Sunday, September 25, 2016

KIKWETE APIGIWA CHAPUO UWENYEKITI WA UMOJA WA AFRICA (AU)

MWANA DIPLOMASIA Mashuhuri barani Afrika, ambaye pia ni Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ana uwezekano mkubwa wa kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika (AU) endapo Tanzania itakubali kumuunga mkono kwenye kinyang’anyiro hicho.

Mwanadiplomasia Mashuhuri Afrika na
Rais Mstaafu wa Tanzania Dr. Jakaya Kukwete


AU inatarajiwa kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti wa AU Januari mwakani, baada ya kushindikana kupatikana kwa mshindi miongoni mwa watu watatu waliojitokeza kuwania nafasi hiyo hapo awali. Waliochukua fomu na kujitokeza hapo awali ni Makamu wa Rais wa zamani wa Uganda, Dk. Specioza Kazibwe, Waziri wa Mambo ya Nje wa Botwana, Pelonomi Venson-Moitoi na Agapito Mokuy kutoka Guinea ya Ikweta.

Hata hivyo, vyanzo vya kuaminika vinasema kuwa viongozi wa Afrika sasa wako tayari kumpa Kikwete nafasi hiyo endapo tu nchi yake itakubali kumuunga mkono katika mchakato huo. Katika uchaguzi wa kwanza uliofanyika Kigali, Tanzania pamoja na nchi nyingine za Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) zilimuunga mkono Moitoi.



Kwa mujibu wa gazeti maarufu la Botswana, Sunday Standard, viongozi wa SADC sasa wamegawanyika baada ya kuonekana kwamba Kikwete ana nia ya kuwania nafasi hiyo; akionekana kuwa na uwezo mkubwa wa kushika wadhifa huo kuliko washindani wake.
Likinukuu vyanzo mbalimbali vya kidiplomasia, gazeti hilo limedai kwamba zaidi ya ujio wa Kikwete, jambo jingine lililomharibia mtarajiwa huyo wa SADC ni habari zilizoibuka hivi karibuni kwamba mgombea huyo sasa anaungwa mkono na Marekani.

“Kuna baadhi ya nchi wanachama wa SADC kwa kupitia njia zao za kijasusi zimedaka taarifa za kiintelijensia jijini Gaborobe kwamba Moitoi ndiye kipenzi cha Wamarekani. Kuna nchi kama Zimbabwe na Lesotho hazitaki kusikia mtu anatumika na Marekani. Hiki ni kikwazo kwa Moitoi.
“Kuna shaka kuwa Venson-Moitoi atakuwa kibaraka wa Marekani barani Afrika kwani zipo taarifa kuwa nchi hiyo imemuahidi mgombea huyo kuwa itamsaidia kifedha kwenye kampeni yake ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa AU,” limeandika gazeti hilo.

Katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Julai mwaka huu jijini Kigali, Rwanda, nchi wanachama wa Umoja wa Kiuchumi wa Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wenye nchi 15 haukupiga kura kwa kile kilichoelezwa kuwa haukuona kama kuna mgombea makini miongoni mwa watatu hao wa kwanza.

Vyanzo vya kuaminika vinasema kuwa viongozi wa Afrika Magharibi wanamuunga mkono Kikwete; huku Rais wa Senegal, Macky Sall, akitajwa kuwa mmoja wa waungaji mkono wake wa wazi.

Viongozi wengine wa Afrika ambao tayari wanafahamika kwa kuunga mkono Uenyekiti wa Kikwete ni Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Mfalme Mswati wa Swaziland, Rais Ali Bongo wa Gabon, Mugabe, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Rais Muhamadu Buhari wa Nigeria na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.

Kwa sababu nchi za ECOWAS hazikupiga kura Kigali, ndiyo sababu akina Moitoi walishindwa kupata kura za kutosha kuweza kushinda nafasi hiyo.

Pamoja na uungwaji mkono huo wa Kikwete, hadi mwezi uliopita Tanzania ilikuwa ikimuunga mkono mgombea wa SADC, Venson-Moitoi na hakuna taarifa mpya zilitolewa na serikali kama imebadili msimamo wake.

Mpaka sasa Rais huyo mstaafu hajachukua fomu na taratibu za kuwania nafasi hiyo zinataka mtu achukue fomu kwanza.


Dr. Jakaya Kikwete akizungumza na Rais Barack Obama
na mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama
cha Democratic Bi Hillary Clinton Ikulu mjini Washington

Kikwete ni miongoni mwa wanadiplomasia mashuhuri katika duru za AU ambapo mwaka huu aliteuliwa kuwa Mwakilishi wake maalumu katika mgogoro unaoendelea hivi sasa nchini Libya.
Kwa vile sehemu kubwa ya shughuli za AU zinafadhiliwa na nchi wahisani, Mwenyekiti wa chombo hicho anatakiwa kuwa mtu ambaye ana uhusiano mzuri na wahisani na mwenye uwezo wa kuzungumza nao na wakamsikiliza; sifa ambazo inaelezwa kuwa Kikwete tayari anazo.

Sunday, September 18, 2016

Fahamu maua ya rosela na faida zake.

Rosela ni ni maua yanaoteshwa au kupandwa mazingira ya kawaida haswa nyumbani, maua haya   yanapatikana kirahisi katika nyumba za ndugu, jamaa na marafiki na sehemu zinginezo japo kuwa baadhi ya watu huyaita maua damu



MATUMIZI YA ROSELA NA FAIDA ZAKE  KWA BINADAMU
Maua ya rosella utengenezwa juisi inayo  ongeza damu mwilini kwa haraka

Hutumiwa kama mboga na mbegu zake hutoa mafuta yanayo tumika kama dawa ya vidonda
Dawa ya magonjwa mbalimbali kama kushusha presha, sukari, uric acid mwilini, inatibu kikohozi na mafua, ina punguza mwili pia hutengeneza ngozi na kuifanya iwe laini
Maua ya rosela hutumika kutengenezea juisi , chai ,jam, pia hutumiwa kama rangi ya chakula



MAMBO MENGINEYO KUHUSU MAUA HAYA
Maua ya rosella yana vitamin C,A,D B1,B2,calcium,magnesium,iron, nk

PENDEKEZO
Kulingana na matumizi na faida za  maua ya rosella ni vyema kupanda kwa wingi maua haya katika mazingira ya nyumbani kama ya navyo pandwa maua mengine ili iwe rahisi kuyapata pindi yanapo hitajika.

Friday, September 2, 2016

UJUE MMEA UNAOITWA BANGI

Bangi ni nini? Bangi ni mmea wenye rangi ya kijani, ambayo hutoa majani. Maua na mbegu zake hutumika kama kilevi. Bangi inastawi karibu maeneo yote hapa nchini na inatumika kwa wingi ikilinganishwa na dawa nyingine za kulevya. Takwimu zilizopo zinaonesha kwamba mmea huo hulimwa na hupatikana kwa wingi katika mikoa ya Mara, Iringa, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Tabora, Tanga, Kagera na Mbeya.

Bangi hutumiwa zaidi na vijana na imepewa majina mengi kama vile msuba, ganja, jani, stiki, ndumu, kaya, msokoto na kadhalika.


Madhara ya bangi:
Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya inaelezea athari za bangi kupitia kijarida chenye ujumbe usemao, “Dawa za Kulevya Zisitawale Maisha Yetu.” Kijarida hicho kimezitaja athari nyingi zitokanazo na matumizi ya bangi.

Athari na madhara mbalimbali ya bangi ni pamoja na kuumwa koo, kupata kikohozi, macho kuwa mekundu na saratani ya mapafu. Pia madhara mengine yatokanayo na matumizi ya bangi ni kuathirika kwa mfumo wa uzazi, ikiwa ni pamoja na kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na taahira ya akili pamoja na mabadiliko ya hedhi kwa wanawake.


Athari nyingine ni pamoja na kuchanganyikiwa, kufanya ukatili, ukorofi, uhalifu na kupungua kwa kinga ya mwili. Madhara mengine makubwa kwa watumiaji wa mmea huo ni kupoteza kumbukumbu, uoni hafifu hadi kutoona kabisa, ukosefu wa umakini wa kusikia na kufanya maamuzi, na kuhisi vitu visivyokuwepo sambamba na utegemezi na usugu. Athari ya bangi kwa wajawazito ambao ni watumiaji ni kuharibika kwa mimba, kuzaa mtoto njiti, kuzaa mtoto mwenye mtindio wa ubongo na matatizo ya ukuaji.



Pia watumiaji wa bangi huridhika na hali duni waliyo nayo, hivyo kukosa mwamko wa maendeleo huku hali ya kuchanganyikiwa ikimfanya ajihisi ni mwenye mafanikio makubwa! Hivyo mvutaji wa bangi hubakiza moshi mwingi kwenye mapafu kwa muda mrefu na moshi huo unapoingia kwenye mapafu hutengeneza kitu kama lami ambavyo huganda na kuathiri utendaji wa kazi wa mapafu. Kijarida hicho kinasema bangi ina kemikali ‘sumu’ inayosababisha saratani zaidi.
Bangi imeelezwa pia kwamba hufanya mishipa ya ubongo kusinyaa, hali inayosababisha kupungua kwa uwezo wa kufikiri na kukumbuka.