Saturday, October 1, 2016

NDEGE ZA AINA YA BOMBARDIER NI MKOMBOZI KWA SAFARI ZA NDANI


Na Masudi Rugombana.

Kumekuwa na mjadala mkali unaoendelea hapa nchini kuhusiana na ndege mpya za ATCL aina ya Bombadier Dash 8 Q400. Ndege za kwanza kabisa kununuliwa na serikali kwa ajili ya usafiri wa ndani tangu mwaka 1978.


Kwa kuzingatia changamoto zinazoikabli sekta ya usafiri wa anga nchini hasa kwa upande wa gharama za uendeshaji na ubora wa viwanja vyetu vya ndege, matumizi ya ndege zinazotumia gharama ndogo ya uendeshaji na zenye uwezo wa kutua katika viwanja vyenye ubora mdogo ndio suluhisho sahihi wakati nchi ikiendelea kuimarisha miundo mbinu ya usafiri wa anga.

Shirika letu la ndege lilikufa kwa sababu ya kushindwa kujiendesha kutokana na gharama kubwa za uendeshaji pamoja na ufinyu wa abiria wanaotumia usafiri wa anga uliosabishwa na gharama kubwa ya nauli za ndege.

Mwanzo ilidhaniwa labda ni wizi unafanyika lakini baada ya utafiti uliofanywa ili kujua gharama chache za uendeshaji ikaonekana ni sawa kwa shirika hili kushindwa kujiendesha.
Kwa nini nchi imefanya ununuzi wa ndege aina ya Bombardier badala ya boeing kwa ajili ya usafiri wa ndani?


BOEING. Ndege aina ya Boeing inauzwa kwa dola za Marekani milioni mia mbili tisini na sita (US296 millions) wakati ndege aina ya Bombardier Q400 inauzwa dola za Marekani milioni 35 tu (US35millions.

Hesabu yake

Ili kununua bombardier tisa unahitaji dola za Marekani milioni 315. Sasa ukichukua dola hizo milioni 315 ukatoa dola milioni 296, utakuwa umebakiwa na dola milioni 19.
Ambapo hizi Bombardier tisa zingetusaidia kwa upande wa shirika kujiendesha lenyewe na kutupatia faida kubwa mara tisa ya boeing.
Kuhusu kasi (speed) ya Boeing ni sahihi kabisa kwamba ni kubwa kuliko Bombardier kutokana na uchomaji wa mafuta, speed yake ni 590mph wakati speed ya Bombardier ni 414mph au 667km/h.
Kama kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ni Km 1,100 maana yake Bombardier itatumia saa moja na dakika arobaini (1 hr and 40mnts) wakati Boeing itatumia saa moja na dakika kumi na tano (1hr and 15 mnts) tofauti iliyopo hapa dakika 25 tu.
Boeing inatumia dumu moja la mafuta la lita 4 kwa sekunde moja kwa hiyo kwa saa moja inatumia lita elfu kumi na nne mia nne (14,400) (4l×60s×60m)
Kwa mfano, mafuta ya ndege kwa lita yakiuzwa shilingi 2,000 maana yake ili tutie mafuta ya kuelekea safari ya Songea inayochukua takriban saa moja tu tunahitaji milioni 28,800,000 (14,400×2000). Na tunahitaji abiria 96 watakaolipa Tsh 300,000 ili kuweza kulipia gharama za mafuta tu.
Ukijumuisha gharama za ‘service’ na wafanyakazi utakuta faida inayopatikana ni ndogo sana au hakuna kabisa.

Bombardier inatumia lita 1.187 ya madumu ya mafuta kwa mile moja yaani ukikadiria inatumia lita moja ya mafuta kwa mile moja (1mile=1.6kms)
Umbali wa Songea hadi Dares Salaam (Air Distance) ni takribani kilometa 537 sawa na miles 335.625.

Kwa hiyo itatumia lita 398.386875 ambazo ukizizidisha kwa gharama ya Tsh 2,000 kwa lita unapata laki saba tisini na sita elfu mia saba sabini na tatu (796,773). Swali la kiuchumi, jambo gani muhimu kati ya kugharimika 28,800,000 na kugharimika 797,000?

Bombardier Dash 8 Q400

Kwa mtu yeyote mwenye mawazo tulivu na mwenye kutaka shirika hili kujiendesha kwa kibiashara ni lazima atumie Bombardier ili apate faida.


Pia kutokana na hali ya viwanja vyetu ndege hizi zinafaa kwa sababu zinaweza kutua katika viwanja vya kawaida na ndiyo maana serikali ilizinunua ndege hizi mahususi kwa safari za ndani!

Ni jambo lisilokubalika kabisa kutenga bajeti ya serikali iende ikahudumie shirika la ndege ambalo ukitumia akili ya kiuchumi linaweza kujiendesha na likaliletea taifa faida.

No comments:

Post a Comment