Saturday, October 1, 2016

DUTERTE: NITAENDELEA KUUWA WAUZA UNGA KAMA HITLER ALIVYOUWA WAYAHUDI

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amejifananisha na kiongozi wa zamani wa Ujerumani Dikteta Adolf Hitler katika vita vyake dhidi ya walanguzi na watumiaji wa dawa za kulevya.
Rais Rodrigo Duterte


Amesema anaweza kuua walanguzi wengi wa dawa hizo za kulevya sawa na alivyofanya Hitler akiua Wayahudi wakati wa vita kuu ya pili ya dunia
"Hitler aliua Wayahudi milioni tatu ... kuna watumiaji milioni tatu wa dawa za kulevya hapa Ufilipino. Ningefurahi sana kuwaua," alisema bwana Duterte katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Davao.

Wayahudi zaidi ya milioni sita waliuawa na Wanazi chini ya Hitler.

Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino


Tangu aapishwe kuwa Rais wa Ufilipino June 30 mwaka huu, zaidi ya watumiaji na wauza madawa ya kulevya 3100 wameuwawa katika operesheni za police na makundi ya kiraia.

Duterte amesisitiza kuwa Marekani na nchi za jumuiya ya Ulaya hawana mahala pakuishutumu nchi yake kwa sababu ya unafiki wao wanaoendelea kuufanya katika nchi za mashariki ya kati kwa kuviunga mkono vikundi vya waasi vinavyoua maelfu ya watu wasiokuwa na hatia huku vikiwabaka wanawake na watoto.

No comments:

Post a Comment