Mshauri wa Kiongozi wa kidini wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Masuala ya Kimataifa amesema tabia zisizo na mantiki za Rais Donald Trump wa Marekani zinaashiria kuwa hajui siasa wala hana ufahamu kuhusu mambo ya historia.
Dr. Ali Akbar Velayati amesema matamshi ya kibabe ya Trump yanaonyesha wazi kuwa hana ujuzi wowote katika masuala ya siasa na diplomasia na ni mtu ambaye amekulia katika ulimwengu wa biashara.
Dr. Ali Akbar Velayati |
Rais Donald Trump wa Marekani
|
Dr. Velayati amesisitiza kuwa makubaliano ya JCPOA yalipasishwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na hivi sasa yanatambuliwa kuwa ya kimataifa. Ameongeza kuwa, wanachama wengine wa kundi la 5+1 wanapasa kuilazimisha Marekani isikengeuke fremu iliyoainishwa na wakala wa shirika la nguvu za atomic (IAEA)na mazungumzo ya JCPOA.
Siku ya IjumaaTrump alitoa matamshi yasiyo na msingi na kukariri tuhuma zisizo na maana za huko nyuma dhidi ya taifa la Iran; akidai kuwa Iran haijaonyesha moyo wa dhati katika kufungamana na makubaliano hayo ya nyuklia.
Aidha alikariri madai yake ya huko nyuma yasiyo ya kimantiki kwamba Tehran inaunga mkono ugaidi.
Source: Pars today.
No comments:
Post a Comment