Wednesday, February 15, 2017

Waziri wa mambo ya nje wa Oman aikosoa Saudi Arabia kwa kupendelea vita


Muscat.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Yusuf bin Alawi ameikosoa Saudi Arabia kutokana na kushupalia utumiaji njia za kijeshi badala ya diplomasia kwa ajili ya kutatua migogoro ya eneo la Mashariki ya Kati.

Waziri wa mambo ya nje wa Oman bwana Yusuph bin Alawi
Akizungumza katika mahojiano aliyofanyiwa na kanali ya televisheni ya Kiarabu ya Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman ameashiria kushupalia Saudia utumiaji njia za kijeshi kwa ajili ya kutatua migogoro ya eneo na kueleza kwamba: Badala ya njia za kjeshi, matatizo na migogoro ya eneo inapasa itatuliwe kwa njia za kidiplomasia.

Akizungumzia safari aliyofanya nchini Syria, Bin Alawi ametetea hatua yake hiyo kwa kueleza kwamba: Syria ni nchi ya Kiarabu na Oman haijavunja uhusiano wake wa kidiplomasia na nchi hiyo.


Kuhusu upatanishi wa nchi yake kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Yemen, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amesema, kitu kinachopewa umuhimu na Oman ni kusimamishwa vita na kutatuliwa hitilafu zilizopo kulingana na matakwa ya wananchi wa Oman.

Yusuf bin Alawi amesisitizia pia nchi za eneo hili kupambana na ugaidi na kueleza kwamba magaidi wakiwemo wa Daesh wamehatarisha amani na uthabiti wa eneo

No comments:

Post a Comment