kabisa kukubaliana na historia hiyo ya Dola la Mrima lililokuwa likipatikana pwani ya Azania na ndio Dola lililokuwa dola kuu Afrika kiuchumi, kijeshi, kisiasa na kiteknolojia. Pia ndio dola lililokuwa na ushawishi katika ulimwengu wa zama hizo uliokuwa ukiongozwa na Dola la Rumi na baadae Dola la Hermani (Ujerumani).

Taifa la Mrima ni Dola lililo kuwa likipatikana mashaliki ya bara la Afrika iliokuwa pakiitwa "Azania" na ilikuwa na miji mikubwa iliokuwa chini ya himaya ya dola hilo zaidi ya 36 kama Lamu(Amu), Mvita (mombasa), Ofiri(Sofala), Rhapta, Mafia, Unguja na Cambula (pemba), Ngozi(Mogadishu), Simayu(kisimayu) na makao makuu ya dola ilikuwa Kilwa.

Historia ya utawala wa Dola la Mrima kiutawala ilikuwa chini ya "mwinyi mkuu" (sulutani) ambaye yeye alisaidiwa na mihimili mingine ya dola.
Pwani ya Azania ni pwani ilikuwa inapatikana mashariki ya Afrika kuanzia Msumbiji ya leo mpaka Asmara (Eritrea) ya leo. Azania ni neno lenye asili ya kiarabu yaani "Ajania" ikiwa na maana ya "isiyokuwa Waarabu". Historia ya mwambao huu imefahamika tokea zama za mwanzo za mileniamu (1st millenia) katika kitabu cha "the periplus of Arithrean sea" unaweza kupata maeelezo zaidi ya namna gani dola ya Mrima ilivyo shamili duniani kote. Pia wanahistoria kama Betram ThomasThomas na M.H. Dorman ambao wote kwa pamoja wameeleza kwa pamoja namna Dola hilo lilivyostawi sana.

CHANZO CHA DOLA LA MRIMA-665 AD
Hassani ibn Abduraufu (Mbega) ni moja ya watu ambao historia inaowataja kuwa viongozi wa mwanzo kuanzisha dola ya Mrima. Mbega inasadikika alikuja Azania kutokea Hijjaz na alifika mji wa mta'nga'ta (Tanga) na aliishi hapo mpaka 665 na baadae alielekea katika milima ya Usambala (kitabu cha zamani mpaka leo kilicho andikwa na taasisi ya utafiti wa kiswahili 1930) kimejaribu kuelezea habari za mtu huyu Mbega (Hassan ibn Abduraufu) kuwa aliishi Nguu huko Zigua na baadaye alielekea Kilindi alipo amua kuoa Bumbuli na baadae akawa kiongozi.

Huko "Kilindi" ilimfanya kuwa kiongozi wao baada ya kuwasaidia wakazi wa hapo kuwaondolea tatizo sugu la nguruwe pori kwani nguruwe hao walikuwa wanawatafuna watoto wachanga mpaka ilipo fikia mpaka mtoto wa kiongozi wa eneo hilo alipoliwa na nguruwe ndipo Hassan ibn Abduraufu alipo fanikiwa kumaliza tatizo hilo na
Kuwafanya wenyeji kumpa jina la Mbega yani mkombozi (liberator).

Mpaka kufikia mwaka 689 alifanikiwa kusimamisha dola iliyojulikana kwa wakati huo kama Dola ya KILINDI. Makao makuu ya Dola ya kilindi ilikuwa Handeni na Dola hii ilienea tokea kwenye safu ya milima ya Usambala mpaka Mombasa (mvita), Lamu (amu), mpaka Mogadishu(Somalia). Pia ilikuwa na mji mikubwa kama Saadani, Pete, Tongoni, Kaole na Rhapta. Na ilipokuwa dola imara ilifahamika kama Dola la VEGA(Vega state) chini ya kiongozi alieitwa Kimweri ambaye alikuwa mjukuu wa Hassan Mbega. Na taifa (Dola) hii ilikwenda mpaka 1234 ilipo mezwa na dola jingine lililokuwa linajiimarisha (Mrima).

Dola ya Mrima ilipanuka kutokana na kile kilichoitwa mgogoro wa "Muhawiya" uliotokea bara Arabu na kupelekea idadi kubwa ya wageni kuhamia pwani ya Azania.

VITA YA MUHAWIYA-680 A.D-685 A.D (61-64 HIJIRIA)
Hivi ni vita iliyotokea katika himaya ya Uthumani (OTTOMANI EMPIRE) mara baada ya Khalifa Ally ibn Abuu Twalib kulitokea utawala wa Banu Ummayya chini ya Muawiyya bin Abuu Sufiyani na baadae Yazid Bin Muawiyya wakati wa utawala huu hasa wa Yazid ulikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu lakini wakati wa utawala huu ndio kipindi wakati dini ya Uislam ilipo ingia barani Ulaya (Hispania) 705-715 A.D

Lakini vuguvugu la migogoro ilizidi maradufu baina ya ukoo wa Abbas kujitenga dhidi ya ukoo wa Abuu Muslim ambaye aliungwa mkono kwa kile alichodai kuwa ni utawala wa U-calipha lazima utoke katika ukoo wa mtume Muhammad (s.a.w) yaani "Ahlul Bayt" lakini mwishoni Abuu Abbas alishinda vita na vita kwisha 750A.D.

Katika mgogoro hiyo ya vita idadi kubwa ya wageni walihama bara Arabu na kuingia pwani ya Azania kupitia mji wa Asmara. kundi hili liliongozwa na Hamza ibn Marwani aliwasili Somalia na ndio chanzo cha jamii ya (Polusa) ambayo ni miongoni mwa jamii (kabila) tatu zilizopo Somalia leo yaani Olmo, Polcano na Polusa (ukoo wa Malwani).

Kundi hili ndio lililo anzisha makazi Asmara na Mogadishu na baadae mwaka 780-900 A.D walipo anza kusogea mwambao wa kusini mwa pwani na hatimaye badhi yao kutia makazi Kismayu, Lamu, Galisa katika Kenya na baadhi ya maeneo ya pwani ya Tanzania. (rejea kwenye andiko la Feeman Granville uk 35 history of East coast Africa)

DOLA YA MRIMA (KILWA) 1300 A.D
Ukipitia andiko la Walter Rodney katika kitabu chake " Africa development before 15C" amejalibu kuandika kwa undani namna gani dola la Mrima(kilwa) ilivyo kuwa na kuwa dola kubwa kabisa barani Afrika hata kuzidi dola zingine za afrika kama Songhai, Mali, Benin, Absinia na Ghana. Hii pia dola la Mrima ilikuwa kubwa mpaka dola kuu za dunia zama hizo kama Dola ya Rumi, Dola ya Herman na Dola ya Ottoman kuitambua dola ya Mrima kuwa ndio Dola kuu afrika. Na hata Hassan ibn Batuta alipo wasili mwaka 1300A.D alikiri kuwa

" nilipo fika kilwa nilimkuta mtawala Wao na walinipokea kwa ukarimu mkubwa sana na walikuwa na kila kitu kama tulivyo navyo kwetu (bara Arabu)".

Hivi ndivyo kilwa ilikuwa maarufu sana. Kwani Muundo wa utawala wa Dola ya Mrima ( kilwa) ilikuwa na muundo wa kipekee ulioendana na mazingila ya kijografia ya wakati huo makao makuu ya dola la Mrima ilikuwa Kaole-Bagamoyo lakin makazi ya utawala yalikuwa Kilwa kiswani mahali ilipokuwa ikulu iliojulikana kama (Husuni)



Ikulu ya Husuni-Kilwa kisiwani


Na mtawala wake alijulikana kama Hassan Sulyman kwa title ya Mwinyi Mkuu katika ikulu ya Kilwa ndo iliokuwa ikulu kubwa Afrika kwa wakati huo kwani ilikuwa na vyumba 100 ambavyo vilikuwa vinatumika kama ofisi ya mwinyi mkuu na watumishi wake, pia kulikuwa na idara maalumu kama idara ya...

1-Uvuvi
2-Masoko na biashara
3-Elimu
4-Uchumi na Afya

Mwinyi mkuu Alli Hassan ibn Shirazi

Katika Uvuvi ofisi zake za utendaji ziliwekwa eneo la Mussa Hassan ( Msasani). Masoko na biashara ziliwekwa Bagamoyo (Sadani). Idara ya Elimu ilikuwa Kilwa kiswani pia idara ya Afya ilikuwa Bagamoyo na ndipo ilipojengwa kituo cha Afya cha Tumbatu (shapani) na Makulunge kilichokuwa kikitoa tiba na kikiongozwa na Mtabibu Hamis Mwinyi sembe Shomvu aliyepata elimu ya tiba katika chuo cha Aveccina (Iraq) ushahidi wa habari hizi umeelezwa na Saleh Miskir toka Iraq kwenye kitabu chake cha ( A thousand and one night).

Katika Dola ya Mrima (Kilwa) kulikuwa na bandari marufu iliokuwa katika mji wa Rhapta hapa ndipo wafanyabiashara kutoka nje ya pwani ya Azania walifika kufanya biashara nao na pia katika uchumi dola ya Mrima (Kilwa) ilikiwa tayari imesha tengeneza pesa yake iliyokuwa inatumika katika biashara ya mabadilishano ya bidhaa na ndio dola pekee kwa wakati huo ilikuwa imevumbua utaratibu huo barani Afrika.

Sarafu ya Kilwa

Mfano ni Hassan Ibn Batuta 1331-1333 A.D huyu alikuwa mpelelezi, msafiri, mtaalamu na Misionari wa kiarabu (Kiislam) aliefika pwani ya Azania katika karne ya 12C na alizuru mji wa kilwa na Rhapta katika safari yake ambaye binafsi aliueleze mji wa kilwa na dola ya Mrima kama dola kuu na kubwa iliokuwa imestaarabika katika kiwango kikubwa na kutumia sarafu ya pesa katika mfumo wa uchumi (curency economy Oriented theory) kama sehemu ya mabadilishano ya bidhaa (rejea kitabu cha "Ibn Batuta" uk 143-147 chapa ya Beiruti) au vitabu kama "introduction" cha Mohamed Khadum, au kitabu "The incoherence for the incoherence" cha Benmon Harph Herzre chapa ya Jerusalem. Pia mwaka 1498 alipo fika Vasco Dagama pwani ya Azania alieleza namna Dola ya Mrima (Kilwa) ilivyo kuwa na nguvu.

SAFARI YA VASCO DAGAMA KUJA PWANI YA AZANIA 1497 A.D
Vasco Dagama safari yake kuja pwani ya Azania ilipelekea pakubwa na uvumbuzi wa njia rahisi ya maji ya kufika India hii ilitokana na njia ya ardhi kufungwa na adui yao mkubwa wa Dola ya Othuman (Ottomani Empire) ambaye alikuwa ametoka kushindwa kwenye vita ya msaraba (Crused War) ya Ulaya hali hii ilipelekea miliki ya Uthumani kupoteza makoloni yake Ulaya kama Hispania jambo hili ilibidi mataifa ya Ulaya magharibi kutafuta njia nyingine salama kwani walihofia wafanyabiashara wake kutekwa iwapo wataendelea kutumia njia ya Constantinepoli mpaka India kwani wakati huo Constantinepoli ilikuwa chini ya Dola ya Ottomani.


VITA YA MSALABA
Ni vita iliyoanzishwa na Pope Urban II katika karne ya 13 A.D na vita hivi ilikwenda awamu nne na ilipelekea nchi nyingi zilizokuwa zinakaliwa na iliyokuwa Dola na himaya kubwa ya Uislam wakati huu ya Othumani (Ottoman Empire) ambayo ilikuwa imekalia mataifa kadhaa ya Ulaya kama Spain, Ugiriki, sehemu ya Ufaransa na sehemu kadhaa za ulaya ya kati ziliweza kujipatia uhuru. Na baadae mataifa hayo huru kuliongezeka hali ya kutokuwepo na Utengamano na kusababisha nchi hizo za ulaya kutafuta njia mbadala ya kufika India.
Ndipo Vasco Dagama alipo tumwa kutafuta njia nyingine na aliwasili pwani ya Azania tarehe 7/4/1497 alifika na merikebu yake iliokuwa ikiitwa "San Raphael" Mombasa na baadae Tongoni na hatimaye mji wa Kilwa. Pamoja na safari hii ya Vasco Dagama Kilwa pia aliandika kwenye andiko lake habari za Mrima ( Kilwa) kwenye kitabu kilichoitwa "Sarade san Raphael" yani 'milima ya raphael mtakatifu' inayopatika kwenye kitabu cha Kesteloot uk 86. Ndani yake Vasco Dagama kaelezea wazi kuwa dola ya Mrima(Kilwa) ilikuwa dola kubwa na yenye pesa yake katika uchumi na utawala wake wenye nguvu. Hali hii ilimfanya Vasco Dagama kupeleka taarida nchini mwake Ureno iliyosababisha kuandaliwa kwa utaratibu wa utawala na uvamizi wa Ureno pwani ya Azania.

UVAMIZI NA KUANGUKA KWA DOLA YA MRIMA (KILWA)
Kutokana na ujio wa Vasco Dagama uliopeleka kuandaliwa utaratibu wa kupanua himaya ya Ureno ndipo Ureno ilipoagiza jeshi la uvamizi pwani ya Azania kikosi kilicho ongozwa na kamanda Fransisco D' Almenda ambacho kilianza safari na kuwasili kilwa tarehe 22/7/1505 akiwa na merekebu 22 zilizojaa wanajeshi 1500 na silaha za kutosha, ikumbukwe kwamba safari hii ya D' Almeida ilikuwa tayali imeshatanguliwa na ile ya mashushushu ambao walikuwa tayari wapo mjini Kilwa na tayari walikuwa wakiishi hapo mfano ni shushushu mreno aliejulikana kama Antonio Fernandes ambaye aliishi Kilwa kwa muda na kufanikiwa kuandaa wasaliti kadhaa akiwemo mtu mzalendo wa Kilwa aliyejulikana kama Mohamed Ankoni. (Rejea kitabu "History of Africa" uk 129-135, Kelvin Shillington). Kupitia ujasusi huu uliokuwa umeandaliwa na Wareno mapema ulifanikisha mpango wake wa uvamizi (rejea kitabu "history of East Africa up to 19C. Uk 77)

1505 uvamizi ulianza katika miji mbalimbali ya pwani ya Azania ikiwa ni sambamba na ujenzi wa ngome za Ureno mfano wa ngome hizo ni ngome ya Ureno Kilwa kiswani na Ngome ya Yesu iliopo Mombasa. Binafsi nilipata bahati ya pekee kabisa kama ilivyo kasumba yangu ya kupenda kutembelea (travelogy adventure) vivutio mbali mbali napokuwa ndani na nje ya nchi ili angalau niweze kujifunza jambo (perspective analysis).

Hivyo basi nilipo pata fursa ya kutembelea mji wa Mombasa mwaka huu ilikuwa tarehe 16/1/2016 na nilifika mahali ilipo ngome inayoitwa ngome ya yesu (Fort Jesus) mantiki ya kutoa kisa hiki cha kuzuru mahari hapo ni kujaribu kukuonyesha namna  Dola la Mrima lilivyo poromoka kwa usiku mmoja (siku chache) ukilinganisha na masiku lilivyojengwa kwa miaka isiopungua 200. Katika safari yangu katika eneo hilo la kihistoria mahali hapo panapofahamika kama Ngome ya Yesu (Fort Jesus) ndipo aliekuwa mwanamakumbusho (Museulogist) alipo nipa simulizi ya kusisimua na iliyopelekea kudondoka kwa iliyokuwa dola ya Mrima (Kilwa) ya pwani ya Azania.
Kwa mujibu wa maelezo ya msimulizi huyo uvamizi huo ulikuwa na sura mbili (2) na ulifanyika kwa awamu nne (4) .

SURA YA 1

AWAMU YA I.
Ilikuwa ni mnamo mwaka 1506 ambapo jeshi la Ureno likiongozwa na kamanda Fransisco D' Almeida akiwa na jeshi alivamia mji wa Kilwa Mafia na baadae ZANZIBAR. Na ZANZIBAR kukawa eneo la kwanza la kireno kuwa chini ya himaya yake chini ya capteni Ruy Lourenço Ravasço.

AWAMU YA PILI.
Awamu hii mnamo mwaka 1510 uvamizi ulifanyika kutokea kusini yani Sofala kuja mpaka kwenye visiwa vya "Mayote, Mororoni na Anjuani" jeshi hili liliongozwa na kapteni Vermudezi. Kikosi hichi ndicho kilichoenda kutia nguvu baadae Mombasa.

AWAMU YA TATU.
Kikosi hiki kiliongozwa na kamanda D' Almeida kufanya maangamizi eneo la Kilwa, Mafia na Pemba (kamablu). Mwaka 1513 A.D

AWAMU YA NNE.
Hiki ndiko kilicho ongoza uvamizi kuanzia Malindi, Lamu, Pate, Kismayu, Barawa na Mogadishu. Mwaka 1509-1516 A.D

SURA YA 2
Katika sura hii ni ule vamizi wa mji wa Kilwa ambao kulitokea patashika ya mapambano. Na wanahistoria kadha pamoja na wakazi ambao wamerithi habari toka kwa kizazi kilicho ishi hapa huelezea kuwa baada ya uvamiz wa kilwa ndipo viongozi wa dini wakiongozwa na mtu aliefahamika kama Hassani Mwinyipembe walifanya maombi matakatifu kwa zaidi ya masaa 9 hali iliyopelekea maajabu makubwa sana majabu hayo yapo yanaishi mpaka leo moja ya maajabu hayo ni:-

1- Zile merikebu zilizokuwa pale Songo mnara ziligeuka kuwa " Majabali" na mabaki ya merekebu hizo ambazo ziligeuka kuwa majabali huonekana leo hasa ukiwa unatokea Dar es salam kuelekea Mtwara ambapo siku hizi kumewekewa taa nyekundu ili kuwaongoza mabaharia wasigonge miamba hiyo iliyokuwa merekebu na kugeuzwa kuwa Miamba.

2- Pia kundi la wenyeji 100 ambao walikuwa wasaliti pia wamegeuka kuwa "Vichuguu" na mpaka leo huonekana pale msitu wa Mikoche ( mikoche historical site) pale Kilwa kiswani ambapo hivyo vichuguu 100 vinavyo aminika kuwa walikuwa wasaliti huonekana hadi leo. Na ningependa kuwasihi kuwa iwapo utapata wasaa basi hebu tembelea miji hii ikiwa ni pamoja na eneo hili ili ili uweze furahia wingi wa maajabu na historia hii ambayo mimi Mbwana Allyamtu binafsi nilifarijika sana.

Lakin katika kipindi cha uvamizi huu Dola ya Mrima ilijaribu kuomba msaada toka constantinepoli lakini msaada haukufua dafu kwani merikebu zao zilikuwa ndogo ukilinganisha na za Wareno ambazo walikuwa wamejipanga kiasi cha kutosha kwani mashambulizi haya yaliacha athari kubwa na mbaya sana kama
- "vifo, uharibu wa miji na mali zao, kuangamiza kabisa baadhi ya miji kama Rhapta ambao uliangamia na kupotea kabisa mpaka ulipo kuja kuthibitika tena kwa mujibu wa kitabu (A Guide to Tongoni Ruins cha A.A.Mturi) kinachosema "The ruins of Rhapta are yet to be found though it is generally agreed tha the town was situated on Tanzania coast" yaani " mabaki ya mji wa Rhapta umepatikana tena kwa makubaliano ya pamoja kwamba kunauwezekano mkubwa wa mji huu ulikuwa pwani ya Tanzania".

Mpaka kufika mwaka 1599 tayali ngome yote ya Mrima (Kilwa) ilikiwa tayali imekaliwa na Ureno na kuifanya ngome ya Kiswahili ya Azania (Mrima) kuangushwa na kuwa chini ya Ureno ambapo utawala huu ulidumu takribani kwa miaka 100 bila maasi ya kujikomboa mpaka mwaka 1698 mapambano ya kujikomboa yalipoanza tena na kuifanya Ureno kuanza kuachia baadhi ya ngome za Mogadishu, Mombasa mpaka ZANZIBAR na Kilwa na kuifanya Ureno kurudi nyuma na kubakia Sofala- Mozambiq( Musa bin beq) na kuamua kujizatiti na kujikita kiutawala huko amabapo utawala wake ulidumu kwa zaidi ya miaka 500 huko mpaka walipo kuja kuanza harakati za kujikomboa mwaka 2/6/1960 chini ya Eduardo Mondlande nakujikomboa kabisa kuwa huru mwaka 1975 chini ya "FRELIMO ya Samora Machel.

Watawala wa Dola ya Mrima (kilwa) kuanzia mtawala wa kwanza mpaka wa mwisho pale ilipo dondoka dola ya Mrima jumla walikuwa ni "50" yani kuanzia mtawala wa kwanza Mwinyi mkuu Hassan bin Ali.(Allyamtu) mpaka na wa mwisho (50) yaani ambaye uvamizi na utawala wa Kireno ulipo shinda na kumuangusha alikuwa ni Mwinyi mkuu Said ibn Mwinyi.

MWISHO.
Naomba nitangulize shukrani zangu za dhati kwa mwenyezi Mungu mwingi wa rehema (Allah) kwa utukufu wake kwa ulimwengu na mbingu yote na vyote vilivyomo ndani yake pia na pamoja na shukurani hizo za pekee kabisa pia naomba nipeleke shukurani zangu kwa wadau wangu wote ambao kwa pamoja wamenipa ushirikiano wa kufanikisha kuandika andiko hili langu kwa kiwango kikubwa japo kwa uchache tu japo natambua kuwa ni wengi kwa idadi lakini nyote nawashukuru kwa utukufu mkubwa kabisa ambapo mmefanya niweze kulikamilisha jambo hili (andiko hili la nyumbani Azania) lenye mvuto na msisimko wa pekee kabisa kwa wakati.

Lakini pia naomba kuwashukuru Bwana Alfosi Wanjilu (Mombasa historical site) toka Kenya, Abdala Msumbuko (Kaole historical site) Bagamoyo na bibi Aisha Zuberi kutoka Kilwa historical site. Ambapo kwa pamoja mmefanya niandike makala hii kwa mvuto wa pekee kabisa kwani nimeandika yale ambayo nimeyaishi na kuyashuhudia kutoka kwenye ziara ya kujionea na kushuhudia historia ya miji hiyo.

Watafiti wengi na wanahistoria wengi sasa wanakubaliana kuwa Dola ya Mrima (kilwa) kuanzia mnamo miaka ya 967 mpaka 1399 A.D ndio ilikiwa dola kubwa ukanda wa kusini wa bara la Arabu na Ulaya. Pia ndio iliokuwa dola la 4 kwa "Ushawishi wa Dunia ya wakati Ule" ikiwa nyuma ya Dola la Rumi (ROME EMPIRE) Dola la Sackxoni (HEREMAN EMPIRE) Dola la Uthumani (OTTOMAN EMPIRE) na Dola la Mrima-(kilwa) (MRIMA EMPIRE) lakini kutokana na hila au ubinafsi wa wasomi wa kizungu (Eurocentric views) kwa makusudi wamefunika kabisa historia hii na kuifanya isahaulike kabisa hata bila soni moyoni mwao.

Lakin pia hata nchi yetu imeshindwa kuitambua historia hii kwa upana wake na kuifanya kuwa chanzo cha muhimili wa taifa letu la Tanzania katika historia na uchumi. Pia kasumba hii imeathiri mataifa yote yaani Kenya, Somalia, Msumbiji na hata Tanzania wote wameshindwa kuenzi historia hii ili iwe ni urithi wa vizazi vyetu na duniani kwa ujumla kwani wenzetu Ugiriki na Italia na mataifa mengine ya Ulaya wamegeuza historia kuwa ni moja ya muhimili muhimu sana wa uchumi mfano tu kwa Ugiriki kwani Ugiriki pekee huingiza US$ 11.4 bilion( karibu Tsh 26 Trilion) kwa mwaka kwajili ya urithi wa tasnia nzima ya historia.

Kwanin sisi tusiwekeze kwenye hili? Natamani sana kuendelea kuandika juu ya upembuzi yakinifu juu ya kile kinachoitwa kuwekeza kwenye "Curiosity asset" yani vitu vyenye urithi na manufaa ya pekee kabisa na vyenye mvuto wa hali ya juu. Hivyo basi itanibidi kwa namna yoyote ili niishie hapa kwa maana ya kuwa nitatafuta wasaa mwingine wa kuliandikia hili la kuwekeza kwenye "Urithi wa dunia" kwa upana wake.

Japokuwa kulieleza hili ni jambo la muhimu sana itanibidi sasa niandae makala ambayo nitaishauri Serikali yangu tukufu ya Tanzania namna ya kuwekeza kwenye eneo hili ili tuweze kunufaika na historia ya Dola la Mrima (Kilwa) kupitia kwenye nyanja za kiuchumi, kisiasa, kielimu na kifahari kama Taifa.

Sasa ningependa kuitua kalamu yangu kwa nukuu ya Mtawa (mwasisi) wa Dola la Rumi (Roma Empire) JURIUS KAISAR alisema " Enzi ni fahari kwa jamii kama itakukumbusha ufahari wako kwa jamii nyingine na ukubwa wa jamii(Dola) yako kwani hukufanya uwe na sauti kwa jamii nyingine iwapo kama utaenzi hiyo hadithi kipindi ambacho hauko nayo tena huo umiliki wako lakini utawafanya muwe mafahari kwa vizazi vingi vijavyo" 368 BC

"MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU BARIKI KIZAZI CHETU NA FIKRA ZAKE"

NDIMI: COMRED MBWANA ALLYAMTU
© copy rights reseved
®written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika kwa mawasliano
™Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.
Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234
Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail. Com

Thursday, November 23, 2017

UHASAMA KATI YA KOREA KASKAZINI NA KOREA KUSINI

Na Masudi Rugombana.

Mgogoro wa Peninsular ya Korea ni zao la vita baridi (cold war) kati ya Mataifa ya Kibepari ya Ulaya Magharibi na Mataifa ya Kijamaa ya Ulaya Mashariki. Ikumbukwe kuwa Korea ilikuwa moja chini ya Ukoloni wa Japan hadi mwaka 1945 baada ya Japan kushindwa vita kuu ya pili ya Dunia.

CHANZO CHA KUGAWANYIKA KWA
PENINSULA YA KOREA.
Chanzo cha mgawanyiko ni vita ya kumuondoa Mjapan katika peninsula ya Korea iliyoongozwa na Marekani na Urusi. Urusi ilianzisha mapambano ya kumuondoa Mjapani ikitokea Upande wa Kaskazini mnamo Mwezi August 1945. Kwa kuwa tangazo la Urusi la vita dhidi ya Japan liliungwa mkono na Mataifa ya Marekani na Uingereza kwenye mkutano wa Marais watatu wa nchi hizo uliofanyika Yalta, Crimea (Yalta Conference) mnamo August 4 hadi 11 Mwaka 1945, kwa kuhofia Peninsular yote ya Korea kuangukia mikononi mwa Urusi, Marekani iliiomba Urusi katika vita yake dhidi Japan huko Korea iishie kwenye mstari wa latitudo unaofahamika kama 38th Paralleh north unaogawa peninsula ya Korea pande mbili sawa za Kusini na Kaskazini. Upande wa kusini wa 38th Paralleh north kilikuwa kituo cha mwisho kwa majeshi ya Japan kujisalimisha kwa vikosi vya Marekani, na upande wa kaskazini ilikuwa kituo cha mwisho kwa majeshi ya Japan kujisalimisha kwa vikosi vya Urusi.


September 8, 1945 Majeshi ya Marekani yaliingia upande wa Kusini na kuanzisha Serikali ya kijeshi chini ya jeshi la Marekani baada ya vikosi vya Japan kusalimu amri na kuondoka.   Kwa hivyo 38th Paralleh north ukawa ndio mpaka unatenganisha majeshi ya Marekani upande wa kusini na Majeshi ya Urusi kwa upande wa Kaskazini.

38th Paralleh

Marekani na Urusi zilijaribu kutaka kuunganisha tena Korea lakini juhudi hizo zilikumbana na vikwazo kutokana na migawanyiko ya itikadi za kisiasa baina ya Wafuasi wa sera za kijamaa walioungwa mkono na  Urusi na Wale wa vuguvugu la utaifa (Nationalist) ambao waliegemea kwenye siasa za kibepari waliokuwa wakiungwa mkono na Marekani.

Kitendo cha Marekani na Urusi kuweka mbele itikadi zao za kibebari na Kijamaa ndicho kilikuwa chanzo cha kushindwa kuunganisha tena Korea kuwa nchi moja. Marekani ilipendekeza ufanyike uchaguzi wa kidemokrasia ili kuwapa fursa wananchi wa Korea kuchagua uongozi wao ambapo upande wa Kaskazini chini ya Urusi ulikataa mapendekezo hayo. Hali hii ilipelekea Marekani kuitisha uchaguzi upande wa Kusini na kumkabidhi nchi Mwanaharakati wa vita dhidi ya Ukoloni wa Japani Syngman Rhee August 15, 1948 ambaye alishinda kwa asilimia 92.


Urusi nayo mnamo 9 September 1948  ilimsimika Kiongozi wa Chama cha kikomunist Kim Il-Sung kuwa Rais wa Korea Kaskazini ya Kijamaa na Mwezi October Mwaka 1948 Urusi ilitangaza kumtambua Kim kuwa ndiye kiongozi halali wa Korea yote ikiwemo Korea Kusini.

NINI CHANZO CHA MGOGORO UNAOENDELA HADI SASA
Tawala zote mbili zilikataa kutambuana ambapo kila upande ulijitangaza kuwa ndiye mtawala wa peninsula yote ya Korea. Na msimamo huu umeendelea mpaka sasa. Baada ya Marekani na Urusi kujiondoa kijeshi kutoka Korea, hali ya wasiwasi na kutokuaminiana iliendelea katika eneo la mpaka wa nchi hizi mbili, ambapo kulikuwa na kushambuliana mara kwa mara baina ya pande mbili.

Hali hii ilipelekea Korea Kaskazini ikishauriwa na China na Soviety Union kuamua kuivamia kijeshi Korea Kusini June 25, 1950 na kufanikiwa kuuteka mji mkuu Seoul June 28, 1950. Kufuatia uvamizi huo June 27, 1950 baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura na kuidhinisha kupeleka Vikosi vya umoja huo ili kuiondoa kwa nguvu Korea Kaskazini kutoka kwenye ardhi ya Korea Kusini.

Urusi haikuhudhuria kikao hicho kwa sababu ilikuwa imesusia vikao vya baraza la usalama kuanzia mwezi January 1950 kupinga kiti cha China kwenye baraza hilo kukaliwa na Jamhuri ya China (Taiwan) badala ya Jamhuri ya Watu wa China (China Bara) hivyo haikuweza kupinga maamuzi hayo kwa kupiga kura ya turufu (Veto). Jeshi la Umoja wa Mataifa liliongozwa na Marekani ambayo ilitoa karibu asilimia 88 ya wapiganaji wote, huku ikiungwa mkono zaidi na wanachama wa NATO kama vile Uingereza, Canada, Uturuki na Ufaransa.

Vikosi vya umoja wa Mataifa chini ya Marekani vilianza rasmi vita ya kuiondoa Korea Kaskazini kutoka kwenye ardhi ya Korea Kusini July 2, 1950 ambapo vilifanikiwa kuukomboa mji mkuu Seoul mwezi September 1950 na kusonga mbele zaidi ndani ya Korea Kaskazini na kufanikiwa kuuteka mji mku Pyongyang October 19, 1950. Vikosi vya Marekani chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa vilisonga mbele zaidi kuelekea kwenye mpaka kati ya Korea Kaskazini na China. Hatua hii ilipelekea China kuingilia kati kijeshi kuisadia Korea Kaskazini kwa kudeploy askari Milion Moja. Urusi nayo iliiunga mkono China kwa kutuma ndege za kivita na wakufunzi wa kijeshi.

Vikosi vya China na Korea Kaskazini vilifanikiwa kuiondoa Marekani Kutoka Korea Kaskazini, na kuuteka tena mji mkuu Pyongayanga mnamo December 5, 1950. Vikosi vya China vilisonga mbele zaidi na kufanikiwa kuuteka  tena mji mkuu wa Korea Kusini (Seoul) January 1951. Marekani na washirika wake chini ya Mwamvuli wa UN walifanikwa kuuteka tena mji mkuu Seoul mwezi March 1951 na kuyarudisha Nyuma majeshi ya China hadi kwenye mpaka wa Korea mbili kabla ya vita. (The 38th parallel north). Marekani haikusonga mbele zaidi badala yake iliitaka China wakae kwenye meza ya Mazungumzo ili kuangalia namna ya kufikia makubaliano.

MAKUBALIANO YA KISITISHA VITA (ARMISTICE AGREEMENTS)
July 27, 1953 Korea ya Kaskazini ikiungwa mkono na china walifikia makubaliano ya kusimamisha Vita na Korea Kusini (armistice agreements) kwa kuchora mpaka mpya wa kijeshi (Military Demarcation Line-MDL)  ambao kwa jina lingine unajulikana kama armistice line unaozungukwa na eneo la kilometa nne kaskazini na kusini mwa mpaka lisiloruhusiwa kufanyika harakati za kijeshi (Demilitarized Zone-DMZ).

Mpaka wa Korea mbili baada ya Makubaliano
ya kusitisha vita July 27, 1953.

Tokea hapo hapajawahi kuwa na mkataba wa Kumaliza mgogoro baina ya Korea mbili huku kila upande ukiendelea kudai kuwa na mamlaka ya utawala wa Korea yote, wakati huo huo pande zote zikiendelea kujiimarisha kijeshi nje ya eneo la mpaka wa mataifa hayo mawili. Hali hii ya kutokuwa na mkataba wa kumaliza mgogoro ndio unaozifanya Korea zote mbili kuendeleza uhasama hadi sasa.

Ukinakili Makala zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
© Copy rights of this article reserved
®Written by Masudi Rugombana

Napatikana kupitia simu namba

+255743 184 044.
Email: masudirugombana@gmail.com



Sunday, November 19, 2017

MKATABA WA NYUKLIA WA IRAN (IRAN NUCLEAR DEAL-JCPOA) NI KITISHO KWA ISRAEL NA SAUDI ARABIA

Na Masudi Rugombana

Iran ilianza harakati za kumiliki technolojia ya Nyuklia miaka ya 1970 kwa kusaidiwa na Marekan wakati ikiwa chini ya utawala wa Mohammad Reza Pahlav (Shah) ambapo kinu cha kwanza cha Nyuklia cha Bushehr (Bushehr Nuclear Plant) kilijengwa na makampuni ya Kijerumani. Mpango huo ulisimama baada ya mapinduzi ya kiislamu yaliyoongozwa na Sayyid Ruhollah Khomein mwaka 1979 ambapo ilishuhudiwa baadhi ya wataalam wa Nyuklia wa Iran wakiikimbia nchi baada ya mapinduzi hayo.


Iran Ilianzisha tena mpango wa nyuklia miaka ya 1980 kwa kusaidiwa na Pakistan. Mwaka 2003 ilibainika kuwa kwa takribani miaka 18 Iran ilikuwa ikificha shughuli zake za nyuklia kinyume na mkataba wa kimataifa iliosaini mwaka 1968 unaozuia kuenea kwa silaha za nyuklia ( Treaty on the Non-Proliferation of Nuclear Weapons-NPT).
Katika kipindi hicho Iran ilijenga kwa Siri vinu viwili vya Nyuklia, kile cha maji Mazito cha Arak (Arak heavy water facility) na cha urutubishaji uranium cha Natanz (Natanz Uranium enrichment reactor).

Kituo cha uzalishaji maji mazito cha Arak
(Arak heavy water facility)


Mwezi February mwaka 2003 Rais Muhammad Khatami ilithibitisha uwepo wa vinu hivyo viwili na kusisitiza kuwa Iran ilikuwa inarutubisha kiwango kidogo cha Uranium kwa ajili ya kuzalisha umeme hatua iliyopelekea Wakaguzi kutoka Wakala wa Kimataifa wa nguvu za atomic (IAEA) kutembelea kinu cha Nyuklia cha Natanz. Mwezi May mwaka 2003 serikali ya Iran iliwaruhusu wakaguzi kutoka IAEA kutembelea Kampuni ya umeme ya Kalaye kwa masharti ya kutochukua sampuli zilizokuwa zikitumika kuzalisha umeme.

Hali hii ilipelekea Wakala wa Kimataifa wa nguvu za atomic katika ripoti yake ya June 2003 kulijulisha baraza la usalama la umoja wa mataifa kuwa Iran imeshindwa kufikia viwango vilivyoainishwa katika mkataba wa NPT hivyo kupelekea kuanzishwa kwa mazungumzo ya kidiplomasia baina ya Iran na nchi tatu za umoja wa Ulaya (The EU3) ambazo ni Ufaransa, Ujerumani na Uingereza na kufikia azimio kuwa Iran imekubali kushirikiana na Wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomic (IAEA).

Mwezi November Mwaka 2004 Iran na Jumuiya ya Ulaya zilifikia makubaliano jijini Paris (Paris accord) kuwa Iran Ifunge vinu vyake vya Natanz na Arak, isimamishe kurutubisha Uranium ikiwa ni pamoja na kutengeneza, kufunga, kufanya majaribio na kuendesha cenfrifuges wakati mazungumzo yakiendelea ili kufikia makubaliano ya muda mrefu.

Mwezi August 2005 Kiongozi mwenye msimamo mkali ambaye aliwahi kuwa meya wa Jiji la Tehran Mahmoud Ahmednejad alichaguliwa kuwa Rais wa Iran. Ahmednejad Aliwatuhumu kwa makosa ya Uhaini wajumbe wa Iran walioshiriki kwenye majadiliano ya mkataba wa Paris. Miezi miwili baadae Rais Mahmoud Ahmednejad aliiondoa Iran kwenye Mkataba wa Paris na kuvunja mazungumzo yaliyokuwa na lengo la kufikia makubaliano ya muda mrefu. Iran iliujulisha wakala wa kimataifa ya nguvu za atomic kuwa inaanzisha upya urutubishaji wa Uranium kwenye kituo chake cha Esfahan. Mnamo mwezi February mwaka 2006 Iran ilifungua kinu chake cha Natanz na mwezi June 2006 ilifungua kinu chake kingine cha Arak na hivyo kuendelea kurutubisha uranium kwa spidi ya kiwango cha juu.

Rais Mahmoud Ahmednejad akikagua kituo cha Nyuklia
cha Natanz.


Mwaka 2009 mwezi September, Rais Barack Obama aliishutumu Iran kwa kujenga kwa siri kinu kikubwa cha chini ya ardhi cha kurutubisha Uranium kwenye eneo la Fordow karibu na mji wa Qom. Kitendo cha Iran kujenga kinu kipya cha Nyuklia bila kuifahamisha IAEA  kilisababisha hofu kubwa katika jumuiya ya kimataifa iliyopelekea Israel kutishia kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran.

Mkurugenzi mkuu wa IAEA Dr. Mohammed El Baradei ilionya kuwa hatua za kijeshi dhidi  ya Iran zitasababisha janga kubwa na hivyo kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kukaa mezani na Iran kwa ajili ya kutafuta suluhisho kwa njia ya amani.

Mwezi March 2013 Marekani ilianzisha mazungumzo ya siri na maofisa wa Iran huko Oman yalioongozwa na Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani William Joseph Burns na mshauri wa masuala ya usalama wa Taifa wa Makamu wa Rais wa Marekani Jacob Jeremiah Sullivan (Jake Sullivan) ambapo kwa upande wa Iran yaliongozwa na Mwana Diplomasia nguli Ally Asghar Khaji naibu Waziri wa mambo ya nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya Ulaya na Amerika. Katika mazungumzo hayo hapakuwa na muafaka uliofikiwa.

Mwaka 2013 mwezi June Mwanasiasa mwenye msimamo wa wastani Hassan Rouhan alichaguliwa kuwa rais wa Iran. Siku tatu baada ya kuchaguliwa Rais Hassan Rouhani alitoa wito wa kufufuliwa mazungumzo thabiti ya kumaliza mgogoro wa nyuklia kati ya Iran na mataifa ya Magharibi yatakayoshirikisha nchi 5 wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa pamoja na Ujerumani (P5+1).

September 2013, Rais wa Marekani Barack Obama alizungumza kwa njia ya Simu na Rais Hassan Rouhan yakiwa ni mazungumzo ya kwanza kwa viongozi wa ngazi ya juu wa nchi hizo tangu yalipotokea Mapinduzi matukufu ya Kiislamu mwaka 1979. Mazungumzo hayo yalifuatiwa na mkutano kati ya Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na Mwenzake wa Iran Muhammad Javad Zarif hivyo kuashiria kuwa Madola hayo mawili yameamua kuanzisha ushirikiano wa wazi. Huo ndio ukawa mwanzo wa kuanzishwa kwa Mazungumzo ya Nyuklia ya Iran yaliyopelekea kusainiwa kwa mkataba wa JCPOA.

JCPOA:
Mkataba wa nyuklia wa Iran ambao unajulikana kama  (JCPOA-The Joint Comprehensive Plan of Action- kwa Kiswahili Mpango wa kina wa utekelezaji wa pamoja) ni makubaliano ya kimataifa kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran yaliyofikiwa huko Vienna nchini Switzeland mnamo 14 July 2015. Makubaliano hayo yalifikiwa kati ya Iran na nchi tano wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa Mataifa ambazo ni China, Ufaransa, Urusi, Marekani na Uingereza  jumlisha na Ujerumani au kwa kifupi P5+1.

Wajumbe wa P5+1 na Iran wakiwa Vienna Uswiz kwenye
mazungumzo ya kutanzua mzozo wa nyuklia wa Iran.Kutoka
kushoto ni Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry, Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond, Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, Mkuu wa sera za nje wa Jumuiya ya Ulaya Bi Catherine Ashton na Waziri wa Mambo ya nje wa China Wang Yi.



Mkataba huo uliosainiwa baada ya majadiliano ya kina yaliyodumu kwa miaka miwili kwa lengo la kuzuia Iran kutengeneza silaha za Nyuklia.
Chini ya makubaliano hayo ya JCPOA, Iran alikubali kuondoa akiba yake yake ya uranium iliyokuwa tayari imerutubushwa kwa kiwango cha kati (medium-enriched uranium), kuondoa hadi asilimia 98 ya akiba ya uranium iliyokuwa imerutubishwa kwa kiwango cha chini ( low-enriched uranium ) na kupunguza kwa karibu theluthi mbili ya idadi ya centrifuges kwa miaka kumi na tatu.

Mkataba unairuhusu Iran kutumia maji mazito kutoka kwenye kinu chake cha Arak kwa ajili ya shughuli za viwanda na utafiti na kuuza ziada inayobaki ya maji mazito kwenye soko la kimataifa.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, kwa miaka kumi na tano ijayo Iran itakuwa ikirutubisha uranium hadi asilimia 3.67 tu. Pia Iran ilikubali kutojenga vituo vyovyote vipya vya maji mazito (heavy-water facilities ) katika kipindi  hicho cha miaka kumi na tano. Mkataba unataka katika kipindi cha miaka kumi urutubishaji wa Uranium ufanyike katika kituo kimoja kwa kutumia idadi ya first generation centrifuges 5,060 tu badala ya 19,060 ambapo Iran inatakiwa kutenganisha (disconnect) centrifuges 14000, pia vituo vingine vitabadilishwa matumizi ili kuepuka urutubishaji wa iranium.

Kufuatilia na kuhakikisha kuwa Iran inatekeleza makubaliano, Mkataba unataka wakaguzi kutoka Wakala wa kimataifa wa nguvu za atomic (IAEA) ambao idadi yao itaongezwa kutoka 50 hadi 150 waruhusiwe kufika mara kwa mara kwenye vituo vyote vya nyuklia vya Iran kwa ajili ya ukaguzi kuanzia kwenye viwanda vya Uranium hadi kwenye ununuzi wa technolojia zinazohusiana na nyuklia.

Mkataba unairuhusu IAEA kufunga vifaa vya kisasa (sophisticated monitoring technology) kama fibre-optic seal, survaillance camera, radiation-resistant Cameras na infrared satelite imagery ili kufuatilia kwa karibu zaidi nyendo za Iran katika vituo vyake vya Nyuklia. Kama wakaguzi watatilia shaka kuwa Iran inaendeleza program ya Nyuklia kwenye maeneo ambayo hayajatangazwa (non-declared sites) wataomba ruhusa ya kuingia kwenye hayo maeneo ambapo mkataba unataka wakaguzi kutoka wakala wa Kimataifa wa nguvu za atomic watakao husika kuingia katika maeneo hayo watoke kwenye nchi ambazo zina uhusiano wa kidiplomasia na Iran.

VIKWAZO
Mkataba unaeleza kwamba IAEA itakapothibitisha kuwa Iran imetekeleza makubaliano , vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na Marekani, Umoja wa Mataifa (UN) na Jumuiya ya Ulaya (EU) vitaanza kuondolewa ndani ya miezi sita tokea kusainiwa kwa mkataba na ndani ya miaka nane tokea kusainiwa kwa makubaliano, vikwazo dhidi ya makampuni ya Iran, makombora ya kibalistiki, taasisi na watu binafsi vilivyowekwa na Jumuiya ya Ulaya vitasitishwa . Hata hivyo vikwazo visivyohusiana na masuala la Nyuklia vilivyowekwa na Marekani kama vile ukiukwaji wa haki za binadamu, makombora na kufadhili ugaidi havitaathiriwa na makubaliano haya ya JCPOA.

NANI AMEFAIDIKA
Marekani na mataifa ya Ulaya wamefanikiwa kuizuia Iran  kutengeneza silaha za nyuklia kwa muda wa miaka 15. Na baada ya kumalizika kwa mkataba itachukua mwaka mmoja kwa Iran kurudisha program yake ya nyuklia katika kiwango ilichofikia kabla ya kusainiwa kwa mkataba wa JCPOA.

Makubaliano haya yamesaidia kwa kiasi kikubwa kulifanya eneo la Mashariki ya kati na Dunia kwa ujumla kuwa salama zaidi kutokana na kitisho cha kusambaa kwa silaha za nyuklia kwani Marekani na Washirika wake walikuwa na wasiwasi kuwa ikiwa Iran ingefanikiwa kumiliki zana za kinyuklia kungekuwa na uwezekano mkubwa kwa zana hizo kuingia mikononi mwa makundi ya Hizbullah na Ansarullah Movement (Houthis) ambayo Marekani na Washirika zake inayachukulia kama makundi ya kigaidi.

Kwa upande wa Iran, mkataba huu umeiwezesha kujiondoa kwenye kitanzi cha kutengwa na jumuiya ya kimataifa, kuiwezesha kufanya biashara na mataifa makubwa hivyo kuongeza mauzo ya mafuta nje ya nchi. Iran pia imeweza kupata mapato ya dola bilion 30 za Kimarekani kati ya dola bilioni 100 ambazo ni sehemu ya fedha zake zilizokuwa zimezuiwa kwenye mabenki mbalimbali duniani. Kwa muda mfupi toka kusainiwa kwa mkataba Iran imeweza kusaini mikataba ya uwekezaji yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 60. Pia mkataba umefungua njia kwa Iran kuweza kununua vifaa na technolojia za kisasa kama ndege za abiria, mitambo na vipuri  kutoka kwenye makampuni ya kigeni kama vile Boeng, Airbus n.k.

Pia mkataba umeiwezesha Iran kuongeza mapato zaidi kupitia mpango wake wa kuzalisha maji mazito kwenye kituo chake cha Nyuklia cha Arak. Mwaka 2016 Marekani ilitiliana saini mkataba na Iran ambapo Iran iliiuzia Marekani tani 32 za maji mazito yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 8.6 yatakayotumika kwa ajili ya viwanda na utafiti. Urusi pia mwezi April 2016 ilisaini makubaliano na Iran ambapo Iran iliiuzia Urusi tani 38 za maji mazito (heavy water) yatakayotumika katika viwanda vyake vya zana za kinyuklia pamoja na shughuli za utafiti.

HOFU YA ISRAEL NA SAUDI ARABIA.
Saudi Arabia na Israel ni mataifa ambayo hayajaridhishwa kabisa na kufikiwa kwa makubaliano haya ya JCPOA. Mataifa haya yanauona mkataba huu kama ni kitisho kikubwa kwa usalama wao na eneo zima la mashariki ya kati. Waziri mkuu wa Israel Binyamini Netanyahu aliwahi kuyaita makubaliano hayo kuwa ni mabaya (bad deal)

Israel na Saudi Arabia zinalalamika kwamba Mkataba umeshindwa kuibana Iran kuachana na mpango wa nyuklia badala yake unaibana Iran kusimamisha tu mpango wake wa  nyuklia na mara tu mkataba utakapofikia kikomo ndani ya muda mfupi Iran itakuwa na uwezo wa kurudisha program yake kama awali na kuweza kuunda bomu la nyuklia.

Programu ya Makombora ya Kibalistiki ya Iran inayotishia usalama wa Israel na Saudi Arabia.

Israel na Saudi Arabia zinalalamikia hatua ya Iran kuruhusiwa kuchukua pesa zake ambazo ni mabilioni ya dola yaliyokuwa yamezuiliwa kutaiongezea uwezo mkubwa zaidi wa kuendeleza programu yake ya kutengeneza makombora ya kibalistiki ya masafa marefu ambayo ni kitisho kikubwa kwa usalama wao, kufadhili makundi ya Hizbullah, Hamas na Houthis makundi ambayo nchi hizo zinayachukulia kama makundi ya kigaidi na kitisho kikuwa kwa usalama wao.

Ukinakili Makala zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
© Copy rights of this article reserved
®Written by Masudi Rugombana

Napatikana kupitia simu namba

+255743 184 044.
Email: masudirugombana@gmail.com



Wednesday, November 15, 2017

ISRAEL HAIKUPIGANA PEKE YAKE KATIKA VITA YA SIKU SITA (THE SIX DAY WAR)

Na Masudi Rugombana.

Vita ya siku sita (Six day war or 1967 Arab–Israeli War, or Third Arab–Israeli War) ilipiganwa kati ya June 5 hadi 10, 1967. Vita ilihusisha Israel, Marekani na Uingereza dhidi ya Mataifa ya kiarabu ya Misri, Jordan, Syria na Lebanon yakiungwa mkono na Urusi kwa kuuziwa silaha. Vita hii ilikuwa ni muendelezo wa uhasama ulioanza tangu mwaka 1948 kati ya Israel na Wapalestina  uliotokana na kuzaliwa kwa Taifa la Israel. Marekani na Uingereza zilishiriki katika vita hii kwa lengo la kuilinda Israel na kukabiliana na ushawishi wa Urusi katika mataifa ya Kiarabu ambao ulikuwa ni kitisho kwa maslahi ya kiuchumi ya Marekani.

Vifaru vya Israel aina ya Centurion vikiwa katika maandalizi ya vita Mwezi June, 1967.


Ingawa kulikuwa na hali tete baina ya mataifa ya kiarabu na Israel kwa muda mrefu tangu kuanzishwa kwa Taifa la Israel, lakini chanzo kikuu cha vita hii ya siku sita kilisababishwa na Misri kukiuka sheria za kimataifa baada ya kuizuia Israel kutumia mlango bahari wa Tiran kwa ajili ya kupitisha meli zilizokuwa zinasafirisha shehena ya mafuta kutoka Iran kwenda Israel. Iran ndio kilikuwa chanzo kikuu cha Mafuta kwa taifa la Israel. Hatua hiyo ya Misri ilipelekea Israel kuanzisha vita kwa shambulizi kubwa la kushtukiza dhidi ya jeshi la anga la Misri mnamo June 05, 1967.
Mlango bahari wa Tiran


Katika makala hii fupi kuhusiana na vita vya siku sita nimeamua kuandika ukweli ambao vyombo vya habari vya Israel, vyombo vya habari vya mataifa ya magharibi na mashabiki wa Israel ambao baadhi yao ushabiki wao unatokana na shinikizo la kiimani zaidi hawataki kuusikia wala kuuandika katika makala zao. Ukweli huu ni kwamba ISRAEL HAIKUPIGANA PEKE YAKE KATIKA VITA YA SIKU SITA. 

Wakati Misri ilipofunga mlango bahari wa Tirane (Tiran straits)  Mei 22-23, 1967 mwezi mmoja kabla ya vita ili kuzuia meli zisipeleke mafuta Israel, Rais wa Marekani wakati huo Lyndon Johnson aliionya Misri kuwa kitendo hicho ni sawa na Tangazo la vita kwa kuwa kinakiuka sheria za kimataifa. Rais Johnson alikwenda mbali zaidi kwa kuiambia Misri kuwa ikiwa vita itatokea basi Israel haitakuwa peke yake, labda yenyewe itake kwenda vitani peke yake (Israel will not be alone unless it decides to go alone.)

May 26, 1967 Shirika la upelelezi la Marekani la CIA  lilitoa taarifa za kiintelijensia zikikadiria kuwa Israel kama itaingia vitani kwa wakati huo basi itawachukua wastani wa siku 7 hadi 10 kushinda vita. Israel yenyewe iliamini kuwa ingekuwa na uwezo wa kushinda vita ndani ya siku tatu au nne. Huu ni ushahidi wa namna Israel ilivyokuwa ikisaidiwa kiintelijensia na CIA katika vita ya siku sita.

Katika kitabu chake cha Six Days, aliyekuwa mwandishi wa BBC (BBC Correspondent based in Jerusalem) Jeremy F. J. Bowen anasema kwamba June 4, 1967, meli ya Israel iliyopewa jina la Miryam iliondoka katika bandari ya Felixstowe ikiwa imebeba Makontena ya machine guns, 105 mm tank shells, na magari ya kivita kuelekea Israel. Huo ulikuwa ni muendelezo wa shehena kubwa a silaha zilizokuwa zinatumwa kwa siri kutoka nchini Uingereza na Marekani kwa ajili ya maandalizi ya vita ya siku sita. Bowen anaandika kwamba Waziri Mkuu wa Uingereza Mr. Harold Wilson alimwandikia barua ya siri Waziri mkuu wa Israel Mr. Levi Eshkol akimhakikishia kuwa Uingereza itakuwa bega kwa bega na Israel katika uwanja wa mapambano.

Kwa mujibu wa Mwandishi mashuhuri wa Marekani na mchambuzi nguli wa siasa za mashariki ya kati George Lenczowski, akiizungumzia vita ya siku sita, aliandika kuwa mnamo tarehe 23 May 1967 siku moja baada ya Marekani kuionya Misri kuwa kuizuia Israel isipitishe meli kwenye mlango bahari wa Tiran ni sawa na Tangazo la vita, Rais Lyndon Johnson aliidhinisha kwa siri kupelekwa kwa shehena ya zana za kivita nchini Israel kwa njia ya ndege hivyo kukiuka marufuku ya kupeleka silaha katika eneo la Mashariki ya kati yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa.

Mwaka 1993 wakati akifanya mahojiano katika maktaba ya The Johnson Presidential Library oral history archives, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani wakati wa vita ya siku sita, Robert Strange McNamara alikiri kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani iliamuru Meli ya Kivita (Air Craft carrier) iliyokuwa imebeba ndege za kivita kuelekea mashariki ya bahari ya Meditereania kwa lengo la kuisadia na kuilinda Israel katika vita iliyotarajiwa kuanza wakati wowote.

Pia Meli ya upelelezi (Spy Ship) ya USS Liberty nayo ilipelekwa katika peninsular ya sinai ili kuchunguza na kuipa taarifa Israel kuhusiana na harakati za jeshi la Misri. Wakati vita ilipokuwa imepamba moto usiku, ndege za kivita za Israel ziliishambulia kimakosa meli hii katika peninsula ya Sinai upande wa bahari ya mediterania zikidhani ilikuwa ni meli ya kivita ya Misri. Shambulizi hili lilisabisha vifo vya askari 34 wa Marekani na wengine 171 walijeruhiwa, pia meli iliharibika vibaya. Israel iliomba msamaha kwa shambulio hilo, pia ililipa fidia kwa familia za askari waliouawa na kujeruhiwa.

Meli ya upelelezi ya Marekani USS Liberty


June 9, 1967, katika hotuba yake ya kujiuzulu Rais Gamal Abdel Nasser alisema kuwa Manowari za kivita (Air craft Carriers) za Marekani na Uingereza zilikuwa katika pwani ya Israel zikisaidia jeshi la anga la Israel kushambulia safu za mbele za askari wa Misri na Syria. Abdel Nasser alisema kuwa "bila kutia chumvi jeshi la anga la adui linafanya mashambukizi ya anga yenye nguvu mara tatu ya uwezo wake wa kawaida ("... Indeed, it can be said without exaggeration that the enemy was operating with an air force three times stronger than his normal force")Hata hivyo ombi lake la kijiuzulu lilikataliwa.

Siku ya pili tokea kuanza kwa vita vyombo vya habari vya kiarabu viliripoti uwepo wa majeshi ya Marekani na Uingereza yakipigana bega kwa bega upande wa Israel. Radio Cairo na Gazeti la Serikali ya Misri la Al-Ahram ziliripoti kwamba Marekani pia ilikuwa ikifanya Mashambulizi Mazito ya anga dhidi ya Misri kutoea kwenye Manowari yake (Aircraft carrier) iliyokuwa kwenye kituo chake cha kijeshi cha Wheelus Air base cha huko Libya, pia American Spy Satelite ilikuwa ikituma picha za mienendo ya majeshi ya Waarabu kwa jeshi la Israel.

Ikumbukwe kuwa miongoni mwa sababu zilizopelekea Muamar Gaddafi kupindua Serikali ya Libya tarehe 1 September 1969 ni hiki kitendo cha kuruhusu Marekani Kushambulia Majeshi ya Misri ikitokea katika pwani ya Libya wakati wa vita ya siku sita. Pia iliripotiwa kupitia radio Damascus kuwa Mfalme Hussein wa Jordan binafsi alithibitisha kuwa radar za Jordan zilionyesha ndege za kivita za Uingereza zikiruka kutoka kwenye Air craft Carrier iliyokuwa karibu na pwani ya Israel nakufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya Waarabu.

Katika vita hii Israel, Marekani na Uingereza waliibuka na Ushindi mkubwa ulioiwezesha Israel kuongeza eneo lake la ardhi baada ya kufanikiwa kuiteka milima ya Golan kutoka Syria, Ukanda wa Gaza kutoka Misri na eneo la West bank kutoka Jordan.

Ramani inayoonyesha ushindi wa Israel baada ya vita ya siku sita.
Eneo la Sinai ambalo pia lilitekwa, lilirudishwa mikononi mwa Misri baada ya Makubaliano ya amani yalitokana na vita ya Yom Kippur.

Ukinakili Makala zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
© Copy rights of this article reserved
®Written by Masudi Rugombana

Napatikana kupitia simu namba

+255743 184 044.
Email: masudirugombana@gmail.com

Sunday, November 12, 2017

UJUE MGOGORO KATI YA CHINA NA TAIWAN

Na Masudi Rugombana.

Mgogoro unaoendelea sasa baina ya China na Taiwan ni matokeo ya mivutano ya tofauti za mitazamo ya kisiasa ya wafuasi wa vuguvugu la utaifa (Nationalist ) wenye kupendelea mfumo wa uchumi wa Kibepari waliokuwa wakiungwa mkono na Marekani dhidi ya wafuasi wa sera za kiuchumi za kijamaa (Communist) waliokuwa wakiungwa mkono na Soviet Union. Mivutano hii iliendelea kwa muda mrefu hadi kupelekea pande mbili kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kugombania madaraka.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China (The Chinese Civil War) ilipiganwa kuanzia mwaka 1927 hadi mwaka 1949. Vita ilihusisha wafuasi wa Nationalist wa Chama chenye mrengo wa kibebari cha  Kuomintang (KMT) kilichokuwa kinatawala Jamhuri ya China dhidi ya Wafuasi wa sera za kijamaa wa Chama cha upinzani cha  Kikomunist cha China (CPC).

Vita ilipiganwa katika hatua mbili, hatua ya kwanza ni kuanzia Mwaka 1927 hadi mwaka 1937 ambapo vita ilisitishwa na pande mbili hasimu ziliungana ili kukabiliana na kitisho ya jeshi la Japan, lengo la kuungana lilikuwa ni kuilinda China isisambaratike. Pande hasimu zilirudi tena kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe Mwaka 1946 baada ya kitisho cha Japan kumalizika.
Mwaka 1949  Wakomunist wakiongozwa na Mao Tse Tung walishinda vita na kuitimua madarakani Serikali ya Rais Chiang Kai-shek wa Chama cha kibebari cha Kuomintang (KMT) kisha kuunda Jamhuri ya Watu wa China (People's Republic of China-PRC).

Baada ya kushindwa vita, Mwaka 1949 serikali ya Kuomintang chini ya jenerali Chiang Kai-shek na mabaki ya jeshi lake pamoja na wafuasi wake wengi ilihamia kwenye Kisiwa cha Taiwan na visiwa vingine vidogo vinavyoizunguka Taiwan ambapo waliendelea kutawala huku wakisisitiza kuwa serikali yao ndiyo serikali halali ya Jamhuri ya China. Wakomunisti walikosa nguvu ya kuwafuata hadi kwenye visiwa kutokana na vitisho vya Marekani. Hivyo serikali katika kisiwa cha Taiwan iliendelea kujiita "serikali halali ya Jamhuri ya China" (Republic of China-ROC) na kutangaza shabaha yake ya kuikomboa China yote kutoka mikononi mwa Chama cha kikomunist cha Mao Tse Tung.

Wakati huo huo Serikali ya Kikomunist huko China Bara nayo ilijitangaza kuwa ndio serikali halali ya China yote huku ikitangaza shabaha yake ya kukikomboa kisiwa cha Taiwan kutoka mikononi wa wafuasi wa chama cha Kuomintang na kukiunganisha tena na Jamhuri ya watu wa China. 
Serikali ya Chama cha Kuomintang katika kisiwa cha Taiwan iliendelea kutambuliwa na umoja wa mataifa kuwa ndiye serikali halali ya China na ilikalia kiti cha China katika umoja wa mataifa hadi tarehe 25 Oktoba 1971 ambapo mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa uliamua kwamba Jamhuri ya Watu wa China (PRC) iwe mwakilishi halisi wa China kwenye Umoja wa Mataifa (UN) , hivyo Jamhuri ya China (Taiwan) ilifukuzwa. Hali hii ilipelekea Mataifa mengi zaidi ikiwemo Marekani na Washirika zake kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Kufunga ofisi zao za ubalozi huko Taiwan

Kwa kuwa hakuna mkataba wa amani uliofikiwa baina ya pande mbili hasimu mpaka sasa, kila upande bado unaamini kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe baina yao bado havijamalizika.

 
KUIBUKA KWA SERA YA CHINA MOJA (ONE CHINA POLICY)
Serikali zote mbili yaani Jamhuri ya China (Taiwan) na Jamhuri ya watu wa China ( China Mainland-Beijing)ziliweka msimamo wa kuitambua China moja tu (One China Policy) hivyo basi ziliweka sharti kwa mataifa mengine kuwa hayaruhusiwi kuwa na uhusiano rasmi na serikali zote mbili kwa pamoja kwa madai kuwa kufanya hivyo kunachochea mgawanyiko wa China. Hivyo kama nchi fulani itakuwa na uhusiano rasmi na Jamhuri ya China (Taiwan) italazimika kuvunja uhusiano rasmi na Jamhuri la watu wa China (China Mainland-Beijing) au kinyume chake(vice versa).

FAIDA NA HASARA ZA SERA YA CHINA MOJA (ONE CHINA POLICY) KWA PANDE ZOTE MBILI.
Jamhuri ya watu wa China (China Mainland) imenufaika zaidi na sera hii kwa kufanikiwa kupata uungwaji mkono kidiplomasia kutoka mataifa mengi.Katika bara la Africa, Burkina faso ndiyo nchi pekee yenye uhusiano rasmi na Taiwan huku ikiwa haina uhusiano wowote na China. Afrika kusini, Libya na Nigeria zina uhusiano rasmi na China wakati huo huo zikiwa na uhusiano usio rasmi na Taiwan. Mataifa mengine yote ya bara la Afrika yana uhusiano rasmi na China bila kuwa na uhusiano usio rasmi na Taiwan.  98% ya mataifa yote Duniani (Yakiwemo mataifa yote Makubwa) yana uhusiano rasmi na China. Hali hii inaipa China nguvu ya kuendelea kuichukulia Taiwan kama jimbo lake lililojitenga. Hata hivyo Uhusiano  wa kijeshi unaoendelea kunawiri kati ya Taiwan na Marekani umekuwa ni kitisho kwa Jamhuri ya Watu wa China.

Kwa upande wa Taiwan, sera hii imewawezesha kuendelea kujitawala bila kusumbuliwa. Pia imekuwa na uhusiano usio rasmi na mataifa yote ya Ulaya Magharibi, Amerika na baadhi ya mataifa ya Asia. Ingawa kuna harakati nyingi za kijeshi kwenye eneo la mlango bahari wa Taiwan (Taiwan strait) unaotenganisha nchi hizi mbili bado raia wa nchi hizi mbili wanatembeleana na ikiwa ni pamoja na kufanya biashara. Inakadiriwa kuwa raia milioni mbili wa Taiwan wanaishi na kufanya kazi China. Pia uungwaji mkono kiuchumi kutoka kwa  Marekani na Washirika zake umeifanya Taiwan kuwa miongoni mwa Mataifa yaliopiga hatua kubwa Kimaendeleo huku ikishika nafasi ya 21 kwa kuwa na uchumi mzuri duniani. Hasara iliyopata Taiwan ni kutengwa kidiplomasia na mataifa mengi Duniani.

Ukinakili Makala zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
© Copy rights of this article reserved
®Written by Masudi Rugombana

Napatikana kupitia simu namba

+255743 184 044.
Email: masudirugombana@gmail.com