Thursday, August 11, 2016
MAAMBUKIZI SUGU YA NJIA YA MKOJO
Maambukizi Sugu ya Njia ya Mkojo (Chronic UTI) ni Nini?
Njia ya mkojo ni sehemu ya mfumo wa mkojo wenye ogani mbalimbali kama figo, urethra (mirija inayobeba mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu cha mkojo.
Yapo maambukizi ambayo hayatibiki kwa urahisi au yanajirudia mara kwa mara licha ya kutibiwa. Maambukizi sugu ya njia ya mkojo (Chronic Urinary Tract Infections (UTIs) ni miongoni.
Njia ya mkojo ni sehemu ya mfumo wa mkojo wenye ogani mbalimbali kama figo, urethra (mirija inayobeba mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu cha mkojo).
Maambukizi kwenye njia ya mkojo yanaweza kutokea sehemu yoyote katika mfumo huu. Ikiwa maambukizi yataathiri kibofu cha mkojo peke yake ni rahisi kutibika lakini yakisambaa mpaka kwenye figo, mwathirika huumwa zaidi na pengine kulazwa hospitali.
Ingawa maambukizi ya njia ya mkojo yanaweza kumpata mtu yeyote kwa wakati wowote, sanasana wanawake. Utafiti wa National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases (NIDDK) inakadiria kuwa katika kila wanawake watano, mmoja ana maambukizi sugu ya njia ya mkojo yanayojirudia mara kwa mara.
Kinachoongeza hatari ya maambukizi sugu ya njia ya mkojo
Maumbile: Maambukizi sugu ya njia ya mkojo huwapata sana wanawake kutokana na maumbile yao.
Kwanza, urethra yao ipo karibu sana na puru (rectum) hivyo kurahisisha bakteria kutoka kwenye puru kuingia kwenye urethra hasa wakati wa kutawaza. Mara nyingi hutokea endapo mhusika atajisafisha kwa kurudisha mkono kutoka nyuma kwenda mbele. Watoto wadogo wa kike hupata maambukizi ya UTI kwa kuwa hawaijui kanuni hii.
Pili, urethra ya mwanamke ni fupi zaidi ikilinganishwa na ya mwanaume. Bakteria wana umbali mfupi wa kusafiri kufika kwenye kibofu cha mkojo ambako wanaweza kuzaliana na kuongezeka kiurahisi na kusababisha maambukizi.
Aina ya Maisha: Kuna aina ya maisha ambayo yanaweza kukufanya uwe kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi kwa urahisi. Kwa mfano kutumia diaphragm (mpira laini maalumu unaowekwa ukeni wenye kizibo cha kuzuia mbegu za mwanamme kupenya ili kukutana na yai la mwanamke) inaweza kusukuma juu urethra na kufanya iwe vigumu kutoa mkojo wote baada ya kukojoa. Mkojo unaobaki kwenye kibofu huongeza uwezekano wa bakteria kuzaliana na kusababisha maambukizi.
Vilevile, matumizi ya vitu vyenye kemikali kuosha uke vinavyoua bakteria walinzi wa kwenye uke, kama sabuni, marashi au viua mbegu za kiume (spermicides). Pia, kunywa dawa za kuua bakteria mwilini huweza kuua walinzi kwenye uke. Hii inaweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi sugu ya njia ya mkojo.
Kukoma hedhi: Kukoma hedhi husababisha mabadiliko ya homoni ambayo mwisho husababisha kubadilika kwa hali ya bakteria walinzi ndani ya uke hivyo kufanya wafe kwa wingi na uke kukosa ulinzi na kufanya iwe rahisi kupata maambukizi ya njia ya mkojo mara kwa mara.
Aina za maambukizi ya UTI
Maambukizi ya njia ya mkojo husababishwa na bakteria ambao mara nyingi huingia kwenye mfumo wa mkojo kupitia urethra na kisha kuzaliana na kuongezeka zaidi kwenye kibofu cha mkojo. Ili kuelewa zaidi maambukizi haya namna yanavyotokea ni vizuri kugawanya maambukizi katika kibofu cha mkojo na maambukizi katika urethra.
Maambukizi katika kibofu cha mkojo (Cystitis) mara nyingi husababishwa na bakteria waitwao Escherichia coli. E.coli ni bakteria wanaoishi kwenye utumbo wa watu na wanyama wenye afya nzuri. Bakteria hawa wakiwa mahala pao hawana madhara, isipokuwa wakipata upenyo wa kutoka huenda njia ya mkojo na kusababisha maambukizi.
Mara nyingi hutokea pale mabaki ya kinyesi yasiyoonekana yanapoingia kwenye njia ya mkojo.
Kushiriki ngono ya kinyume na maumbile kunaongeza hatari ya kupata maambukizi ya UTI.
Maambukizi katika urethra (Urethritis) yanaweza kusababishwa na E.coli au magonjwa na maambikizi ya zinaa au yanayofahamika Sexually Transimitted Infections (STI) kama pangusa, kisonono au klamidia. Hata hivyo, magonjwa na maambukizi haya ya zinaa mara chache husababisha maambukizi ya njia ya mkojo.
Dalili za Maambukizi sugu ya UTI
Kwa mtu anayehisi maumivu chini ya kitovu au kwenye kibofu cha mkojo au mara kwa mara, kukojoa mkojo uliochanganyika na damu ni dalili za wazi za maambukizi haya.
Dalili zingine ni kutoa mkojo mzito, kuhisi kuchomwa au maumivu wakati wa haja ndogo na maumivu kwenye figo yaani chini ya mgongo au mbavu.
Ikiwa maambukizi yatasambaa hadi kwenye figo, yanaweza kusababisha kichefuchefu, kutapika, baridi, homa kali (zaidi ya nyuzi joto 38.3), uchovu na kuchanganyikiwa.
Mara nyingi, dalili hizi hutofautiana kati ya watoto na watu wazima. Umakini unahitajika kumbaini mtoto mwenye maambukizi haya.
Wakati gani wa kumuona daktari?
Mwanzoni, dalili za maambukizi ya njia ya mkojo zinaweza zisiwe zenye maumivu makali lakini baadaye yakawa makali kiasi cha kutovumilika na kuathiri shughuli za kila siku.
Ikiwa dalili zitakuwapo kwa zaidi ya siku tano, inashauriwa ni vyema ukamuona daktari. Pia, muone daktari haraka ikiwa mwili utachemka sana, ikiwa una mimba au kisukari.
Ikiwa una maambukizi sugu ya njia ya mkojo hii ina maana ulikuwa na maambukizi ambayo hayakutibiwa ipasavyo. Madaktari huwatuma wateja wao maabara kwa ajili ya vipimo zaidi kubaini ni maambukizi ya aina gani. Wataalamu wa maabara huangalia mkojo kupitia hadubini ili kuona bakteria wanaosababisha maambukizi.
Kuotesha mkojo (urine culture test) ni kipimo kingine kinachoweza kufanywa na wataalamu wa maabara ili kubaini aina mahususi ya bakteria aliyemshambulia mgonjwa husika na mara nyingi hurahisisha uchaguzi wa dawa kwa daktari anayetoa tiba. Kipimo hiki huchukua siku moja mpaka tatu kabla majibu kutoka.
Ikiwa daktari atahisi kuna uharibifu wa figo uliosababishwa na maambukizi hayo atapendekeza vipimo zaidi vya figo kama X-ray na Ultrasound. Kama una maambukizi yanayojirudia mara kwa mara daktari anaweza kufanya kipimo cha cystoscopy kinachohusisha mpira mrefu wenye lenzi mwishoni unaotumika kuangalia urethra na kibofu cha mkojo. Daktari anaweza kuangalia pia tofauti za kimaumbile alizonazo mwanamke zinazosababisha kujirudia kwa maambukizi.
Madhara ya muda mrefu ya UTI
Maambukizi sugu ya njia ya mkojo yanaweza kusababisha madhara kwenye figo. Ugonjwa wa figo husababisha kuharibika kwa figo yenyewe na kwa watoto wadogo, kusambaa kwa bakteria kwenye damu (septicaemia). Kwa wajawazito huongeza hatari ya kuzaa watoto njiti endapo hautakabiliwa kwa wakati.
Kujikinga na UTI
Kojoa mara nyingi uwezavyo muda wowote unapojihisi kufanya hivyo.
Wakati wa kutawaza, safisha kwa kupeleka mkono nyuma.
Kunywa maji mengi kusafisha bakteria kwenye njia ya mkojo kila mara unapokojoa bila kusahau kuvaa chupi iliyotengenezwa kwa pamba.
Epuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana na kutumia diaphragm kama njia ya uzazi wa mpango.
Tumia mafuta ya kulainisha wakati wa tendo la ndoa ikiwa inawezekana ili kuondoa michubuko isiyo ya lazima yenye kufanya upenyo wa bakteria.
Kwa wanawake, epuka kuoga ndani ya mapovu mengi kwa kuwa kemikali zilizopo kwenye sabuni huingia kwenye uke na kuua bakteria walinzi hivyo kufanya iwe rahisi kupata maambukizi.
Kwa wanaume, ikiwa haujatahiriwa osha vizuri uume wako mara kwa mara baada ya haja ndogo au tendo la ndoa
MSOMALI AGOMBEA UBUNGE MAREKANI
Mwanamke mmoja aliyezaliwa Somalia lakini sasa ni mpiganiaji haki za kibinadamu Ilhan Omar anapigiwa upatu kuweka historia kuwa Mmarekani wa kwanza mzaliwa wa taifa hilo la Afrika Mashariki kuchaguliwa kuwa mbunge nchini Marekani.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 33 amemuangusha mbunge aliyehudumu kwa zaidi ya mika 44 katika bunge la jimbo la kwa chama cha Democratic .
Mbunge huyo wa zamani bi Phyllis Kahn amekuwa akiiwakilisha DFL, kinachoshirikiana na chama cha Democratic .
Bi Omar, na familia yake walitoroka mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia kwenda Kenya walikoishi kwa miaka minne kabla ya kwenda Marekani.
Huko walihamia eneo lenye wasomali wengi la Cedar-Riverside, katika jimbo la Minnesota.
Kizingiti kilichosalia mbele ya bi Omar ni mpinzani wake wa chama cha Republican Abdimalik Askar, ambaye pia ni msomali raia wa Marekani katika uchaguzi mkuu ujao ulioratibiwa kufanyika mwezi Novemba.
Hiyo inamaanisha iwapo kila hali itasalia ilivyo basi Msomali mmoja raia wa Marekani atakuwa bungeni mwakani.

Wednesday, August 10, 2016
"ISIS is honoring president Obama,"-Donald Trump
Donald Trump made a startling accusation against President Barack Obama during a Florida rally Wednesday night, telling supporters that the commander in chief is the "founder of ISIS."
"ISIS is honoring president Obama,".
The Republican presidential nominee said during a rally at BB&T Center in Sunrise, Fla. "He is the founder of ISIS. He founded ISIS. And, I would say the co-founder would be crooked Hillary Clinton.
Trump's declaration was met with chants of "Lock her up!" from rally-goers.
In addressing Obama, Trump included the president's middle name, calling him Barack Hussein Obama -- a move that's typically been employed by those who claim Obama is secretly a Muslim.
"Radical Islamic terrorism," Trump said. "And people don’t like saying that. Our president refuses to use the term. Every time another event happens, I keep saying, I wonder if he’s gonna say it this time. And he doesn’t say it."
He also took aim at Clinton, for her refusal to use the term. "And Hillary won’t say it either," he said. "She doesn’t wanna say it, cause she doesn’t wanna offend the president, because then bad things could happen to her if she offends the president. Bad things could happen to her. So she’s afraid to say it. Hillary’s afraid to say it. She did say that she would say it because of me, but she’s afraid to say it. But, we have a real problem with radical Islamic terror. It's’ what it is. It’s terror."
"ISIS is honoring president Obama,".
Republican presidential candidate Donald Trump |

Thursday, August 4, 2016
Kujua lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Na Sadiq M. Sadiq. (Gazeti la Annur
Haya ni maelezo ya wazi kwa watu (wote na uongozi na mauidha kwa wamchao (Mwenyezi Mungu). Na kwa yakini tumeifanya Qur-an iwe ni nyepesi kufahamika lakini yuko anayekumbuka" (54:17).
"Kitabu kinachopambanuliwa aya zake ni kisomi (kikilichoteremka) kwa lugha ya Kiarabu kwa wanaojua kheri. Kitoacho habari njema na kionyacho lakini wengi katika wao wamekengeuka kwa hiyo hawasikii" (54:3-5).
Aya zilizotangulia hapo juu bila shaka zinajieleza wazi hazihitaji ufafanuzi wa kina. Mwenyezi Mungu (s.w) kateremsha Qur-an kama ni mwongozo.
"Tukasema shukeni humo nyote na kama ukikufikieni mwongozo utokao kwangu, basi watakaoufuata mwongozo wangu haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika" (2:38).
"Hivyo Qur-an ni mwongozo kwa wamchao Allah (s.w)" (2:2).
Allah (s.w) ameteremsha Qur-an kwa watu wote lugha zote hivyo watu wataifahamu Qur-an kama mwongozo wao kwa lugha wanayoielewa wao.
Na Qur-an haina maana ni kitabu tu bali ni uongozi kamili kwa wanaomcha Allah (s.w) utakuta humo maonyo. Mawaidha, rehema, n.k. Hivyo ujumbe uliomo ndani yake ndio hitajio la watu kama aya zote nilizozitaja hapo juu zinavyojieleza wazi. Sasa inachoshangaza kukuta mtu anadai kwamba huwezi ukaisoma Qur-an mpaka ujue kiarabu, kwa maana nyingine huwezi kuongozwa na Qur-an mpaka ujue kiarabu.
Pili, huyo huyo mtu anaedai mtu anasimama katika mimbari hali ana Uislamu wa Kimarekani kwa kuwa amevaa suruali aina ya jeans au suti na tai na pia anaongea kingereza mtu wa aina hiyo ana Uislamu wa Kimarekani.
Nianze na la kwanza. Ni kweli kwamba huwezi kufasiri Qur-an mpaka utimize masharti yake na moja ya sharti ni kujua lugha ya Kiarabu. Lakini kuwa mimi nisiefahamu Kiarabu siwezi kusoma Qur-an ama siwezi kuongozwa na Qru-an hii si kweli kwa sababu japo Qur-an imeteremshwa kwa lugha ya Kiarabu haiitaji lugha bali mwongozo. Hivyo mwongozo humwongoza mtu kwa kuelewa hiki ni nini na hiki ni nini.
Kiarabu ni lugha ya Mtume (s.a.w) ndio maana Allah akamteremshia kwa lugha hiyo na kama Mtume (s.a.w) angekuwa msukuma basi Qur-an ingeshuka kwa lugha ya kisukuma ili wale wanaoteremshiwa wapokee kwa lugha wanayoifahamu ndio maana Mtume (s.a.w) alituma baadhi ya maswahaba wake ili wajifunze lugha zingine kusudi kubwa lilikuwa ni mawasiliano pamoja na kuwafikishia ujumbe wa Allah (s.w) kwa lugha wanayoielewa wao.
Si lengo langu kupinga Waislamu wasijifunze Kiarabu la. Nia yangu wale wanaoifahamu Qur-an kwa maana wanaofahamu ujumbe uliomo ndani yake basi wawafikishie wengine kwa lugha wanayoielewa. Ajabu huyo anaedai huwezi kusoma Qur-an mpaka ujue Kiarabu anatumia aya za duniani kisha anatafsiri kwa lugha ya kiswahili halafu anawambia wengine hawataifahamu au wajue Kiarabu.
Ni vizuri wewe unaeijua watungie watu vitabu kwa lugha wanazofahamu ili iwe rahisi kwao kuelewa ujumbe uliomo kuliko kuwakatisha tamaa kabisa kuwa mpaka wafahamu Kiarabu ndio wajue huku ni kuturudishia maendeleo yetu nyuma.
Wawepo wasomi, katika jamii wataozama katika elimu ili watufahamishe misingi ya Uislamu katika lugha tunayoielewa. Hamwezi wote kuwa watabibu, wanasayansi, wanasiasa, wachumi n.k., lakini wachache wakifahamu watakidhi mahitaji ya wengi. Hivyo si wote wataifahamu Qur-an katika lugha yake ya asili lakini ikifanywa juhudi ya kuitafsiri katika lugha mbalimbali kama ambavyo ilivyo hivi sasa watu watafahamu kulingana na lugha zao. Mswahili, mwingereza, mmasai, mnyamwezi n.k., wote hao wakifikishiwa ujumbe kwa lugha wanazozielewa itakuwa ni busara sana. Kwa kuwa Allah (s.w) anasema Qur-an ni nyepesi kufahamika yaani miongozo yake inakubaliana na akili ya mtu ni wajibu kuifikisha kwetu japo si kwa lugha ya Kiarabu. Maadamu Qur-an inatafsirika kwa lugha zote basi wanazuoni ndio wenye jukumu la kuifasiri katika lugha mbali ili iweze kuwafikia walengwa.
Pili, kwamba kuna Uislamu wa Kimarekani. Sasa yule anaedai kwamba mvaa jeans au suti kisha akasimama katika membari na huku akitoa mawaidha akichanganya na kingereza kwa mtazamo wa mtu huyo, huyo ni Muislamu wa Kimarekani. Kwa uoni wangu madai ya mtu wa aina hii si yenye upeo na bado hajafahamu kuwa Qur-an ni mwongozo. Na kama anafahamu Qur-an kuwa ni mwongozo basi fikra zake zinamtuma kuwa wanaoongozwa ni wavaa kanzu, vilemba, hajari akiwa na tasbihi (shanga) ndefu kama mtu huyo ndie ataeongozwa na Qur-an.
Fikra ya aina hii si ya msomi na kama ni msomi basi ni msomi wa lugha na sio Qur-an ndio maana madai yake yanalenga kujua lugha ndio ujue Qur-an. Mfano mimi nimesilimu kutoka ukristo na kuingia Uislamu itakuwaje basi mpaka nijue lugha ndio nijue mwongozo? Kwa maana hiyo wanaosoma mfano, Tafsiri ya Qur-an ya Abdallah Farsy hawajui Qur-an kwa kuwa lugha imewatupa mkono.
Vivyo hivyo anaevaa jeans atakapoelewa kwamba Qur-an ni mwongozo vipi asiongozwe kwa kuwa amevaa jeans? Watu wa namna ya huyu wanataka Uislamu wa Saudi Arabia wa kanzu, kitu ambacho sicho kinachoupeleka Uislamu mbele. Wapo wanafiki wao hurudisha nyuma maendeleo ya Uislamu, lakini nao utawakuta wamefuga ndevu wamevaa suruali fupi wamenyoa nywele lakini hayo yote ni mapambo ya mwili vitendo ni mnafiki huyu je? Tena na lugha anaijua vizuri sana.
Kwa kifupi Uislamu si kanzu wala kofia bali ni kuukubali moyoni na kuutia katika vitendo kwa lengo la kusimamisha serikali ya Allah (s.w).
Mashariki ya kati vazi lao ni kanzu utakuta mkristo myahudi na mwislamu wote wamevaa kanzu. Kwa hiyo ukidai mvaa jeans ni mwislamu wa kimarekani nasi tutaona mvaa kanzu mwislamu wa saudia au mashariki ya kati kutokana na uvao wake.
Ningeshauri watu wa namna hii wawafunze Waislamu wasiofahamu mwongozo wa Allah (s.w) jinsi ipasavyo Muislamu kutenda na sio kuwakatisha tamaa kwa mavazi, lugha n.k.
"Allah (s.w) anatazama nafsi zetu na matendo yetu, kama yanalingana na mwongozo wake.

UFAHAMU UGONJWA WA MKANDA WA JESHI
MPENZI msomaji wa ukurasa huu wa lishe na tiba za kisuna, leo tuangalie ugonjwa unaojulikana kama mkanda wa jeshi. Tumekuwa tukishuhudia baadhi ya watu wenye ugonjwa huu wakionekana kuwa wana maambukizi ya VVU bila kuwa na uhakika wa afya zao au bila kutambua chanzo sahihi cha ugonjwa wenyewe.
Hali hii imewafanya baadhi ya watu kuamini kuwa mtu mwenye ugonjwa wa mkanda wa jeshi anakuwa na ugonjwa wa UKIMWI jambo ambalo halina ukweli kwa asilimia mia moja kwani sio wote wenye ugonjwa huu wanakuwa na VVU.
Ugonjwa huu kitaalamu unajulikana shingles au herpes zoster ambapo ugonjwa huu husababishwa na virusi aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga. Ugonjwa huu wa mkanda wa jeshi huathiri ngozi ambapo huambatana na vipele na michubuko kama ya kuungua yenye kuambatana na maumivu makali.
Visababishi
Dk Grace Chirwa kutoka Hospitali ya Temeke Dar es Salaam anasema kuwa ugonjwa huu husababishwa na virusi aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga. Baada ya mtu kupatwa na ugonjwa wa tetekuwanga, virusi vya ugonjwa huo hubaki katika hali ya kupooza/ kutokuwa na madhara katika baadhi ya neva mwilini.
Baada ya kukaa mwilini kwa miaka kadhaa, iwapo kinga za mwili zitashuka kwa sababu yoyote virusi hawa hupata nguvu na kuwa imara jambo linalopelekea kutokea kwa ugonjwa wa mkanda wa jeshi. Ugonjwa huu unapotokea ni mara chache sana ugonjwa huo kujirudia mara ya pili kwa maisha ya mtu huyo.
Vihatarishi
Ugonjwa huu unaweza kumpata mtu wa umri wowote ingawa watu wa makundi fulani wanakuwa katika hali ya hatari zaidi kupatwa na ugonjwa huo.
Makundi ambayo yapo kwenye hatari zaidi ni watu walio na umri wa zaidi ya miaka 60, mtu aliyewahi kuugua ugonjwa wa tetekuwanga kabla ya kufikisha umri wa mwaka mmoja.
Pia watu ambao kinga zao za mwili zimepungua kwa sababu zozote zile ikiwemo mwenye maambukizi ya HIV, saratani pamoja na utapiamlo:
Licha ya hiyo ugonjwa huu hauambukizwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kama yalivyo magonjwa mengine. Inapotokea mtoto au mtu mzima ambaye hajawahi kupata ugonjwa wa tete kuwanga au kupata chanjo yake akakutana na mgonjwa wa mkanda wa jeshi, mtoto huyo au mtu huyo anaweza kuugua ugonjwa wa tetekuwanga na siyo mkanda wa jeshi.
Dalili
Dk Chirwa anasema kuwa dalili ya awali kabisa ya mkanda wa jeshi ni maumivu makali sehemu fulani/ upande mmoja wa mwili yanayoambatana na hali ya ganzi na hisia za kuungua kwenye ngozi.
Maumivu hayo pamoja na hisia hizo za kuungua hutokea kabla ya vipele/ michubuko kutokea kwenye ngozi.
Kawaida ya dalili hizi za vipele au michubuko huusisha eneo fulani la mwili hasa kuanzia kwenye uti wa mgongo kuzunguka kuelekea eneo la tumbo au kifua. Michubuko pia inaweza kutokea kwenye maeneo yanayozunguka uso, macho, midomo au masikio.
Dalili nyingine za ugonjwa huu ni maumivu ya tumbo, homa, maumivu ya mwili mzima, kuwa na vidonda sehemu za siri, kuwa na maumivu katika sehemu za kichwa, kuwa na maumivu ya viungo, kuvimba kwa tezi pamoja na tatizo la kutoona iwapo neva za maeneo ya uso zimeathirika.
Vipimo
Ni mara chache sana kufanya vipimo kwa ajili ya kutambua ugonjwa huu, isipokuwa kwa nchi zilizoendelea. Kwa ujumla utambuzi wa ugonjwa huu hufanyika kwa kuangalia historia ya mgonjwa na kuchunguza sehemu ya ngozi iliyoathiriwa. Pia vipimo vya damu FBP huonesha ongezeko la chembe nyeupe za damu.

Subscribe to:
Posts (Atom)